Ndiyo. Wakati wetu waliokuwa wanafeli pale walikuwa wanatafutiwa shule nyingine zilizokuwa zinalingana na speed yao ya kusoma maana pale Maua workload ya masomo ilikuwa kubwa - masomo 12 + vocational training. Halafu tulikuwa na "sauna bath", swimming pool na kilikuwa kituo cha wale wanaopanda mlima Kilimanjaro. Hata wanafunzi walikuwa wanahimizwa kupanda mlima Kilimanjaro. Wakati ule theruji ilikuwa inafunika mlima mzima hadi chini. Eti siku hizi kamebakia kakibandiko keupe tu pale juu. Maua ilikuwa ina provide nguo za kujikinga na baridi, viatu, groves na vifaa vingine vya kupandia mlima Kilimanjaro. Tulikuwa pia tunafanya study tours kule West Kilimanjaro na Mombasa, Kenya + michezo + English debate na sekondari mbalimbali za Kilimanjaro. Sidhani kwa wakati wetu kulikuwa sekondari ambayo hatukwenda, vyuo na mahoteli kwa ajili ya kuandika study project paper Form IV.
Kwa vile Maua iko kijiji cha mwisho kabisa kabla ya kufika kwenye msitu wa Mlima, Padri Ladislaus alipenda sana huo msitu na tulikuwa tukienda kupanda miche mingine ya miti ya asili. Nasikia miti ilipokua vizuri na msitu ukapendeza, vigogo walimzuia asihusike na chochote kule msituni na wakaanza kuuvuna. Nadhani walio Maua sasa hivi wanaweza kutuzuja kama ule msitu umeshageuka mbuga au la maana nasikia vigogo walianza kuvuna miti!