Hongera mheshimiwa rais kwa ku "host" mkutano wa nishati Africa

Hongera mheshimiwa rais kwa ku "host" mkutano wa nishati Africa

pombe kali

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2014
Posts
282
Reaction score
561
Kwa kweli, mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni. Kitendo cha marais wa Afrika kuiamini Tanzania na kuja kufanya mkutano ni dhamana kubwa sana ambayo alikuwa nayo Amiri Jeshi Mkuu.

Tuache chuki, tofauti zetu tuzizike, tumpe maua yake Mheshimiwa Rais kwa kuwa mwenyeji wa mkutano huu mkubwa. Siyo rahisi wala siyo kitu kidogo—marais wanatoka nchi zao zenye fujo, vita, na amani pungufu, wanakuja huku na kuondoka bila rabsha yoyote.

Kama unakumbuka, mwaka 1994, marais wa Rwanda na Burundi walipata ajali ya anga wakiwa wanatokea hapa nchini, na tukio hilo lilisababisha vita vya kimbari vilivyoangamiza takriban watu laki moja.

Kitendo cha mkutano wa Nishati Safi kufanyikia hapa Tanzania kinamaanisha kuwa nchi imeaminika kama sehemu salama, na hili limejidhihirisha baada ya mkutano kuisha salama, kila mmoja akirejea makwao bila rabsha.

Mungu akupe nguvu, busara, na hekima katika kazi hii ngumu, Rais wangu.
 
Washirika wa umoja wa Mataifa kama Wadhamini,leo Unaambiwa Wanajitoa ndio utajua hujui..
 
Kwa hili,Lazima tumpongeze Mama kwa Juhudi aliyofanya
Team Samia tunasema,2025 Tunaenda na Mama,Ushindi lazima.
 
Kwa hili,Lazima tumpongeze Mama kwa Juhudi aliyofanya
Team Samia tunasema,2025 Tunaenda na Mama,Ushindi lazima
 
Back
Top Bottom