Hongera Millard Ayo: Afungua Kituo cha kurusha mawimbi ya redio

Pasco huwa unakujaga huku,?
Snowhite na Corleone, ni kweli yule jamaa yangu wa PPR, anatengeneza vipindi vya redio, TV na matangazo na kuvirusha vituo mbalimbali vya redio na TV. Bongo tuna production houses nyingi sana, na watangazaji wakongwe karibu wengi tunajitegemea!.

TCRA walipoyatangaza makampuni 4 tuu ndio yatakayorusha digital signals za TV, yaani multiplex operators ambao ni Star Media wenye king'amuzi cha Star times, Agape Associates wenye king'amuzi cha Ting, ITV yenye kingamuzi cha Star TV yenye king'amuzi cha continental, tulidhani sasa ndio unafuu, na TCRA wakaweka gharama za kurusha matangazo kwa saa nzima kwa mwezi mzima ni US $ 3,000 tuu, hivyo kila production house ingeweza kurusha channel yake!, kumbe tumepigwa changa la macho!, ili kurusha matangazo kwenye hivyo ving'amuzi lazima uyafikishe mwenyewe kwenye satelite ndipo wao wa pick na kukurushia!, hivyo wengi tunashindwa!, tumebakia kuwapelekea vipindi tuu na kuwalipa wao wavirushe tena bei ya juu.

Kitendo alichokifanya dogo Millard Ayo ni cha kustahili pongezi sana!.

Pasco
 


Uchawi wako usifikie kuua albino
 


Ahsante sana kaka!!
Msalimie jamaa yako yule!!
 

Mkuu asnte kwa kuliweka sawa hili
Pia wapo wengi hasa upande wa TV wanaofanya hivi vitu kina AY na Salama Mkasi TV, Mboni Masimba The Mboni Show
 
Last edited by a moderator:
Nyota njema inaonekana alfajiri, the next Kusaga is on his way.
 

Kwakweli Milard Ayo ni mmoja wa watangazaji ninao wakubali sana tena sana ..ana juhudi ana heshima na anajali sana kazi zake!
Hakika hii ni hatua kubwa sana tena sana bila shaka ataanz kutengeneza matangazo kwa kutumia studio yake na hili litamuongezea kipato!

Hili ndilo watangazaji wanatakiwa wafanye si kulalamika una lipwa kidogo..hakuna anaye kuajiri ili akutajirishe bali umtumikie na kumtajirisha! Lazima watangazaji wfafate nyayo zake!

Hakika namuona mbali sana Milard Ayo hakika kanifurahisha.
 
Santeeeeeeeeee!!
 
Isikamatwe tena!! Wewe soma page ya tatu hapo uone!!

Uchawi hawezi kuisha humu!!

Eti kapewa studio Na Ridhiwani!!

Teh Teh hii nchi ngumu sana kuishi..kuna kipindi Milard Ayo alishalalamikiwa hapa kuwa hatumii vizuri kipaji chake na ikiwezekana arudi shule na mimi niliona kabisa ni kweli Milard ana hitaji kufanya kitu juu ya sauti yake na kipaji alicho nacho.

Lakini cha kushangaza kaanza kupiga hatua tulitakiwa kumpongeza lakini watanzani wana mgeuka tena na kuanza kumzodoa na kumkatisha tamaa.

Nchi ngumu sana hii
 
Ritz na mafisadi kwa mshahara upi watangazaji wabTanzania anaolipwa hembu dadavueni kwamapana kipindi hichi cha kuelekea uchaguzi tutaona mengi.

Aisee mauji ya Albino hayawezi kuisha!
Hivi tanzania kuna watangazaji wangapi wameshindwa kupewa hayo unayo tuaminisha?
Ok let say kweli wamempa kwanini tusipongeze maana hawawezi kumpa kama yeye hana wazo hilo! Kwanini tusikubali kuwa amefanya jambo? Hata kama wamempa hakuna shida maana ni watu wengi husaidiwa kujikwamua..Hakuna tatizo kama Milard aliandika proposal na kuomba wafadhili kwa mradi wake!

Hata Nchi yetu na maendeleo tunayo yaona kuna michango ya watu wengine hasa nchi za jirani na Ulaya! Kwa hiyo kusaidiwa haiwezi kuwa hoja ya msingi hapa.
 
Kama umeanza kumsikia milard ayo kwenye amplifaya lazima useme SHIT ila kama umeanza kumskia milard toka wapo radio lazima umpongeze na uamini HARD WORK PAYS
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…