Hongera Mudathir Yahaya

Hongera Mudathir Yahaya

redio

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2016
Posts
5,813
Reaction score
12,921
Mim kama shabiki napenda kutoa pongezi kwa Mudathir kwasababu umeonyesha upambanaji wa haliyajuu japo timu yetu haikua na muunganiko mzuri katika eneo la kiungo. Nakumbuka kunakipindi timu ya Azam ilimtoa kwa mkopo aende Singida United tokea pale alipandisha kiwango chake kiasikwamba amekua tegemeo kwenye timu ya Taifa na ata aliporudi Azam fc.
Mechi yetu na Kenya alipo pumzishwa ilionekana wazi hali ilikua mbaya sana, Viungo wa Harambee Stars walijitawala kama nyani wanavyo jitawala waki ingia kwenye shamba la Mahindi ambalo mwenyewe hayupo.

Napenda pia kutoa pongez kwa wachezaji na benchi la ufundi mmejitahid sana, Timuyetu bado inamapungufu mengi sana yaani mimi binafsi siamini kama katika mechi 3 mngefungwa goli 7. Goli ambazo stars imefungwa ni chache sana na zaki soka katika mashindano ya ngazi ya Afcon. Siandiki kwa kuwasimanga ila uo ndio uhalisia, hatuku pata point ila kwa kuanzia hamkucheza vibaya.

Mim binafsi nilitegemea labda mechi na Kenya tungepata sare ila sijawahi kufikiri tutamfunga Kenya, Timu ilinitia moyo tulivyo waongoza Harambee stars lakini sikua na hakika kama tungeshinda na ushindi ingekua mme tupa kitu cha ziada.
Kenya na Uganda wametuzidi japo si kwa umbali ule wa Mataifa ya Magharib na Kaskazin.
Ninacho washauri wachezaji wetu wanao chipukia wao wafanye juhudi binafsi kuweza kujifunza vitu vinavyo fanywa na wenzetu kwakutumia mitandao mbalimbali, waangalie vijana wa umri kama wao walio katika nchi zilizo endelea kisoka wanafanyaje ili kuboresha viwango vyao. Kwa wale wachezaji wanao tolewa kwa mkopo Mudathir iwe ndio fundisho kwao, amefanya juhudi na zime zaa matunda japo nayeye anatakiwa aongeze juhudi kwakua kama bahati anayo ayuko mbali na mafanikio.Kwasasa akiongeza juhudi kidogo ayuko mbali na level za akina Fabrice Ngoma kiungo wa Vita klabu.

Wachezaji wanao chipukia wasifikirie kabisa kucheza soka hapa nchini kama wanahitaji kufanya mpira ndio maisha yao. Watafute watu wazuri wa kuwa simamia na kuwatafutia nafasi za kucheza vilabu vya nje, Kucheza bongo liwe chaguo la mwisho kabisa kwakua mpira wa bongo umepotea na hauonyeshi dalili za kurudi hivi karibun.
Nawashauri huwezi ukawa unategemea mpira uwe ndio maisha yako ukawa una amka saa 12 asubui uende mazoezin.

Mwanamichezo anaye jitambua ana anza mazoezi binafsi saa 10 alfajir au 10:30 asubui anafanya yeye kama yeye mbaka saa 12 asubui, atapumzika mbaka saa moja asubui ili aanze program za kocha ambazo mara nyingi zinaisha saa 3 asubui. Jioni unatafuta saa moja lingine binafsi kabla kocha hajafika uwanjani.

Kama utafanya mazoez kwa bidii na kuachana na anasa utafanikiwa wenzetu wamefanikiwa kwa kuiga kwa wanaofanya vizur na kujitunza. Huwezi kufanikiwa bila ziada ya mazoezi binafsi, kusoma na kuangalia ratiba za walio fanikiwa.
 
Nadhani pia kuna haja ya viongozi wa soka (TFF) kabla hawajachaguliwa waje na proposal zinazoonyesha watafanyaje kazi.
 
Back
Top Bottom