HOW TO DEAL WITH A ROGUE & CORRUPT INTELLIGENCE AGENCY
1. A PLAY-BOOK FROM PEOPLES REPUBLIC OF CHINA
Hili linalotokea Tanzania liliwahi kutokea Uchina mwaka 2013 baada ya Raisi Xi Jinping kuchaguliwa kuongoza nchi. Duniani kote walitegemea Bo Xilai ndiyo awe Raisi wa Uchina, maana alikuwa na uzoefu wa ujasusi, diplomasia na alikuwa ndani ya MTANDAO wa Raisi Mstaafu Jiang Zemin ulioitwa The Shanghai Clique. Jiang Zemin na genge lake ndiyo walikuwa wameshika rimoti ya nchi na wao ndiyo walikuwa wanaongoza hata wakati Raisi Hu Jintao yupo madarakani.
Ubaya ni kwamba Bo Xilai katika harakati za kutaka kuwa Raisi alitengeneza maadui wengi sana wakiweme Raisi Hu Jintao, Waziri Mkuu Wen Jibao na Makamu wa Raisi Xi Jinping. Jamaa alikuwa na MTANDAO mkubwa ambao ulishikilia vyombo vya habari, lakini kubwa sana alikuwa analiongoza shirika la kijasusi (Ofice 610) ambalo lilikuwa linadukua mawasiliano ya mahasimu wake akiwemo Raisi Hu Jintao. Kiukweli alichezewa mchezo mbaya baada ya kutambulika kwamba mke wake alikuwa na mahusino ya kimapenzi na Jasusi wa MI6, hivyo akafukuzwa uanachama wa CCP.
Mambo yalivyokuwa magumu kwenye chama, ikabidi CCP wamempe Uraisi Xi Jinping mtu ambaye alikuwa hana makundi. Kumbe bwana genge la Jiang Zemin na Bo Xilai halikuridhika na lilikuwa linapanga UHAINI dhidi ya Xi Jinping. Kule kwenye jimbo la Xinjiang na Tibet kuna maelfu ya wanajeshi na makomandoo ambao wamewekwa kuwadhibiti waislamu. Bahati mbaya mno vile vikosi vilikuwa vinaongozwa na mtu mwingine kutoka MTANDAO (The Shanghai Clique)wa Raisi Mstaafu Jiang Zemin aitwaye Zhou Yongkang.
Bo Xilai na Zhou Yongkang walianza kuviondoa vikosi kwa kisingizio cha mazoezi, huku wakishirikiana na wanajeshi majenerali wakubwa tu. Bahati mbaya waliwahiwa mapema na kuwekwa kizuizini. Baada ya hapo Xi Jinping akavunjilia mbali shirika la kijasusi (Office 610) ambalo lilikuwa ndiyo chombo cha genge la Raisi Mstaafu Jiang Zemin kuongoza serikali na kuwaendesha viongozi wa nchi ili kufanikisha dili zake za kifisadi. Jiang Zemin na familia yake nao waliwekwa kizuizini.
Hivi mpaka kufika mwaka 2016, Xi Jinping alikuwa ameshughulikia maafisa usalama na makada wa CCP waliokuwa ndani ya mtandao wa Raisi Jiang Zemin wasiopungua milioni 4 (4,000,000). Angecheza tu, nakwambia wangemuua na Raisi angekuwa Bo Xilai. Huu ndiyo ukweli mchungu.
==============================================
2. A PLAY-BOOK FROM THE USSR
Kule USSR, baada ya Stalin kuwa Raisi alikuwa shirika la kijasusi (The Cheka) limejaa WAYAHUDI ambao walikuwa wafuasi wa Raisi Vladmir Lenin na Leon Trotsky. Stalin alifahamu fika, kwamba ili aongoze nchi vizuri ni aidha yeye aende, au hili genge liende. Akaanzisha THE PURGES, ambapo alianza kusafisha chama (CCCP), shirika la kijasusi la jeshi (The GRU), shirika la kijasusi la chama (COMINTERN), shirika la kijasusi la mambo ya nje (INO) na shirika la kijasusi la kiraia (The Cheka).
Mashirika yote makubwa ya kijasusi ya USSR yalianzishwa na Wayahudi wakiwemo Leon Trotsky na Felix Dzerzhinsky, ambao hawakuwa wanamkubali kabisa Stalin. Mpaka kufika mwaka 1935, shirika la kijasusi (The Cheka) lilikuwa limepunguzwa maofisa 150000, ambao aidha walipigwa risasi za kichwa au walipelekwa Siberia kwenye Gulag. Baada ya hapa, ndiyo Stalin alianza kuongoza nchi kiurahisi hadi kuifanya USSR liwe taifa lenye nyuklia na kuwabagaza Wajerumani.
Stalin aligundua jambo la msingi kabisa: USITEGEMEE SHIRIKA MOJA LA KIJASUSI NDANI YA NCHI. Baadaye akaamua kuunda mashirika mengi ya kijasusi ambayo yalikuwa yanafanya kazi moja na kushindana. Mwishowe haya mashirika yakaundiwa wizara moja ya uratibu iitwayo, THE KGB, ilhali hata hayashirikiani hata kidogo.
==============================================================
3. A PLAY-BOOK FROM REVOLUTIONARY FRANCE
Kule Ufaransa baada ya mapinduzi ya mwaka 1789, wajamaa walitambua jambo moja muhimu kabisa. Hawawezi kutawala endapo wafuasi (The Royalists) wa Mfalme Louis XVI wangeendelea kuwepo. Kabla ya Vatican kuunda mwaka 1929, Ufaransa ndiyo kilikuwa kitovu cha Ukatoliki duniani. Mapadri ndiyo walitumika kuusaidi ufalme kufanya Ujasusi dhidi ya wanamapinduzi (The Jacobins). Baada ya wanamapinduzi kufahamu hili walifanya jambo rahisi kabisa, nyonga mfalme Louis XVI, pamoja na kubomoa mfumo mzima wa kijasusi wa Kanisa Katoliki.
Maxmiliien Robespierre na wenzake wakaanzisha kamati ya usalama wa nchi (Committee of Public Safety) ambapo walianza kushughulika na wote wanaopinga mapinduzi. Maaskofu wakajichanganya wakaanza kupiga propaganda kupinga mapinduzi, eeh bwana eeh, kumbe walikuwa wanatafutiwa sababu. The Committee of Public Safety ilikamata mapadri zaidi ya 30,000 waliokuwa wanashirikiana na serikali ya kifisadi ya mfalme Louis XVI na kuwapiga risasi au kuwanyonga hadharani (Guillotined) ndani ya siku moja.
Baada ya hapo hata Napoleon Bonaparte anashika madaraka, alikuta hakuna upinzani mkubwa kivile na mifumo yote ya kijasusi ya Mfalme Louis XVI ambayo iliratibiwa na Kanisa Katoliki ilikuwa ishabomolewa. Ndiyo chanzo cha Ufaransa kuwa taifa lenye nguvu Ulaya yote hadi kufika mwaka 1814.
======================================================
4. A PLAY-BOOK FROM THE UNITED STATES OF AMERICA (CIA vs JF. KENNEDY)
Raisi John Kennedy amechukua nchi alikuta kuna mambo hayaelewi kabisa. Tena yeye ndiye Raisi wa kwanza Mkatoliki kuwahi kushika nyadhifa hiyo nchini Marekani. Wakubwa wengi ambao ni Waprotestanti na Walokole walikuwa hawamtaki kabisa. Ile ameingia madarakani, amemkuta Allen Dulles kama Mkurugenzi wa CIA ambaye amekaa kwenye nafasi hiyo siyo chini ya miaka 9. Huyo Dulles familia yake ilikuwa kubwa nchini Marekani, wakati yeye ni Mkurugenzi wa CIA, kaka yake John Foster Dulles alikuwa ni Secretary of State. Alianza kipindi cha Eisenhower hivyo Kennedy alimkuta tu.
Mwaka 1961, Raisi Kennedy anapigiwa simu na Mkatoliki mwenzake, Raisi wa Ufaransa Charles De Gaulle na kuulizwa kwanini CIA inaivuruga Ufaransa hasahasa kusababisha vurugu kwenye makoloni yake kama Algeria. Raisi Kennedy anashangaa kwasababu hakutoa amri ifanyike oparesheni yoyote ile. Kumbe CIA na Allen Dulles wanajifanyia mambo wanayotaka huku wakijinufaisha binafsi bila serikali ya Marekani kujua. Wanaua watu, wanapindua viongozi wa nchi na kuteka wakisingizia kupambana na ukomunisti, kumbe dili zote za uwekezaji ni zinazofanikishwa na CIA kwenye nchi za watu ni mali ya matajiri akiwemo Allen Dulles.
Mwaka 1961, JF Kennedy alimfukuza kazi Allen Dulles na kusema hivi "I will splinter the CIA into athousand pieces." Alitaka kuivunja CIA na kuisuka upya na kuwashughulikia mafisadi. Kumbe kauli hii iliwaudhi wakubwa, miungu watu kama Allen Dulles na wenzake akina Edgar J Hoover. Bahati mbaya JF Kennedy hakufahamu, jinsi gani CIA inaendeshwa. Allen Dulles alijifanya amestaafu na kwenda kukaa kwenye nyumba yake nje ya Virginia, kumbe ile siyo nyumba binafsi, ila CIA BASE OF FOR CLANDESTINE/COVERT OPERATIONS. Bado Dulles akawa anaendesha CIA kwa mlango wa nyuma.
Wakamvutia kasi Kennedy, siku ameingia kwenye kumi na nane zao, wakamtafuta muhitimu wa MK-ULTRA bwana Lee Harvey Oswald afanye yake na kumuua Kennedy. Haikuishia hapo, waliua hadi ndugu na jamaa wa karibu wa Kennedy kimya kimya. Baada ya Kennedy kufariki bunge la Marekani likaunda tume ya uchunguzi, bahati mbaya mwenyekiti akawa ni mkurugenzi mstaafu wa CIA, Allen Dulles ambaye alisema kwamba aliyemuua Kennedy alikuwa anaumwa kichaa. Ndiyo nitolee hivyo, wao wakapona. Allen Dulles alinukuliwa akisema, "That man Kennedy, thought he was a god."
JF Kennedy angefanya kama alivyofanya Abraham Lincoln huenda angemaliza muda wake vizuri tu. Wakina Jeff Davis walitoa majeshi na kutaka kumtishia Abraham Lincoln, kilichofuatia yeye akapeleka majeshi na kuwatandika kweli majimbo ya Kusini hadi wakatia adabu. Walikufa watu wengi lakini Lincoln alinukuliwa akisema hivi " I will bring respect to the Union " Angecheka tu ula mwaka 1861 Marekani ingekuwa ishagawanyika vipande viwili na ingefutika kwenye uso wa dunia.
Hata Raisi Andrew Jackson alipopinga kutaka kuanzishwa kwa The Federal Reserve, walitaka kumuua ila wakashindwa. Kilichofuata ni kwamba aliwanyoosha kweli vibaraka wa matajiri wakubwa hadi wakakimbia nchi na kutupilia mbali kabisa mpango wa kuanzisha The Federal Reserve.
==========================================================
Uziri hapa Tanzania NYOKA wanafahamika, tena tunaishi nao kabisa. JOHN wetu aliwachekea akidhani angeweza kulala kitanda kimoja na nyoka halafu yasimkute. Alidanganywa kwamba wanamuogopa na hawawezi kumgusa tena. Akaanza kuwaiga kuchota mapesa, akawajengea nyumba na kuwapa hadi Ubunge kumbe wenyewe wanasubiri ajae kwenye 18. Haya kiko wapi sasa, ???
Binafsi huwa nampenda sana General Paul Kagame, ukiwa ndani ya Rwanda ukajifanya unaleta fyoko-fyoko yaani itakula kwako. Hata uwe Raisi Mstaafu, Jenerali Mstaafi au Afisa Usalama Mstaafu, lazima ile kwako. Huwa natamani Tanzania ipate mtu wa aina ya PAUL KAGAME walau miaka 7 tu, hawa machekibobu waliopo TISS, PCCB, TPDF, PT, BOT, FOREIGN AFFAIRS ambao wameenda kwa vimemo na mbeleko za wazazi halafu wanatuletea ujinga wa DP WORLD, tungekuwa tunawakuta gerezani au tunawaokota kule mabwepande kila siku.
Leo mijitu inaingea udini na ukabila hadharani halafu inaachwa tu, mingine inaiba hela na kuhonga mahawala V8 halafu inapewa kabisa uwaziri. Sehemu kama Marekani, Uchina, Uingereza na Urusi huwezi kufanya mambo kama haya halafu ukaachwa tu. Binafsi huwa nawatamani mno watanzania, nasomaga comments hapa jukwaani halafu nasema, Hiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii, I WISH I KUDU BE THE PRESIDENT, kuna watu wangepata shida mnoo.
Watanzania hawajawahi kukutwa ndiyo maana linchi halina adabu kabisa. Ila ipo siku tu...