Hongera ndugu zetu Waislamu. Wakristo tujifunze kwa hili kutoka kwa ndugu zetu

Hongera ndugu zetu Waislamu. Wakristo tujifunze kwa hili kutoka kwa ndugu zetu

Tukisema ukweli bila kua na upendeleo, kipi katika masuala ya dini, wa kristo wamezidi hao wavaa kobazi (waislamu)

Kwenye mazishi wako excellent kwenye ndoa hata masikini muislamu ana oa, kwenye ibaada wana swali mara tano kwa siku, kwenye kutoa zakat masikini hujaa nyumba zao za ibaada kwa sababu wana jua wanatoa pesa na chakula, likija suala la kufunga mwezi wao hata muislamu mlevi mvuta bagi atafunga au atajificha,

je sisi wakuristo hao watu tuna wazidi nini kwenye dini? Au tuseme dini yao ina uhalisia na ukweli.

Shida Wakristo dini yenu haiko katika udhibiti. Mafundisho ya dini lazima yapokelewe Moja kwa Moja Toka kwa yule ambaye ameyafundiaha. Kuanzia kufanya ibada, kufanya biashara, kuamiliana na watu.

Leo hii nikiwauliza Wakristo ibada zenu mnazitoa wapi, mnafanya vipi biashara ? Mnaamiliana vipi na watu wengine na mfano kama huo ? Hamna majibu.

Mfano naombeni mnijibu maswali haya :

1. Yesu alifundishaje ibada ya Kufunga ?
2. Alifundishaje ibada ya ndoa ?
3. Alifundishaje namna ya kuzika ?
4. Alifundishaje namna ya kufanya biashara ?

Hivi vyote na vingine mlitakiwa muwe mna mafundisho yake Moja kwa Moja Toka kwa Yesu.
 
Wasalaam

Ndugu zetu waislamu wameanza mwezi mtukufu tangu tar 2...wanatimiza moja kati ya nguzo muhimu katika imani yao

Chanda chema huvishwa Pete...tangu wenzetu wameanza mwezi mtukufu,mwamko unauona ni mkubwa sana,watu wa kada mbalimbali,wakubwa kwa watoto,hata wale tunaowaweka kwenye makundi hatarishi kama wahuni,nao wakionekana kujitahidi...heko

Wakristo tunaanza Mfungo Jtano ya majivu ya wiki hii (hasa wakatoliki)
Ajabu muitikio wa kufunga huwa mdogo...huwa tunasingizia kufunga sio mpaka chakula kufunga ni matendo mema...sote tunajua kufunga ni namna tunayouadhibu mwili kwa kuukatalia vikali katika yale ambayo ungedai ni haki yake kama...vyakula,vinywaji,ashki,mazoea tunayoyapenda mfano burudani na michezo

Haya wakati mwingine yametusonga kiasi tumekosa tafakari kwa Mungu...mungo husaidia waliowahi kufunga mashahidi

Tusifunge pale tunapokuwa tumebananishwa na hali ngumu kama uchumi,maradhi na kadhia mbali mbali kubwa au ndogo

Tuweke uwe ni utaratibu wa kujiunganisha na Mungu...kumbuka pamoja na dini zetu...bado binadamu anatakiwa ku connect kwa namna ya pekee na Mungu wake

Hongera waislamu wakristo tuige na tubadilike

NB:Shetani akimghiribu mtu anampa na kisingizio kuhalalisha ughiribu wake...wako watakuja na hoja...ooh waislamu hawafungi wanabadili ratiba ya kula...owk basi ninyi mnajua kufunga...tuwaoneshe wenzetu

Ukweli funga yao ni nzuri na Mungu anaipokea
"sote tunajua kufunga ni namna tunayouadhibu mwili kwa kuukatalia vikali katika yale ambayo ungedai ni haki yake kama...vyakula,vinywaji,ashki,mazoea tunayoyapenda mfano burudani na michezo "

Hapa umeingia chaka plus 😁. Harafu madhehebu ya wakristo yapo mengi, nikujuze kama unaongelea kufunga ni kuadhibu mwili, Basi bado mko mbali, maana kuna madhehebu wanapiga 3 kavu, wengine wanaprogram za kupiga hadi 7 kavu.

Kama ni hoja kuadhibu mwili bado upo chaka, maana mostly wanaubadili tu namna ya ulaji, 6pm futari, kuna snacks hapo hadi saa nne wanakula, na bado daku 😊. Kuna wababe msipo muamsha kula daku, anagoma kufunga Kesho yake.

Imagine : Mtu amekula saa tisa au kumi alfajiri unadhan anasikia njaa saa ngapi 😁. Still kazini wengine hawatak ku engage asilimia nyingi atasema amefunga..

Mfungo ni way kutengeneza displini ya rohon kwa kuutiisha mwili, zile dopamine za mwili, ukiweza ku control means unataka ownership na control ya maisha yako, kutengeneza utulivu ,faida za kiafya etc.

Hauna ugomvi na mwili wako hadi uanze kuuadhibu, then ukisha upa adhabu then what??
 
Back
Top Bottom