Haijawahi kuwa rahisi hivyo.Itaungurumia hapo hapo chini ila kupaa na kwenda mbele ni kimbembe.Kwanza huo uzungukaji wa hilo panga sidhani hata kama wakikanyaga mafuta mwisho linaweza fua upepo wa kuamsha hilo sanduku hapo chini.Walilipeleka kwenye maonyesho nadhani ni haya ya sabasaba ambako nako iliunguruma ikiwa chini.Nilidhani angeingia rubani aipaishe izunguke uwanja kuwafurahisha wananchi ambao walikuwa wengi tu kumbe nayo ni kilema wa ardhini tu na asie sogea.Engine ya noah urefushe shaft ya panga,uigeuze engine iangalie juu na kuifungia panga kubwa hivyo itazunguka kwa mwendo mdogo sana.Kutokana na uzito wa panga bearing ya kuzungusha panga itazidiwa uzito na kuchemka na itajum mapema sana.Kutokana na uzito wa panga haiwezi kufua upepo wa kuiamsha hapo chini sembuse kukadiria mwendo na utumiaji wa mafuta angani.Simkatishi tamaa mtengenezaji ila walishajitokeza hata wa redio huko Geita na watengeneza bunduki na bastola hawakupewa msaada wowote na serikali na hawasikiki tena.Tunawasubiri hao wa Arusha hiyo 2018 huenda wao wakaja nayo Dar na kutua nje ya ofiai ya sayansi na teknolojia.