Katika zawadi nzuri aliyotupatia Rais na Serikali ya muhula huu wa awamu ya Tano ni kuanzisha wizara inayosimamia TEHAMA. Uchumi wa dunia na wa nchi yetu unabebwa na TEHAMA kutokana na sababu zifuatazo:
1. Mawasiliano ya kibiashara, kimalipo, ukusanyaji mapato, maduhuli,matangazo ya kibiashara, mahospitalini, mashuleni, utafiti, hali ya hewa,anga, majini, usalama wa raia nk sasa hivi ni ya kidigitali.
2. Kwa ujumla maisha yetu duniani yanaendeshwa na TEHAMA kuliko kitu kingine chochote.
3. Ushindani wa kiuwekezaji kikanda na kidunia unawezeshwa na teknolojia ya habari.
4 uendeshaji wa serikali na sekta binafsi ni TEHAMA.Tumeshuhudia e-governments na e -industrial and hotel managements.
Kwa msingi huo wizara hii itahitaji kuwa na uwajibikaji wa hali ya juu ili.
1.kulinda mahitaji ya walaji na watumiaji wa teknolojia ya habari
2. Nidhamu na usahihi wa teknolojia hii kwa mazingira yetu
3. Unafuu wa gharama za matumizi ya teknolojia hii
4.ufanisi
5. Uwekezaji wa Mkonga wa mawasiliano wenye kasi kubwa inayotakiwa kwa internet nk. Uliopo uendelee kusambazwa maeneo yasiyofikiwa. Watanzania zaidi ya milioni 15 wanatumia inteneti lakini pia zaidi ya milioni 30 wa simu za mikononi.
6. Kushirikiana na polisi nk Kupambana na makosa ya kimtandao kiufundi.
7. Elimu na kuzalisha wataalam wengi zaidi wa TEHAMA. Ikibidi hata kuanzisha Bodi ya ithbati au kitaaluma ya wana TEHAMA kama ilivyo kwa bodi za wahasibu, madaktari, walimu, mainjinia nk ili kudhibiti taaluma hii.
8. Iwepo program ya kufundisha TEHAMA kuanzia elimu ya msingi hadi chuo kikuu nk.
9. Kuanzisha mpango wa TEHAMA vijijni ili kuwafikishia huduma hii wananchi popote walipo. Teknolojia hii kwa sasa inaonekana kuwa ni muhimu sana kijijini kwa kupashana habari na mawasiliano ya haraka katika uzalishaji. Watu wengi wana simu za mikononi hata bibi wazee kabisa, walemavu nk.
10. Kuzidi kupunguza kodi na ushuru wa forodha kwenye vifaa vya TEHAMA.
Tunamtakia mema waziri Ndugulile kwa kupewa wizara hii nzito na matumaini ya watanzania wakati tukielekea uchumi wa juu. Kama ulivyosema DIJITALI ni uchumi na ni "software" ya maendeleo jadidi. Hongera waziri heri ya Mwaka Mpya.