Hongera Rais wa JMT. Nimeona nyumba wanazojengewa wakazi wa Ngorongoro huku Handeni. Kusema kweli unastahili kuwa Rais wa JMT

Hongera Rais wa JMT. Nimeona nyumba wanazojengewa wakazi wa Ngorongoro huku Handeni. Kusema kweli unastahili kuwa Rais wa JMT

Lord denning

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2015
Posts
15,819
Reaction score
33,255
Kusema ukweli Huyu mama sio wa kawaida.

Nimeona nyumba za kudumu na kisasa wanazojengewa wakazi wa Ngorongoro wanaohamishiwa Mkoani Tanga maeneo ya Handeni na Kilindi.

Ni nyumba za kisasa zinazoakisi akili ya Serikali yako katika kupanga na kutekeleza mipango thabiti kwa maslahi ya Tanzania. Mtu ambaye amehamisha hakuwa hata na makazi wala hati ya eneo Leo hii anajengewa nyumba ya kisasa na kupewa hati kabisa. Kwangu Mimi so far Naona Serikali ya Awamu ya 6 ndo serikali Bora zaidi katika kufanyia kazi mawazo chanya wanayotoa wananchi.

Tulitoa mawazo humu kuwa hela zinazotumika kuwanunulia chakula Wakazi wa Ngorongoro takribani Bil 4-6 kwa mwaka zipelekwe kuwajengea makazi ya kisasa na kudumu wakazi hawa eneo lingine, na Naona leo wazo hili limefanyiwa Kazi na Serikali ya Awamu ya sita.

Hongera sana Rais Samia. Tutazidi kuleta mawazo zaidi kwako kupitia jukwaa hili.

65B6C30E-84F6-47D4-9D44-7A854C9889BD.jpeg
4B01496A-018E-4F71-A4B0-D0C2FED0D5CB.jpeg
 
Propaganda za kipumbavu sana hizi.

Hela zinazotumika kuwanunulia chakula Wakazi wa Ngorongoro takribani Bil 4-6 kwa mwaka zipelekwe kuwajengea makazi ya kisasa na kudumu wakazi hawa eneo lingine, na Naona leo wazo hili limefanyiwa Kazi na Serikali ya Awamu ya sita.

Hizo pesa za kuwalisha mlikuwa mnazitoa wapi? Katika mfuko gani?
 
Unajua haya maneno;
Social; Economical and Environmental ?

Ili kuepuka makosa au watu kutokuona kwamba haya makazi ni yao ni vema kuwashirikisha tangia mwanzo na sio kujenga tu na kuwapa kama pipi...

Ni pengi yalipofanyika kama haya matokeo yake hayakuwa mazuri muda si muda makazi hayo yalibadilika kuwa magofu
 
Hujui ulisemalo mkuu, Wazo la kuwatoa, kelele na nguvu zilizotumika kuwatoa ndugu zetu then wakajengewa Nyumba haraka kiasi hicho, try to think deep, angalia length of time kwa mambo yote hayo je? Hupati doubt yoyote?

TUNASUBIRI MAENDELEO BAADA YA NDUGU ZETU KUTOKA NGORONGORO
 
Kusema ukweli Huyu mama sio wa kawaida!

Nimeona nyumba za kudumu na kisasa wanazojengewa wakazi wa Ngorongoro wanaohamishiwa Mkoani Tanga maeneo ya Handeni na Kilindi.

Ni nyumba za kisasa zinazoakisi akili ya Serikali yako katika kupanga na kutekeleza mipango thabiti kwa maslahi ya Tanzania

Mtu ambaye amehamisha hakuwa hata na makazi wala hati ya eneo Leo hii anajengewa nyumba ya kisasa na kupewa hati kabisa!

Kwangu Mimi so far Naona Serikali ya Awamu ya 6 ndo serikali Bora zaidi katika kufanyia kazi mawazo chanya wanayotoa wananchi.

Tulitoa mawazo humu kuwa hela zinazotumika kuwanunulia chakula Wakazi wa Ngorongoro takribani Bil 4-6 kwa mwaka zipelekwe kuwajengea makazi ya kisasa na kudumu wakazi hawa eneo lingine, na Naona leo wazo hili limefanyiwa Kazi na Serikali ya Awamu ya sita.

Hongera sana Rais Samia. Tutazidi kuleta mawazo zaidi kwako kupitia jukwaa hili.
Picha ziko wapi?
 
Back
Top Bottom