Hongera sana Collins Obinna Chibueze, Prince of Country Music.

Hongera sana Collins Obinna Chibueze, Prince of Country Music.

Damaso

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
3,978
Reaction score
6,739
Nikipewa nafasi nitaje wanamuziki wangu bora kwenye muziki wa Country basi sitoweza kumuacha John Denver na nyimbo zake bora za “Take Me Home, Country Roads,” pamoja na “Thank God I’m a Country Boy”. Carrie Underwood, Keith Urban mpiga gitaa bora sana, Brad Paisley, Chris LeDoux, Webb Pierce fundi sana huyu na wimbo wake wa “In the Jailhouse Now,”.

1726130142934.png


Halafu kuna mwamba mmoja matata sana alitupatia chuma kizito sana “The Gambler” huyu ni Kenny Rogers, Gary Stewart, John Prine. Ila kuna watu watatu ambao dunia inawaheshimu kupita maelezo linapokuja suala la muziki wa Country, haswa ni Merle Haggard, Hank Williams, pamoja na Legendary kabsa, Johnny Cash, ukipata nafasi sikiliza wimbo wake wa “I Walk the Line” utaamini kuwa hawa ni wachonga njia.
1726129693816.png

Ila kwa sasa kuna kajamaa kana miaka yake 29 tu ila kamewavuruga wazungu kwa mahaba yake kwenye muziki wa Country, acha kabsa! Kijana kutoka Nigeria amewafanya watu waanze kuupenda sana muziki wa Country, albamu zake tatu za Lady Wrangler, Cowboys Live Forever, Outlaws Never Die, pamoja na hii ya mwaka 2024 Where I've Been, Isn't Where I'm Going zimetosha kabsa kumfanya awe wa kipekee sana ndani ya Marekani.

Majina yake anaitwa Collins Obinna Chibueze ila wengi tunamfahamu kwa majina ya Shaboozey, ni mwandishi, mtunzi na mwanamuziki kutoka Marekani. Kama ulipata kutazama filamu ya Spider-Man: Into the Spider-Verse basi fahamu kuwa wimbo wa "Start a Riot" ulimpa umaarufu sana. Mwaka huu alishirikiana na Beyonce kwenye nyimbo mbili kwenye albamu ya nane ya Beyonce, inayoitwa Cowboy Carter, ila kubwa ni mwaka huu amefanya maajabu, kupitia wimbo wake wa "A Bar Song (Tipsy)" ambao umetia fujo sana ndani ya chati za Billboard Hot 100.

1726129751797.png


Chibueze ama Shaboozey amezaliwa na kukulia Marekani katika jimbo la Virginia na wazazi wake ni Wanaijeria kutoka kabila la Igbo. Jina lake Chibueze lina maana ya "God is king" au Mungu ni Mfalme kwa lugha ya Igbo. Wimbo wake wa kwanza ulikuwa ni "Jeff Gordon", kabla ya mwaka 2017 kupewa nafasi ya kuwa sehemu ya Republic Records ikiwa ni baada ya kuonesha uwezo wa ajabu sana kwenye nyimbo za "Starfoxx" pamoja na "Robert Plant".

Kwa sasa mwamba anawafanya watu kama Jon Pardi, Carly Pearce, Luke Combs, Cody Johnson pamoja na Kane Brown waumize vichwa sana, wimbo wake huu wa A Bar Song (Tipsy) ambao una miezi mitano tu umepata views zaidi ya milioni 116 na sasa inaonesha kuwa katika hizi wiki mbili za hivi Karibu amepata views zaidi laki nne! Mnaijeria unawakimbiza Kaka! Wape muda wavute pumzi! Hakika Mungu ni Mfalme, Chibueze. Kwa hakika Ogak Jay Oke anakuona kama role model mkubwa sana!

1726129793798.png


Kwa leo tu mwanaume amesepa na Kijiji cha watu zaidi ya 40K! 116,289,688 na wimbo wake ni namba 76 top global! Takwimu kutoka kwa Luminate zinasema “A Bar Song (Tipsy)” imesikilizwa na watu zaidi ya mara milioni 78 radio katika radio za Amerika ya Kaskazini pamoja na Kusini, huku pia ikiwa na jumla ya streams zaidi ya milioni 30 katika mitandao ya kimuziki. Kuanzia kesho Ijumaa mwamba ana show zaidi ya 32! Hapo ni mpaka December 13 ndo atatulia!


View: https://www.youtube.com/watch?v=t7bQwwqW-Hc

Nyingine ni kwamba mtaalamu ameweka rekodi yake ya kipekee, wimbo wake huu wa "A Bar Song (Tipsy)" ndo unashika rekodi ya kuwa wimbo namba moja wa 2024 kwenye chat ya Billboard Hot 100 kwa wiki saba ikichukua nafasi ya wimbo wa "I Had Some Help" wa Post Malone akishirikiana na Morgan Wallen. Wao wazungu wanakuambia #1 single of 2024 on the Hot 100 for seven weeks!

Asante sana Mwamba Collins Obinna Chibueze!
 
Hongera kwake.
Ilq kwangu my favourite ni Maren Morris kwenye Country music
Ni kweli kabsa Maren Morris ni 🔥 ingawa wamarekani kwa sasa hawapendi kusikia Classic Country
 
Ni kweli kabsa Maren Morris ni 🔥 ingawa wamarekani kwa sasa hawapendi kusikia Classic Country
Mkuu yaani toka nimeanza kuusikiliza huu music basi nimepata faraja kubwa katika maisha ukiachana na gospel
 
Shaboozey’s “A Bar Song (Tipsy)” rounds up a 15th round at No. 1 on the Billboard Hot 100.

The song, which became the singer-songwriter’s first Hot 100 leader in July, extends 2024’s longest reign. It also ties Harry Styles’ 2022 smash “As It Was” for the second-longest reign this decade; Morgan Wallen’s “Last Night” — like “A Bar Song (Tipsy),” a country-pop crossover hit — dominated for 16 weeks in 2023.

Wakimbize Obinna 😃
 
Back
Top Bottom