Hongera sana Freeman Mbowe kwa kuifikisha Tanzania hapa!

fazili

JF-Expert Member
Joined
Jun 10, 2011
Posts
16,427
Reaction score
22,418
Freeman Mbowe ni matunda ya harakati za mapambano dhidi ya dhuluma, uonevu na ukoloni. Amerithi hulka ya mapambano ya kudai haki za wananchi wenzake kwa baba yake Aikaeli Mbowe aliyekuwa mwana Afrika shupavu na mpigania uhuru hodari. Freeman (Uhuru) alizaliwa katika miaka ile ambapo watanganyika akiwepo baba yake walikuwa wanapigania uhuru wa Tanganyika.

Tunamshukuru mwanamapinduzi huyu hodari kwa umahiri wake wa kuongoza mapambano dhidi ya dhuluma katika nyakati zetu chini ya wakoloni weusi. Hongera sana Freeman Mbowe kwa kuirudisha Tanzania katika siasa za vyama vya upinzani, hakika wewe ni baba namba 2 wa Taifa letu!
 
Sasa nyie mkipewa nchi Lumumba si cha mtoto kwa uchawa? Nimeona mnaparurana na ACT kugombea sifa aliyefanya Samia aruhusu mikutano.

Hatuna vyama nchi hii. Mifumo iwe makini, hivi vyama vikienda hivi raia wataanza kubuni njia mbadala za kujitetea.

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
 
Kuweza kumshawishi rais aliyeko madarakani hadi ajikane mwenyewe na kukubali hoja yako ni ufundi wa ajabu mno! Hongera mwanadiplomasia mbobezi Freeman Mbowe!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…