Hongera sana homeboy kwa kumleta Flora (Mbasha) Henry nyumbani

Hongera sana homeboy kwa kumleta Flora (Mbasha) Henry nyumbani

Status
Not open for further replies.
Hivi taratibu za dini ya kikristo zikoje juu ya hili???..Unaweza kumuacha mke wako wa ndoa na kuoa mwanamke mwingine?
soma hili andiko hili ( Mathew 19:3-12).Amemalizia kwa kusema awezae kupokea neno hili na apokee.Hivo inahitaj neema ya Mungu kuish ktk neno lake.Ingawa najua si vema kufanya hayo.
 
Unatumia nguvu nyingi sana kwenye hii post. Kaweke pingamizi mkuu
inaelekea mnapenda sana wake za watu
sasa nikaweke pingamizi kwani huyo mke wangu
.
halafu sijaona hizo nguvu nyingi nilizotumia
 
Ni kweli zogo (controversy) au hekaheka kubwa inayowagawa watu katika makundi mawili kuhusu talaka inapatikana katika injili ya Mathayo 5:32 na 19:9
Kumbuka Injili ya Luka na Marko pia imeripoti tukio la Mathayo 19:9 Yesu alipotegwa swali na Mafarisayo isipokuwa ni Mathayo peke yake ameandika kuhusu exception ya kutoa talaka ambayo ni kosa la uasherati (tutaangalia baadae kwa nini ni mathayo peke yake ameripoti hivyo).

Kabla ya kufika huko ni Muhimu sana kufahamu mazingira (geography) iliyopelekea Yesu kuulizwa swali na Mafarisayo.
Tukumbuke kwamba Yesu alikuwa Galilaya na alikuwa amemaliza huduma yake na sasa alikuwa anasafiri kupitia eneo la Perea ili kurudi Yerusalemu kwa ajili ya pasaka (yaani kifo chake).

Mafarisayo waligundua kiwamba Yesu atapita hilo eneo ambalo kwa wakati huo lilikuwa chini ya himaya ya Herodi.
Hivyo mafarisayo walijua ni wakati muafaka wa kumuuliza swali (trick question) ili ajichanganye na wapate sababu ya kumuua.
(kumbuka mafarisayo walikuwa wanamfafuta sana Yesu wamuue ila walikosa sababu au shitaka Mathayo 12:14, Marko 3:6)
Kwa hiyo mafarisayo walimuuliza Yesu swali ambalo lengo ni kumtega yeye (test) na si kutaka kujua.

Kumbuka miaka 2 iliyopita Yohana mbatizaji ambaye alimtangulia Yesu alikuwa amefungwa Jela kwa sababu aliongelea suala la talaka ya Herode Antipas ambaye alioa mke wa mdogo wake Filipo ambaye mke wake alitoa talaka kwa mume wake Filipo na kwenda kuolewa na Herodi Antipas (kaka mtu) Soma Mathayo 14:1-12.

Yohana mbatizaji hakubabaika au kujisikia vibaya kumkemea Herodi na dhambi yake hata kama ni ikulu (Math 14:4) matokeo yake akawa arrested na kutupwa jela na baadae kukatwa kichwa.

Kwa kuwa Yesu alikuwa anapita maeneo ambayo ni himaya ya herodi Antipas, mafarisayo walijua fika kwamba Yesu atajichanganya tu na jibu la swali watakaloulizwa na atajimaliza kwa kumtaja Herode na dhambi yake ya kuoa mke wa mdogo wake na kama Yohana mbatizaji kwa kutamka tu aliuawa Yesu Je ambaye anapita kwenye himaya yake?

Swali aliloulizwa Yesu lilikuwa:
Ni halali mtu kumwacha mke wake kwa sababu yo yote?’

Kumbuka wakati Yesu yupo duniani talaka ilikuwa inakubalika kutokana na Musa alivyoamuru hata hivyo kulikuwa na gumzo na utata wa sababu ipi hasa mume anaweza kutoa talaka kwa mke au sababu ipi hasa inaweza kupelekea mume kutoa talaka kwa mke wake na kumbuka pia wayahudi walikuwa hawaruhusu mwanamke kutoa talaka bali mwanaume tu.

Ndipo kukawa na makundi matatu yanayopingana

KUNDI LA KWANZA – SHAMMAI
Wao walikubaliana kwamba sababu inayoweza kumfanya mume kutoa talaka ilikuwa ni uzinzi (adultery)

KUNDI LA PILI – HILLEL
Wao walikubaliana kwamba sababu inayoweza kumfanya mume kutoa talaka ni pale mke akipika chakula kisichoiiva au kibaya au ovyo.

KUNDI LA TATU – RABBI
Wao walikubalkiana kwamba hata mume akikutana na mwanamke mzuri zaidi ya Yule anaye nyumbani basi anaweza kutoa talaka

Sasa swali kwa Yesu lilikuwa wewe upo upande gani?
SHAMMAI, HILLEL AU RABBI?

Yesu alifahamu fika mioyo ya mafarisayo inawaza kitu gani na akawajibu kwa swali (counter attack) kwa kuwauliza tangu mwanzo Mungu alifanya kitu gani kwa ajili ya mke na mume.

Mafarisayo wakajikuta swali lao limekosewa na kwamba wamekosa point kwani wao walitaka ajibu Kumbukumbu la Torati 24:1-4) na Yeye akajibu Mwanzo 2:24.

Ikabidi wamrukie kwa swali kuhusu Musa kuruhusu talaka ndipo wakajibiwa kwamba Musa aliruhusu talaka kwa sababu ya ugumu wa mioyo yao na kukataa kwao design ya ndoa tangu mwanzo na ndipo Yesu akazusha mambo 4 muhimu kabisa

JAMBO LA KWANZA
Hapo mwanzo Mungu aliumuumba mwanaume mmoja kwa ajili ya mwanamke mmoja, kama angetaka Adamu awe na wanawake wengi basi angewaumba akina Sandra, Joan, Jane, Linda wakutosha na si Eva peke yake.
(mwanzo 1:27, 5:2, Marko 10:16)

JAMBO LA PILI
Yesu anatia mkazo kwamba ndoa ndicho kifungo (strongest bond) duniani hivyo kabla ya kuingia kwenye ndoa ni muhimu sana anayehusika kufahamu kwamba anaingia kwenye kitu ambacho huwezi kutoka labda kifo kitokee kati ya wawili.
(Mwanzo 2:24, Marko 10:7)

JAMBO LA TATU
Katika ndoa wawili huwa mtu mmoja, mwili mmoja (one flesh)
(Mwanzo 2:24, Marko 10:8)

JAMBO LA NNE
Yesu alithibitisha kwamba Mungu ndiye huwaunganisha wawili wanaooana na kwamba kile Mungu amekitenganisha binadamu asikitenganishe.

Hivyo swali la mafarisayo
Ni halali mtu kumwacha mke wake kwa sababu yo yote?’
Jibu la Yesu ni HAPANA KUBWA
Na kwamba Yesu hakuwa kwenye kundi lolote iwe SHAMMAI AU HILLEL AU RABBI.

Yesu alielezea kudumu (permanency) na kutovunjika (inviolability) ya ndoa hadi wanafunzi wakaendelea kumuuliza jioni yake huku wakipendeleza kwamba kama masuala ya ndoa ni hivyo basi ni busara sana mwanaume asioe kabisa.
Umeelezea vyema sana with evidence
kambagasa pitia hapa utajifunza kitu
 
Hii itakuwa ndoa ambayo itafungishwa na mkuu wa wilaya/mkoa au ni yake kimila, ndoa ya kanisani ni mara moja tu ktk maisha ya mkristo. Kwa uelewa wangu,sijui km mke/mme akifariki sheria za dini ya kikristo huwa zinasemaje.
Ngoja wataalamu waje watudadavulie... Anyway, hongereni kwa hatua nzuri mliyofikia maharusi watarajiwa.
hapo kama mke au mume amefariki kwa mujibu wa neno la Mungu ambayo kwetu sisi wakristo ndio sheria yetu yakutuongoza ni kuwa anaruhusiwa kuolewa tena 1korintho 7:39 anasema mwanamke hufungwa maadamu mumewe yu hai lakini ikiwa mumewe amefariki yu huru kuolewa na mtu yeyote amtakaye;katika Bwana angalizo katika Bwana.
 
Hivi taratibu za dini ya kikristo zikoje juu ya hili???..Unaweza kumuacha mke wako wa ndoa na kuoa mwanamke mwingine?
hilo itabidi tumuulize mch. Gwajima jpili, atueleze ndoa ya E. Mbasha itakuwa halali?
 
Ni utafiti ambao sijauthibitisha; Kwa mwanamke, ukiachika kwenye ndoa yako ya kwanza, hilo ni doa hata kwa jiki halitoki, na uwe na uhakika wa kustrugle sana na ndoa zifuatazo. Too bad, kama mulifikia hatua ya kuwa na mtoto na mume wa kwanza.

Otherwise, all the best Flora wa Mbasha
 
Ndoa inasiri kubwa sana hatuwezi kujua ni nini kilikuwa tatizo hadi madame akaona hawezi kuvumilia. Mimi namtakia maisha mema ya ndoa mpya
 
Wamisionari na waarabu walituweza kweli
Ng'wanapagi, ubebe unkhe wako uliojaniwa naling'wana ukuyega??? Flora ni kama anajitutumua tu lakini ukweli utakuja kuuona mbeleni, na kitu kibaya sana in this life ni kuonja kipawa cha roho mtakatifu then uka-backslide na usitake kabisa kurudia nafasi ya maisha wokovu, ila yawezakuwa ni certain curse maana nimewahi sikia hata mother-in-law wetu naye alikimbiaga mume wake akaenda kuslimu na akaolewa na mwislamu kabisa ili hali husband alikuwa mchungaji kabisa kabisa tena wa kanisa la kiroho, ila maisha ya duniani yana maswali mengi lakini majibu hakuna. Kutoka kuimbiana nyimbo kwenye tv mpaka kuwa public enemies, Ng'wanapagi nalumilaga sana mu moyo gwane!!!!
 
Hivi taratibu za dini ya kikristo zikoje juu ya hili???..Unaweza kumuacha mke wako wa ndoa na kuoa mwanamke mwingine?
Nijuavyo mm ni labda iwe kwa habari ya zinaa ndo waweza toa talaka na ukaruhusiwa kuoa,sijui labda sasa hivi sheria zimebadilika
 
Marriage life is so hard to define especially if ur not the one participating the game, I thnk it's not a real time to judge and blame Flora for her decision. Let us look back to our side if real 100% we are complete.
it doesnt matter how tough the marriage is we need to settle our differences in a Godly way as we know God.Being remarried doesnt guarantee you find an angel to live with and you manage to escape the devil at first place no and big no all make mistake couse we are humans.So she isnt in a position to have an excuse to get married.She might be in that relation b4 and thats why she is conviced to do so.So i find her like a trouble maker.And that spirit of remarry will never let her go bt it will end tormenting her in her entire life unless she repent.
 
Kama una ushahidi wa uzinzi unaruhusiwa
Mungu abarki tu! Ila kw uzinzi inaruhusiwa kutengana na haitenganishwi na mahakama. Ndiyo maana Kanisa Katoliki lina mfumo bora zaidi juu ya ndoa. Haya yetu, unaweza kuoa na kuacha kesho, ukaoa tena. Kama kanisa halikuitenganisha hiyo ndoa ya awali, hapa bado hakuna ndoa, ila kuna uzinzi unaobarikiwa na makanisa ya wajuaji wa sasa
 
Mkuu pitia hapa Mathew 19:3-12
cc Clara Daud
Mathayo 19

9 Nami nawaambia ninyi, Kila mtu atakayemwacha mkewe, isipokuwa ni kwa sababu ya uasherati, akaoa mwingine, azini; naye amwoaye yule aliyeachwa azini.

Labda utufafanulie unaelewa nini maana ya neno uasherati
 
Mmmh frola aone aibu sasa jaman,ndoa ya kwanza watu walichangia(kaivunja mwenyewe)

Na hii ya pili anataka michango aisee
 
Si kweli na hakuna kifungu hicho
Utofauti wa maoni juu ya talaka na kuoa tena unatokana na maneno ya Yesu katika Mathayo 5:32 na 19:9. “isipokuwa kwa habari za uasherati” ndicho kipengele peke yake ambacho Mungu anatoa ruhusa ya talaka na kuoa tena katika maandiko.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom