Hongera sana Hospitali ya mkoa wa Mwanza kwa ubunifu huu

Hongera sana Hospitali ya mkoa wa Mwanza kwa ubunifu huu

Ndebile

JF-Expert Member
Joined
Sep 14, 2011
Posts
7,745
Reaction score
11,267
Upungufu wa watumishi wa sekta ya afya ndio changamoto kubwa, changamoto nyingine ni watumishi wachache waliopo kufanya kazi zaidi ya uwezo wao. Mfano nesi mmoja kuwahudumia wagonjwa hadi 40 au zaidi kwa siku na wakati mwingine hata kunyimwa siku za mapumziko kwa sababu ya baadhi ya zamu kukosa watu. Imefikia wakati watumishi wengine kuomba ruhusa kwa visingizio vya kuumwa, kuuguza nk kwa sababu wanachoka sana huku hakuna jitihada zozote ya kuwapa motisha.

Vifo vingi vya wagonjwa chanzo chake kikubwa ni pamoja na kuhudumiwa na mtumishi ambaye naye ni mgonjwa kisaikolojia, yaani anafanya basi tu! "huwezi kuwapa watu furaha wakati wewe huna furaha" . Mfano mmoja ni hospitali ya wilaya ya Nyamagana ambapo Daktari anaingia zamu maarufu kama "call shift" leo hii jioni, anakesha na asubuhi anatibu kama kawaida kuanzia asubuhi hadi jioni ndipo anarudi nyumbani, zamu ya masaa 24! only in Tanzania! Sasa muulize Daktari huyo hiyo hela ya masaa ya ziada ni sh. na ataipata lini? Kiukweli hajui maana utasikia "basket fund" ikitoka, nk.

Leo jamaa yangu mmoja kaniambia kuna mpango wameuanzisha hospitali ya mkoa wa Mwanza, Sekou Toure kwenye wodi ya Wazazi, mpango huu unaitwa CHIMBO ambapo muuguzi yeyote aliyepo mapumzikoni anaweza "kuuza" muda wake wa mapumziko kwa kufanya kazi kwa ujira wa shilingi 20,000/= shift moja ya masaa 8 na hela yako unapewa hapo kwa hapo hakuna cha sijui cheki haijapitishwa, sijui fungu halijatoka, nk. hiki ni kiasi kidodo cha pesa ila angalau kinapatikana kwa wakati na watumishi wamechangamkia "fursa" hii kiasi kwamba sasa hivi huduma katika wodi ya wajawazito ni za kiwango cha kuridhisha sana.

Nimeandika uzi huu kwa lengo la kutambua mchango wa mtu aliyebuni chimbo, nchi yetu ina wasomi wengi ila sio wabunifu, basi jamii yetu ifike wakati tuwapongeze na kutambua michango ya wabunifu wachache waliopo! Kongore ziende kwa mbunifu wa chimbo wodi ya wazazi hospitali ya mkoa wa Mwanza.

Pia mpango huo usiwe mbadala wa kuajiri watumishi wapya ili angalau kuboresha huduma.
 
Mpango nimzuri sana, ila binadamu anahitaji mapumziko ili aweze kufanya kazi kwa ufanisi. Kazi ya uuguzi inachosha sana mwili na akili ndio maana kukawa na siki za mapumziko sasa kufanya kazi bila kupumzika kunaweza kusiwe na tija kubwa zaidi ya kuwa muuguzi yupo, ndio pale mgonjwa ana kuhitaji muuguzi umelala. Waairi tu kwani hakuna wauguzi walio mitaani waliosoma na kufaulu vyema?
 
Mpango nimzuri sana, ila binadamu anahitaji mapumziko ili aweze kufanya kazi kwa ufanisi. Kazi ya uuguzi inachosha sana mwili na akili ndio maana kukawa na siki za mapumziko sasa kufanya kazi bila kupumzika kunaweza kusiwe na tija kubwa zaidi ya kuwa muuguzi yupo, ndio pale mgonjwa ana kuhitaji muuguzi umelala. Waairi tu kwani hakuna wauguzi walio mitaani waliosoma na kufaulu vyema?
Mkuu ili la kuajiri naona wakubwa hawataki kulisikia!
 
CAG akipita hapo utashangaa ufisadi utakaoibiliwa hapo.Serikali haina malipo ya overtime ya cash
 
Back
Top Bottom