Kwanza kabisa ninakupongeza kocha Zahera na wachezaji wote kwa mshikamano mlionao tangu ligi ilipoanza mpaka sasa hamjapoteza hata mechi moja. Kwa wapenzi wa Klabu jirani zetu kila mara wanatusema kuwa hatuna fedha, Klabu imefilisika sasa tuwaonyeshe kuwa sisi ni wamoja na hivyo tunaiomba Klabu ifufue ile akaunti ya Mpesa,Airtel, Tigo ili wapenzi wa Klabu tuweze kutuma fedha ili kuisaidia Klabu yetu. Watani wetu hawana raha kila tukipata ushindi katika mechi tunazocheza. Tuna imani ubingwa utarudi tena Jangwani msimu huu.