Hongera sana Maxence Melo

Hongera sana Maxence Melo

mediaman

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2011
Posts
451
Reaction score
688
Kwa heshima na taadhima, nakupongeza na kukushukuru sana Maxence Melo kwa kubuni jamvi hili zuri na kulisimamia vema tangu ulipolianzisha miaka mingi iliyopita.

Nakuvulia kofia, Mkuu. Mimi binafsi nimepata faida nyingi sana humu. Kupitia jamvi hili nimeelimika kisiasa, kiafya, kibiashara na hata kiroho. Nimepata habari za kitaifa na kimataifa kwa wakati mwafaka. Na pia nimeongeza ujuzi wa lugha ya Kiswahili kupitia jamvi hili.

Kwangu mimi JamiiForums ni zaidi ya Redio na TV. Ndiyo sababu nimeona vema leo niseme asante sana Mkuu pamoja na timu yako (inayofanya kazi bila kuchoka kuhakikisha vigezo na masharti ya uandishi wa nyuzi, vinazingatiwa). Hata Maandiko Matakatifu yanatuambia "mambo yoyote yaliyo ya kweli, yoyote yaliyo ya heshima, yoyote yaliyo ya haki, yoyote yaliyo safi, yoyote yenye kupendeza, yoyote yenye sifa njema; ukiwapo wema wowote, ikiwapo sifa nzuri yoyote, tuyatafakari hayo." (Flp 4:8).

Mwisho, ingawa sio kwa umuhimu, nawashukuru Waandishi na Wachangiaji wa nyuzi mbalimbali. Mnaifanya JamiiForums izidi kung'ara. Mungu awabariki sana wote.
 
Baada ya Kumaliza Kidato cha Sita sikuona tena haja ya kwenda Chuo Kikuu kupata sijui Degrees, Masters na Doctorates ambazo wengi wenu ( siyo Wote ) mnazikimbilia na bado haziwasaidii na hazijawasaidia kwa lolote lile lenye Tija Kwenu Binafsi na kwa nchi yetu hii ya Tanzania

Kujiunga Kwangu tu hapa JamiiForums na Maarifa makubwa niyapatayo, kuimarika Kwangu kwa Kujenga na Kukabili Changamoto za Kitaaluma na Kifikra najiona si tu nina Degree bali sasa nina PhD yangu kutoka JamiiForums University.

JamiiForums imeimarisha sana uwezo wangu wa Kufikiri na ndiyo maana mara kwa mara nimewahi kusema kuwa ifike mahala sasa ama Serikali imtambue Mtani wangu wa Kihaya Maxence Melo kwa kumpa Tuzo ya Juu ya Heshima au basi Sisi Members wa JamiiForums tumfanyie Jambo jema na la Kutukuka kabisa kwa Ubunifu wake huu ambao una Tija kubwa kwa Ustawi na Maendeleo ya Taifa la Tanzania na Sisi Watanzania pia.

Naamini Serikali ya sasa ya Rais Mstaarabu na Muungwana asiye na Chuki ( Kisununu ) wala Kisasi, Ubabe na Ukatili ( Roho Mbaya ) Mama Samia Suluhu Hassan ( ambaye bahati nzuri nae ni Mwenzetu hapa na huwa tunakesha nae 24/7 ) ataliona hili na Kumtunuku huyu ' IT Guru ' Maxence Melo na Kampuni yake nzima bila kuwasahau na Wafanyakazi ( Watendaji ) wake wote kwa Kazi kubwa, ngumu na sometimes ya Hatari wanayoifanya.
 
ifike mahala sasa ama Serikali imtambue Mtani wangu wa Kihaya @Maxence Melo kwa kumpa Tuzo ya Juu ya Heshima au basi Sisi Members wa JamiiForums tumfanyie Jambo jema na la Kutukuka kabisa kwa Ubunifu wake huu ambao una Tija kubwa kwa Ustawi na Maendeleo ya Taifa la Tanzania na Sisi Watanzania pia.
Point
 
Maxence Mubyazi Melo anastahili heshima iliyotukuka kutoka kwetu sisi wengine tuliokesha nae miaka yote ya Jiwe bila kuteteleka na kuwa hai Mpaka hivi leo, tunamshukuru sana kwa professiolism yake!! Ama sivyo kwa jinsi tulivyokuwa tunawindwa, he could have easily sold us for thirty pieces of silver BUT he resisted to the end inspite of all the hardships he had to endure! Bravo Mubyazi.
 
Genta, upo kaka?

Umetiririka na kuserereka vyema kama D-Kimoko alivyokuwa akizisurubu nyuzi katika kile kibao cha Bolingo fulani nimeisahau jina.

Mengine uliyosema ni sawa. Nimefurahi "kukuona" hapa.
Asante sana Comrade ( Kamarada ) Interest nami pia nimefurahi Kukuona hapa na naamini Salamu zangu kwa Kamarada ( Comrade ) Mwenzetu wa Kinyankole ( Kimbulu ) umezipata kwani huwa nawasiliana nae mno na Kukuulizia sana.

Una IQ Kubwa, Umeiva na Mjenga Hoja.
 
Maxence Mubyazi Melo anastahili heshima iliyotukuka kutoka kwetu sisi wengine tuliokesha nae miaka yote ya Jiwe bila kuteteleka na kuwa hai Mpaka hivi leo, tunamshukuru sana kwa professiolism yake!! Ama sivyo kwa jinsi tulivyokuwa tunawindwa, he could have easily sold us for thirty pieces of silver BUT he resisted to the end inspite of all the hardships he had to endure! Bravo Mubyazi.
Hakika kabisa Mkuu. Jamaa atunukiwe.
 
Baada ya Kumaliza Kidato cha Sita sikuona tena haja ya kwenda Chuo Kikuu kupata sijui Degrees, Masters na Doctorates ambazo wengi wenu ( siyo Wote ) mnazikimbilia na bado haziwasaidii na hazijawasaidia kwa lolote lile lenye Tija Kwenu Binafsi na kwa nchi yetu hii ya Tanzania

Kujiunga Kwangu tu hapa JamiiForums na Maarifa makubwa niyapatayo, kuimarika Kwangu kwa Kujenga na Kukabili Changamoto za Kitaaluma na Kifikra najiona si tu nina Degree bali sasa nina PhD yangu kutoka JamiiForums University.

JamiiForums imeimarisha sana uwezo wangu wa Kufikiri na ndiyo maana mara kwa mara nimewahi kusema kuwa ifike mahala sasa ama Serikali imtambue Mtani wangu wa Kihaya Maxence Melo kwa kumpa Tuzo ya Juu ya Heshima au basi Sisi Members wa JamiiForums tumfanyie Jambo jema na la Kutukuka kabisa kwa Ubunifu wake huu ambao una Tija kubwa kwa Ustawi na Maendeleo ya Taifa la Tanzania na Sisi Watanzania pia.

Naamini Serikali ya sasa ya Rais Mstaarabu na Muungwana asiye na Chuki ( Kisununu ) wala Kisasi, Ubabe na Ukatili ( Roho Mbaya ) Mama Samia Suluhu Hassan ( ambaye bahati nzuri nae ni Mwenzetu hapa na huwa tunakesha nae 24/7 ) ataliona hili na Kumtunuku huyu ' IT Guru ' Maxence Melo na Kampuni yake nzima bila kuwasahau na Wafanyakazi ( Watendaji ) wake wote kwa Kazi kubwa, ngumu na sometimes ya Hatari wanayoifanya.
Huu ni ushahidi tosha kuwa JamiiForums ni chombo muhimu. Naunga mkono hoja: Founder wa jukwaa hili na kampuni yake wapewe tuzo
 
Back
Top Bottom