Shadow7
JF-Expert Member
- Sep 28, 2020
- 24,606
- 39,289
Ndio mkuuKumbe ni wengi tunaofaidika na JF.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ndio mkuuKumbe ni wengi tunaofaidika na JF.
NaamKwa heshima na taadhima, nakupongeza na kukushukuru sana Maxence Melo kwa kubuni jamvi hili zuri na kulisimamia vema tangu ulipolianzisha miaka mingi iliyopita.
Nakuvulia kofia, Mkuu. Mimi binafsi nimepata faida nyingi sana humu. Kupitia jamvi hili nimeelimika kisiasa, kiafya, kibiashara na hata kiroho. Nimepata habari za kitaifa na kimataifa kwa wakati mwafaka. Na pia nimeongeza ujuzi wa lugha ya Kiswahili kupitia jamvi hili.
Kwangu mimi JamiiForums ni zaidi ya Redio na TV. Ndiyo sababu nimeona vema leo niseme asante sana Mkuu pamoja na timu yako (inayofanya kazi bila kuchoka kuhakikisha vigezo na masharti ya uandishi wa nyuzi, vinazingatiwa). Hata Maandiko Matakatifu yanatuambia "mambo yoyote yaliyo ya kweli, yoyote yaliyo ya heshima, yoyote yaliyo ya haki, yoyote yaliyo safi, yoyote yenye kupendeza, yoyote yenye sifa njema; ukiwapo wema wowote, ikiwapo sifa nzuri yoyote, tuyatafakari hayo." (Flp 4:8).
Mwisho, ingawa sio kwa umuhimu, nawashukuru Waandishi na Wachangiaji wa nyuzi mbalimbali. Mnaifanya JamiiForums izidi kung'ara. Mungu awabariki sana wote.
Appreciation to you Maxence Melo
Ndio mkuu