MR.NOMA
JF-Expert Member
- Feb 1, 2014
- 339
- 505
Hongera Sana Mkuu,
Umerudi kwenye Jungu Kuu,
Wahuni walifanya sikukuu,
Pale ulipokamuliwa jipu na Mkuu,
Waoneshe kazi unaiweza, Wala usihangaike nao.
Ulikuwa ukitimizaajukumu Yako,
Tena Kwa kutumia weledi wako,
Ukakumbana na likambako,
Ambalo baba alilipaka upako,
Waoneshe kazi unaiweza, Wala usihangaike nao.
Binafsi niliumia sana,
Ulipotolewa bila la maana,
Nampongeza mama S sana,
Kwa kukuona na kukupa spana,
Waoneshe kazi unaiweza Wala usihangaike nao.
Ubeti wa mwisho namaliza,
Naomba hapa kukuhimiza,
Rudisha uhuru wa habari waliodumaza,
Magazeti yamedumazwa,utazani yanaandikwa na vilaza,
Hata kuyasoma hayana ladha.
Mwisho Nina maliza,na sasa naondoka, Kila la kheri Mkuu,piga kazi. Waoneshe kazi unaweza Wala usihangaike nao.