Hongera Sana Rais Samia kwa Miaka Miwili Madarakani. Japo Umefanya Mengi, Makubwa, Mazuri, Lakini Bado! Linalowezekana Leo, Lisingoje Kesho!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Wanabodi,

Hii ni Makala yangu ya Kwa Maslahi ya Taifa Jumapili ya leo, Tarehe 19 Mwezi Machi, ambapo leo ndio miaka miwili kamili ya Rais Samia madarakani, aliapishwa kuwa Rais wa Tanzania siku kama ya leo, miaka miwili iliyopita.



Kuna msemo wa Kiswahili usemao, "mgema akisifiwa, tembo hulitia maji".

Kuanzia leo na mpaka mwisho wa mwezi huu, vyombo vyetu vya habari, Radio, TV na Magazeti vitashehenezwa na makala za kusifu na kumpongeza Rais Samia kwa miaka yake miwili madarakani, haswa kwa kuangazia mambo mengi, makubwa na mazuri aliyoyafanya ndani ya hii miaka yake miwili madarakani, hivyo kama wote tutapongeza tuu kwa yaliyofanyika, hatutakuwa tunamsaidia Rais Samia, unless kama na Rais Samia ni Rais mpenda sifa kwa kufanya mambo kwa masifa ili watu waone wampongeze!.

Samia ninayemuona mimi hafanyi mambo kwa masifa ili watu waone au kufurahisha watu, anafanya mambo kwa ukweli ili mambo yaende.

Mtu wa namna hii anahitaji kuungwa mkono na watu wote ambao ni Wazalendo wa kweli wa taifa lao na wenye mapenzi mema na nchi yao, hivyo mimi nami, na Safu yangu ya Kwa Maslahi ya Taifa, yenye Fikra Mbadala, najiunga na Watanzania wengine wote kumpongeza Rais Samia kwa kutimiza miaka miwili madarakani.

Ila mimi badala ya kusifu tuu, kwa kuchelea mgema huyu tembo asije kulitia maji, mimi namsaidia mgema wetu kwa kumuangazia jambo moja kubwa muhimu kuliko yote ambalo lilipaswa kufanyika toka mwanzo, lakini bado halijafanyika.

Lengo la kuliangazia hili sio ili kumpangia kazi Rais wetu Samia, afanye hiki au kile, no!. Kwa mujibu wa katiba yetu ya JMT, Rais wa JMT hapangiwi!. Anaweza tuu kushauriwa lakini kwenye kufikia maamuzi, Rais wa JMT anafikia maamuzi yeye kama yeye kwa kufanya kile anaona kinafaa na halazimiki kufuata ushauri wowote wa yeyote, anafikia maamuzi yeye kama yeye hivyo hakuna ubaya wowote kumshauri jambo lolote rais wa JMT, na hiki ndicho ninachokifanya leo kwenye makala hii. Kwa vile wote sio wasomaji wa vitu deep, wale wa short and clear tuishie hapa na ku jump mwisho, wale wazama deep, tuzameni.
Hili la katiba na kumshauri rais Samia aliharakishe kwa utaratibu wa Linalowezekana leo lisingoje kesho ni kwasababu hata aliyelianzisha JK alilianzisha kiungwana tuu, halikuwemo ndani ya ilani ya uchaguzi ya CCM 2010- 2015. Likawekwa ndani ya Ilani ya 2015-2020, lakini Mwamba akasema sio kipaumbele chake!. Kuna akina sisi wa kizazi cha kuhoji, hili tulilihoji Kitendo cha Kukiuka Ilani ya CCM Bila Kikao Chochote, Sio Udikiteta?

Mimi niliamini kabisa Rais Magufuli angetuachia katiba mpya ki JK JK kwenye hili awamu yake ya pili licha ya katiba mpya kutokuwepo ndani ya Ilani ya CCM 2020 - 2025 na nikaandika humu JF vision yangu on JPM na katiba mpya Trends, Visions: Watanzania msitatizwe na kauli zake kuhusu Katiba, baada ya Nyerere, ni Magufuli ndiye ataacha legacy kubwa ikiwemo Katiba Mpya!.

Sasa japo hii ni awamu ya kwanza ya Samia ambayo yeye Samia hana ilani yake ila anaiendeleza ilani ya Magufuli, namshauri hili la katiba amalizane nalo kabla ya 2025.

Japo najua kwa vile CCM wameisha panga 2025 ni Samia na mchakato wa katiba mpya utaingizwa kwenye ilani ya uchaguzi ya CCM ya 2025 -2030 ambayo itakuwa ndio ilani ya Samia, ushauri wangu kwa Rais Samia, hili la katiba kama linawezekana kufanywa leo, lifanywe leo na lisingoje kesho maana tayari viji sauti sauti kuhusu 2025 vimeisha anza anza kama sauti HII hivyo nashauri tena na tena na tena, Linalowezekana leo lisingoje kesho!

Nampongeza Rais Samia kutimiza miaka miwili madarakani.
Mungu Mbariki Rais Samia
Mungu Ibariki Tanzania

Paskali
 
Sita mumunya. Mpeni pongezi zake anazostahili. Zangu mie na mimi zitakuja baada ya Uchaguzi 2025
Nuff said

Amani iwatawale
 
Wanabodi,
Hii ni Makala yangu ya Kwa Maslahi ya Taifa Jumapili ya leo, Tarehe 19 Mwezi Machi, ambapo leo ndio miaka miwili kamili ya Rais Samia madarakani, aliapishwa kuwa Rais wa Tanzania siku kama ya leo, miaka miwili iliyopita....
"Katiba haitakuletea menu mezani, hiyo ni kwa ajili ya wanasiasa' mwisho wa kunukuu.
 
Jambo la katiba mpya ni muhimu. Inshallah mama atalikamilisha.

Tumuombee sana.
 
maoni na mtazamo wangu BINAFSI juu ya uwepo wa haja kubwa ya Marekebisho ya haraka ya Katiba yetu ya JMT kulingana na mahitaji ya sasa. Marekebisho haya yafanyike haraka na mapema kabla ya Uchaguzi wa 2025
Mkuu Mkandara , hili ni ombi langu kama ombi lako kwa Mama, ajitahidi la katiba mpya amalizane nalo kabla ya uchaguzi Mkuu wa 2025.
P
 
Mkuu Mkandara , hili ni ombi langu kama ombi lako kwa Mama, ajitahidi la katiba mpya amalizane nalo kabla ya uchaguzi Mkuu wa 2025.
P
Katiba Mpya ni mchakato mrefu sana na nakuhakikishia haiwezi kupatikana kwa sababu hoja nyingi ni za Kisiasa kuliko haki za Wananchi.
1. Hawatakubaliana kwenye Serikali ngapi?
2. Hawata kubaliana kwenye kupunguza madaraka ya rais
3. Hawata kubaliana Ubunge wa.awamu mbili.
4.. Hawata kubaliana muundo wa uteuzi wa viongozi wa tume huru ya Uchaguzi.
Hawata kubaliana serikali ya Majimbo n.k

Nasema leo na kesho kuwa Sheria mama haiwezi kutokana na maoni ama mapendekezo ya WATU. Just imagine hata Biblia tumeshindwa kuwa na moja kwa sababu tumeruhusumaoni ya watu hivyo kila dhehebu limepingana na dhehebu jingine mahala itakuwa Katiba?. Rasimu ya Warioba haitapita ngazi yoyote ya maridhiano.. Mark my word..
 
Katiba Mpya ni mchakato mrefu sana na nakuhakikishia haiwezi kupatikana kwa sababu hoja nyingi ni za Kisiasa kuliko haki za Wananchi.
Ni kweli kupata katiba bora ni mchakato mrefu, ndio maana kwenye andiko hili nimeshauri tufanye lile linalowezekana leo, lisingoje kesho.
1. Hawatakubaliana kwenye Serikali ngapi?
Hili halihitaji kukubaliana, serikali 3 ndio suluhisho la kudumu la changamoto za muungano japo mimi ni Nyerererist maoni yangu ni serikali moja Kama kweli nia ya dhati ni kuimarisha Muungano, then "Twende kwenye Serikali Moja!"
2. Hawata kubaliana kwenye kupunguza madaraka ya rais
Halihitaji kukubaliana, madaraka ya rais lazima yapunguzwe na kukasimiwa na Bunge na Mahakama kwa ajili ya kuongeza ufanisi. Should We Demand More Right to Information Kwenye Teuzi za Key Posts? Ziwe Endorsed na Bunge With Security of Tenure? Mawaziri Wasiwe Wabunge?
3. Hawata kubaliana Ubunge wa.awamu mbili.
Hili halihitaji mjadala wala kukubaliana, kama kwenye urais limekubalika na kwenye ubunge litakubalika.
4.. Hawata kubaliana muundo wa uteuzi wa viongozi wa tume huru ya Uchaguzi.
Hili watakubaliana tuu kuunda tume huru Shirikishi.
Hawata kubaliana serikali ya Majimbo n.k
Tukiishakuwa serikali 3, hiyo ni federation tayari hivyo majimbo hayakwepeki!. Muungano lazima ujadiliwe kwa Ukweli na Uwazi! - Jaji Mark Bomani
Let's be positive
P
 
Ndugu yangu, baadhi ya vitu vinavyolalamikiwa ni pamoja na katiba mpya na tume huru ya uchaguzi. Je, kasi ya kushughulikia jambo hili anayoifanya SSH wewe inakuridhisha?
Natumaini jibu langu nimeliona.
P
 
Hakuna mwana CCM hata mmoja anayethubutu kudai Tume Huru ya Uchaguzi.
Wewe Paskali huwezi kuthubutu kudai Tume Huru ya Uchaguzi, hususan kwenye 'forum' za CCM.
Duh...!, Mkuu fundimchundo , karibu bandiko hili, jee hilo linalowezekana leo, lisingoje kesho ni nini hapa ninachodai?.
P
 

Hii ni zawadi yangu kwa Birthday ya Mama leo, nilipanga kumpa wiki ya mwisho ya October 2025,

Ili zawadi hii iwe na manufaa kwake, nikisubiri mpaka hiyo 2025, it might be a bit too little too late, kuna ubaya hiyo zawadi, kutolewa mapema mwaka huu ili iweze kutumika mwaka kesho?.

Zawadi yenyewe ni Salaam tuu za Birthday zenye ki parcel fulani!

HBD Mhe. Rais Samia kwa kutimiza miaka 64!, nakupongeza sana na kukuombea afya njema!.

Mwakani 2025 utakuwa unatimiza umri wa miaka 65 na 2030 utakuwa na umri wa miaka 70, hivyo zawadi yangu ya pekee kwako ni HII na kukusisitizia, sio lazima kuizingatia saana kivile, ila ni muhimu kuisikiliza na kujisikilizia kama na wewe pia uliambiwa kama nilivyoambiwa mimi, kwasababu yule YEYE, sometimes ana tabia na mtindo wa kuwaambia watu wake, kupitia kwa watu wengine!, hivyo just listen and try to make sense of this, a think about it, if makes any sense to you, ikitokea it doesn't make any sense to you, then dismiss it as just another set of crap!.

Ila ikitokea na wewe pia uliambiwa, but you are not very sure kama ni YEYE au ni yeye, then don't take a chance!, usipuuze!, maana hicho kitu chenyewe, is nothing compared!.

If this being the case, then tunakuomba sana sana sana, ututekelezee haya mambo tunayokulilia nayo tangu umeingia kwenye usukani, tekeleza tuu yale yaliyomo ndani ya uwezo wako, maana kusubiria post 2025, it might be too little too late!. Please Mama!.

Na ikitokea wewe hujaambiwa mpaka 2025 inaingia na hujawahi kuambiwa na mtu mwingine yeyote, then ipuuze HII itakuwa sio sauti yake YEYE bali itakuwa ni sauti ya yeye tuu ambaye sio YEYE!.

Hivyo endelea na ule mpango wako wa 2025!, na Watanzania wanaolitakia mema taifa letu hili, wote tutakuwa
Tuko nyuma yako,
Tuko pamoja nawe,
Tuko nawe!.

Mungu Akubariki Sana!.
HBD Mamaa!.
Paskali
 
Pongezi Raisi Ssmia kwa miaka 3 madarakani.
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…