Hongera sana Seba Maganga wewe ni ''champion'', hatimaye Fiesta imefanyika

Hongera sana Seba Maganga wewe ni ''champion'', hatimaye Fiesta imefanyika

Kama Kweli Ulienda Uwanjani Jana, basically Seba na team yake wameproove kwamba wanahitaji performance Kubwa Sana, idadi ya Watu sio Inayotakiwa na kile Kiuwanja ni Kidogo Sana
Nachukua nafasi hii kumpa heko new mastermind wa Clouds ndg Sebastian Maganga kwa kuweza kufanikisha show ya Fiesta. Juzi niliandika uzi wa kuonyesha wasiwasi wangu kuhusu show kutopata wahudhuriaji kabisa, lakini hali imekuwa tofauti na washabiki japo sio kama ilivyozoeleka walijitokeza si haba.

Hii inaonyesha kwamba haukuweka silaha chini umepambana bila uwepo wa Ruge na tamasha limefanyika.

Kuhusu kukonga nyoyo za mashabiki na mahudhurio sitopenda nilizungumzie kikubwa ni show imefanyka. Hongera sana na kiasi fulani mmepata cha kujifunza!

View attachment 975187

Juma Nature hongera pia kwa kuwa man of the show

View attachment 975189
Mashabiki wakipata vibe la kutosha

View attachment 975197

View attachment 975199
 
Binafsi sidhani kama ni upinzani ila kwa sasa hali ya uchumi kwa watu wa kati imezorota na sio matamasha tu hata biashara ya kawaida imekuwa ngumu sana dec iko chini sana
Ni kweli ila nafikir ata wenyewe wanaonekana kuweweseka na huu upinzani wa diamond, uchumi ni moja lakini pili kupoteza mvuto watu wanataka vitu vipya
 
Wamejitahidi na kumwalika DAB maana alisikika akimwombea Ruge apone mapema
 
Back
Top Bottom