Eswa
JF-Expert Member
- Dec 14, 2012
- 231
- 617
Ni imani yangu sote tu wazima wa afya.
Nina muda mrefu sijavuka kwa panton kwenda kigamboni takribani miakai minne sasa, japokuwa ninaishi Dar es Salaam. Leo katika ratiba za mishemishe zangu hapa mjini, ratiba moja wapo ilinilazimu niende Kigamboni, wakati wa kwenda nilipita darajani ila kurudi ikabidi nipande panton ili nifike Posta. Sasa nilichokiona kimenifanya niandike huu uzi (Na sisitiza haya nimeyaona upande wa Kigamboni, huku magogoni sikupita)
1. Matumizi ya card badala ya tiketi za karatasi (hii ipo kwa pande zote) hii imeleta unadhifu na usafi wa mazingira, zamani zile tiketi za karatasi zilikuwa zinachwa ovyo na kusababisha uchafu kila mahali.
3. Sikuwa na Card ila nilipoomba mwongozo kwa watoa huduma, nilielekezwa vizuri tena kwa lugha nzuri, kuwa unaweza kumwomba abiria aliye na card yenye salio ukampa 200, aki-swipe akishaingia anakupa card then na wewe una-swipe, sikulazimishwa kununua card (Good customer care service).
2. Eneo la kusubiria abiria - Zamani lilikuwa ni jengo moja, wakati wa asubuhi palikuwa panajaa sana hadi kupelekea wengine kukaa nje, ila kwa sasa yapo majengo mawili. Pia uwepo wa huduma bure ya choo na vikiwa visafi; Awali ulikuwa unalipia 200 na hii imekuwa kero kwa abiria kwenye vituo vya mabasi, unalipishwa 200/300 ukitaka huduma ya choo unalipa tena 200, naona wameamua kuwa mfano mzuri na tunatarajia upande wa vituo vya mabasi watafanya hivyo.
Hongereni sana TEMESA - Kigamboni.
Nawasilisha.😊