SoC02 Hongera Serikali kwa mikopo ya Halmashauri: Kuwepo na elimu zaidi, ufatiliaji na uboreshwaji wa kanuni wenye kuendana na mazingira na uhitaji

SoC02 Hongera Serikali kwa mikopo ya Halmashauri: Kuwepo na elimu zaidi, ufatiliaji na uboreshwaji wa kanuni wenye kuendana na mazingira na uhitaji

Stories of Change - 2022 Competition

Tonytz

Senior Member
Joined
Jul 18, 2022
Posts
159
Reaction score
1,142
Utangulizi
Mkopo ni fedha zipatikanazo kwa makubaliano ya kuzirudisha (maana kutoka kamusi ya Kiswahili sanifu, toleo la tatu-2014). Lakini kuna mikopo ya thamani kama vile nyumba, magari na ardhi.

Mpango wa pili wa Taifa wa maendeleo wa miaka mitano(2016/17-2020/2021), pamoja na malengo mengine, unakusudia kuweka mazingira wezeshi kwa vijana, wanawake na watu wenye ulemavu kujiajiri na kushiriki katika shughuli za kiuchumi kama vile kilimo, ufugaji na uzalishaji wa bidhaa mbalimbali (Nukuu kutoka kikundi kazi cha Tawala za Mitaa cha Policy Forum, 2019).

Miongoni mwa mikakati ya kutimiza lengo hilo iliyoainishwa katika mpango huo ni utoaji wa mikopo yenye gharama na masharti nafuu kwa vijana, wanawake na watu wenye ulemavu. Katika kutekeleza mkakati huo, sharia ya fedha ya serikali za mitaa, sura ya 290 ilifanyiwa marekebisho mwaka 2018 ili kuweka masharti kwa halmashauri zote nchini kutenga fedha kwa ajili ya mikopo kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu. Kwa kufuatia marekebisho hayo, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa ilitunga kanuni zitakazoainisha masharti ya utoaji na usimamizi wa mikopo inayotolewa na halmashauri kwa vikundi hivyo (Nukuu kutoka kikundi kazi cha Tawala za Mitaa cha Policy Forum, 2019).

Katika Makala yangu hii nitazungumzia Zaidi kuhusu kanuni na masharti za upataji mikopo na changamoto zake kulingana na uhalisia, usimamizi, uenezwaji wa elimu kwa jamii juu ya mikopo hiyo, changamoto za michakato wazipatazo wahitaji katika zoezi zima la upataji mikopo hiyo. Pia nitazungumzia ni vipi wanasiasa wanavyofanya mikopo hii isionekane na tija bali kuwa ni sehemu ya kupatia umaarufu wa kisiasa na mwisho nitatoa mapendekezo na hitimisho.

Katika uhalisia, kanuni zilizowekwa na masharti yake kwa namna moja au nyingine huwa ni kikwazo cha mikopo hii kuwafikia watu wengi katika jamii. Mfano (kanuni ya 6), Katika kanuni hii inataka watu wawe kwenye vikundi vya watu kuanzia 10 kwa wanawake na vijana, lakini watano kwa watu wenye ulemavu. Hapa inakuwa zuio kwa mtu mmoja mmoja menye uhitaji na menye vigezo kuchukua mkopo huo.

Mikopo hii haina riba. Lakini ukija katika uhalisia utaona mikopo hii kama inariba tu kwani, watendaji waliopewa dhamana ya kusimamia hasa ngazi ya halmashauri wamekuwa ni watu wa kutaka kupata shukrani Fulani kiasi kwamba kwa kikundi huwa inawapasa walipe kiasi Fulani cha pesa ili fomu zisainiwe na kupokelewa.

Screenshot_20220822-143458_1.jpg

Picha: kutoka mtandaoni.
Katika upande mwingine (kanuni ya 7), imetaja viambatanishi vya kupata mkopo. Miongoni mwa viambatanisho hivyo ni “katiba ya kikundi”. Uwepo wa katiba ni mzuri sana. Hapa tatizo linakuja kuwa maeneo mengi hasa kwa halmashauri za vijini, wanawake, vijana na wanufaika wengine hawana uelewa wa namna ya kuandika katika hizo na kinachofata hapa ni hali ya kikundi kimoja kunakili katiba ya kikundi kingine ambacho kwayo kimefanikiwa kupata mkopo.

Mikopo hii kihalisia inatoa kipaumbele kwa kuzingatia itikadi za kisiasa kwa eneo husika. Watu wengi wanaonufaika na mikopo hii ni wale wa chama ambacho kinashika Dola, sijamaanisha kuwa wengine hawazingatiwi, nimetaja kundi ambalo linanufaika sana. Mbali na sababu ya itikadi, kuna suala la mahusiano ya waomba mkopo na mwenye kutoa mkopo wa eneo husika.

Kuna mfano halisi kuna halmashauri Fulani (halmashauri mpya) kuna vijana wamekopeshwa pikipiki maarufu Bodaboda, lakini nilipowahi kuongea na mmoja anasema “daaah..!! Mbunge wetu yupo vizuri sana, ametukopesha pikipiki hizi” picha halisi inayonijia hapa ni kuwa wanufaika wengine wanaamini wabunge ndiyo wanatoa na siyo wazo au jitihada za serikali iliyopo madarakani. Hivyo wanasiasa wanatumia mianya ya mikopo hii kujipatia umaarufu na kujitengenezea njia ya kuchaguliwa kwa baadaye na serikali kuonekana butu tu.

Kushindwa kurejesha mkopo. Na kiini cha hili tatizo ni kukosekana kwa elimu ya kutosha na kupeana mikopo kwa kujuana pasipokuzingatia vigezo na ufatiliaji hafifu. Kwa mfano, kuna baadhi ya mikoa wakuu wa mikoa waliziua mikopo na kutaka elimu itolewe kwa jamii.

Screenshot_20220817-232346_1.jpg

Picha: mtandaoni

Kanuni haisemi endapo mwankikundi amefariki, kwa upande wa rejesho inakuwaje? Je rejesho litapunguzwa au litafutwa au litaendelea?

Suala la kiwango cha pesa kuwa cha namna moja(uniform amount) kwa wanakikundi wote nalo halina tija kwani humnyima uhuru mwenye uhitaji wa kutimiza malengo yake.

Kanuni ya 13 na 14, suala la kufatilia uhai na maendeleo ya vikundi, katika uhalisia limekuwa ni andiko tu kwani kwa sehemu kubwa hakuna ufatiliaji. Ufatiliaji wa vikundi umekuwa finyu na pia usimamizi kuhakiksha mikopo inatumiwa kama ilivyokusudiwa, katika uhalisia, hakuna ufatiliaji huo na watu wanachukua mikopo na kufanyia mambo mengine ambapo mwishoni huwa ngumu katika marejesho kwa miradi mingi kufa.

Screenshot_20220817-234148_1.jpg


MAPENDEKEZO;
  • Kuwepo na kanuni na masharti yenye kutekelezeka ya kumuweza mtu mmoja mmoja kuchukua mkopo ikiwa tu amekidhi vigezo na siyo mpaka wawe kwenye kikundi Fulani.
  • Katika halmashauri kuwe na kitengo mahususi kinachohusika na mchakato wote hadi mtu kupata mkopo na siyo mfumo wa kuanzia katani ambapo katika uhalisia wanakikundi wanahitajika kutoa fungu kidogo.
  • Kuwepo na elimu juu ya uaandaaji wa katiba yenye kutekelezeka kwa vikundi, au la kigezo hicho kiondolewe au itafutwe namna. Kwa mfano. halmashauri waziandae kwa ajiri ya wahitaji kisha kikundi kitakachokidhi vigezo kipewe elimu kulingana na katiba mradi wao. Kimtazamo yawezekana ikawa ni njia ya halmashauri kujipatia mapato kwa kuzalisha katiba hizo.
  • Serikali iangalie namna bora ya kukomesha wanasiasa kutojihusisha kwenye mikopo hii ili kuondoa ukiritimba wa kisiasa.
  • Suala la elimu kwa vikundi husika lizingatiwe, litiliwe mkazo na elimu iwafikie wanajamii wote na wale waliochukua na wanaohitaji mikopo. Itasaidia sana katika urejeshwaji wa mikopo hiyo. Matangazo kwenye ofisi za halmashauri peke yake haitoshi.
  • Kuwepo na kanuni inayoelezea wazi endapo mwankikundi amefariki, hatma ya mkopo hasa kwenye rejesho inakuwaje?
  • Wahusika wa kufatilia katika kukagua miradi ya vikundi, kufatilia maendeleo ya vikundi, wawe wanatoa taarifa kamili kwa sekta ya mikopo hiyo ili kuweza kuwakopesha wanaostahili.
  • Serikali iangalie utaratibu wa mwanakikundi ndani ya kikundi aruhusiwe kupata mkopo kulingana na mahitaji yake na kiasi atakacho ili kuepusha kuandikisha majina hewa.
HITIMISHO.
Naipongeza serikali kwa jitihada wanazozichukua ili kufikia malengo yaliyokwenye Dira ya Taifa ya Maendeleo. Lakini kila jitihada yenye kuleta maendeleo inahitaji ushirikiswaji wa jamii inayohusika. Elimu Zaidi itolewe kwa jamii ili mkopo iwafikie wengi. Pia ngazi za juu za serikali ziwe zinakuja kutembelea miradi ya wanufaika ili kuona kero na uendeshwaji, hii itasaidia katika uboreshaji wa baadhi ya kanuni na masharti ya mkopo.

Screenshot_20220822-143113_1.jpg

Picha: mtandao
Screenshot_20220817-233351_1.jpg

Picha: mtandaoni.
 
Upvote 52
Kwenye uandaaji wa katiba kunapoteza muda sana. Maana mnaweza mkaandika mkapeleka mkakataliwa, mtarekebisha,mtakataliwa. Mpaka ikamilike ni muda sana
 
Hata Mimi naipongeza sana serikali kwenye mkopo huo. Kikubwa kanuni ziboreshwe na usimamizi uwe wa karibu zaidi. Maana wengine wanazitumia pesa hizo ndivyo sivyo.
 
Kuna baadhi WA wanawake na vijana wanachukua mikopo hii Kwa kufata mkumbo TU, wengi wamekimbia miji Yao Kwa kushindwa kurejesha mkopo huo. Elimu zaidi itilewe kwa imma.
 
Mawazo mazuri sana sana. WENGI wanatamani hii mikopo,tatizo hakuna ELIMU ya kutosha na hofu zimetanda akilini mwetu
 
Mikopo itilewe kwa kuzingatia vigezo,lakini kulingana na mazingira ya sasa,izingatie uhitaji kulingana na vigezo.
 
Back
Top Bottom