1. Simba na Yanga hongera, kujipa nguvu nyumbani
Mmeonesha ubora, bara pia visiwani.
Mmeionesha dira, kwamba mmekuza Fani
Kaza buti msikwame, shikilia hapohapo
2. Kaza buti msikwame, shikilia hapo hapo.
Msitari msihame, kwepa tabia ya popo.
Kwa kabumbu mjitume, kataa kuwa makopo.
Kaza buti msikwame shikilia hapohapo
3. Kwenye hili Simba yanga, muutafute Umoja.
Hapo ndipo kuna mwanga, mkiufunga mkaja.
Mtayaleta majanga, kwa ugomvi uso tija.
Kaza buti msikwame shikilia hapohapo
4. Niseme neno la mwisho, kabula wino kuisha.
Ushindi huja kwa jasho, mazoezi mkikesha.
Bila kutazama Posho, cheza bila kujikosha
Safari mliyoanza iwe njema kwa ushindi