Hongera Tanzania yote yawezekana

Kafika namba tano, hapo amejaribu, labda aishi Kenya kwa muda ili apate uzoefu. Halafu naona kama huyu dogo ni jamaa wa Arusha, watu wa pale wana hulka za Kikenya na akiendelea hivi atakuja ibuka na medali. Anyway hongera zake, kumaliza hizo kilomita zote na pia kubaki ndani ya tano bora ni jambo la kutia moyo, anafaa kutiwa hamasa na kuungwa mkono, apokelewe kishujaa ili iwaamshe na wengine wanaotaka kujiunga na riadha......ila nina mashaka na Bongo, sidhani hata kama wana muda naye.
 
Kwa hiyo mtu ukitoka arusha una hulka ya Kikenya..

Saa zingine sio lazima u post.. unaweza kukaa kimya tu.
 
Kwa hiyo mtu ukitoka arusha una hulka ya Kikenya..

Saa zingine sio lazima u post.. unaweza kukaa kimya tu.

Watu wa pale waligawanywa na mzungu, kaja na kuchora mpaka katikati na ndugu na kuita wa huku Mkenya na wa kule Mtanzania. Leo hii utakuta Mmaasai mjomba wake Mtanzania, shangazi Mkenya, binamu Mtanzania n.k.
Walichanganywa kweli kweli. Wamaasai wanaanzia Arusha na kuingia Narok, kajiado Kenya. Nenda pia kwa Wakuria au Wajaluo wa Tanzania pale Musoma na Wajaluo wa Kenya. Hawa watu wote walikua mandugu, mzungu kachora mpaka usioonekana kwa macho na kuanzia hiyo siku wanaonana kwa misingi ya nchi.
 
Kweli kabisa maana wakenya wa pwani wapo sawa na wa pwani ya Tanzania kwa uvivu

Kwa hiyo hata wavivu wa dar nao wana hulka za kikenya .....
 
Kweli kabisa maana wakenya wa pwani wapo sawa na wa pwani ya Tanzania kwa uvivu

Kwa hiyo hata wavivu wa dar nao wana hulka za kikenya .....

Nakuona kwa mbali unavyotaka kuileta hiyo twist, jameni Dar na Mombasa kuna umbali mkubwa sana, 500km hamna undugu pale, naongea kuhusu watu wanaoishi mipakani. Kwa mfano nenda pale maeneo ya Taita Taveta Kenya na upande wa pili wa Tanzania uone wanavyochakarika Kikenya.....hehehehe.

Anyway, hii mada mnaigeuza wenyewe, mimi namualika yule jamaa aje akimbie na Wakenya. Yeye ametokea Arusha na kwa vile watu wa pale wana uzoefu mkubwa wa kuishi na Wakenya na wana undugu, hivyo hataona ugumu wowote na atahisi yupo nyumbani tu. Nina uhakika ndani ya miezi michache atakua ana uwezo wa kunyakua medali.
 
Hulka za kikenya ni zipi labda?
 
ni watu 15 pekee waliomaliza hio marathon kutoka 155 walio anza kwahivyo msijidharau kabisa, kua namba 5 si jambo dogo
 
Ni mtu wa Singida huyo na sio Arusha, ongea vitu unavyovijua bosi acha kubahatisha.
 

unaonekana kama mtu mwenye upeo mdogo wa kitamaduni na pengine hujui ni kwa nini watu wa pwani ya afrika ya mashariki huwekwa katika sampuli moja ya kihistoria , hebu Rejea katika historia ya ushawishi wa waarabu katika pwani hii................

watu wa mombasa wana ndugu zao wengi tanga na zanzbar lakini waliopo dar ni wachache.....

usijitie upofu kwa kuwa mombasa haikupata kuwa jiji kuu la kenya kibiashara na kiserikali ndio maana hamkupata kuitwa wavivu na mliopo slow lakini cha kushangaza mkifika dar ndo mnaweka conclusion zenu kuwa watanzania ni wavivu kwa kuwa nyie mnadhani kenya inaishia nairobi bila pwani na pia tz inaishia pwani bila bara.........

huu ni udhembe wa kufikiri ambao ni mbaya kuliko hata wa kufanya kazi
 
MK254 hivi hua una kazi nyingine tofauti ya kuipondea Tz?
Unajiita programmer, inashangaza sana sijawahi ona programmer mwenye tabia zako. Unapenda arguments za kitotototo
 

Naona unajichanganya uliuliza kuhusu Dar. Nikakuambia Wakenya hawana undugu na watu wa Dar. Hatuna undugu na hao unaowaita wavivu wa Dar.
Wakenya wetu wa Pwani wana undugu na Watanzania wa Tanga na hadi kule Unguja na Pemba.
 
Congratulations to the Tanzania for finishing 5 th...If he had known that the American ahead of him was running out breathe,he could have taken a medal home...
 
MK254 hivi hua una kazi nyingine tofauti ya kuipondea Tz?
Unajiita programmer, inashangaza sana sijawahi ona programmer mwenye tabia zako. Unapenda arguments za kitotototo

Jadili mada wachana na personal attacks. Huu ni mtandao wa kijamii kila mtu ana uhuru wa maoni. Ukiona yanakushinda unabaki kimya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…