Hongera TCU na UDSM kwa uamuzi huu wa busara

Hongera TCU na UDSM kwa uamuzi huu wa busara

Ngalikivembu

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2010
Posts
1,959
Reaction score
876
WanaJF,Salam.
Nimeona nichukue nafasi hii tena kuwapongeza TCU na UDSM kwa uamuzi wao wa kutupilia mbali baadhi ya majina ya waliokuwa wanafunzi watarajiwa katika chuo kikuu cha DSM yaliyoletwa na Mamlaka ya Hali ya Hewa kwa ajili ya kujiunga na course ya Meteorology.Itakumbukwa kuwa ni hapa hapa JF niliandika kuhusiana na uchaguzi wa wanafunzi wa course ya Meteorology ambayo ni mpya hapo UDSM. Nilisema kuwa watu waliochaguliwa kujiunga hapo hawana sifa.
Nilipendekeza na kuhoji kwanini wasipewe kipaumbele vijana hasa wasichana waliochukua masomo ya sayansi ikizingatiwa kuwa atakayekuwa amemaliza course atapewa ajira ya moja kwa moja kwani hakuna mwajiri mwingine zaidi ya TMA.Hii ingekuwa ni motisha kwa wasichana kupenda masomo hayo.

Nilihoji uhalali wa kuwachagua wanafunzi hao kabla ya muda wake.Leo hii chuo na TCU wametoa majina ya wanaojiunga na course na wengi wao wamaeachwa na hii nadhani huenda zile sifa nilizosema walionekana dhahiri hawana.

Hapa tazama majina ya awali ya waliochaguliwa na linganisha na orodha mpya ya TCU kwenye course hiyo.
Nimekata kipande tu cha majina ya course husika.

Kwa wakuu waliopitia JF nadhani waliona malalamiko yangu na sina hakika kama ndio walitendea kazi au la.Ila Nimefarijika.
 

Attachments

  • Admission Udsm 2013-14.xls
    Admission Udsm 2013-14.xls
    184 KB · Views: 169
  • Provisional Names.JPG
    Provisional Names.JPG
    40.2 KB · Views: 294
Bora hivyo maana kuna rafk yangu anafanya kazi huko ana sifa za kijinga aliniambia watu watakaosoma hio course ni watu wao tu..kumbe wamezinguliwa..maana wengi ni form6 waliopata daraja za ajabu ajabu
 
Back
Top Bottom