SN.BARRY
JF-Expert Member
- Oct 12, 2012
- 4,038
- 8,929
1. Umemuonyesha Magufuli na Ndugai ukuu wa Mungu. Umepona, umerudi na watanzania wote wameshuhudia kuwa Mungu ni mkuu sana.
2. Wale waliokupiga risasi, wakazuia usitibiwe, wakakunyima mshahara na kukuvua ubunge sasa wanatakiwa kutubu mbele za Mungu na mbele za watanzania.
3. Umemuonyesha Magufuli na waliokuwa wanamdanganya kuwa upinzani umekufa kuwa watanzania sio wajinga. Upinzani upo kwenye fikra za watu. Upinzani hauwezi kuondoka kwa maagizo kutoka juu au kwa kutumia polisi na TISS.
4. Umeweza kuzunguka mikoa kadhaa kutoa elimu ya uraia na umeona jinsi muitikio wa watu ulivyo mkubwa. CCM imechokwa.
5. NEC, Polisi na TISS hawatakutangaza kuwa umeshinda. Ila ukweli utabakia kuwa Magufuli hata akitumia mabavu bado atakuwa sio rais halali wa watanzania. Atakuwa rais halali wa NEC na Polisi ila sio watanzania.
6. Hata kama wakikuzuia kufanya kampeni kuanzia leo bado wataonekana wajinga na waovu. Watanzania wanataka haki na uhuru.
7. Kanda ya ziwa wamemuonyesha magufuli kuwa siasa chafu za ukabila hazitakiwi Tanzania huo ni ujumbe tosha. Kama ana akili timamu atabadilika.
NEC WATANGAZE AU WASIKUTANGAZE BADO UTABAKIA KUWA MSHINDI.
wale waliosema uzikwe ndani ya siku tatu bado hawaamini macho yao.