Kweli mkuu haya mambo yanaumiza sana. Hawa mashetani ndio huwa wanaenda kanisani na kukaa siti za mbele. Aibu sana kwa kanisa la Tanzania.
KANISA LA TANZANIA LIKO IMARA NA HALITABADILISHWA NA WATU KWA KUWA:-
Kanisa ni mwili wa Kristo. Watu waliosikia habari za wokovu wa Yesu Kristo, Wakaamini na kumpokea Yesu, naye akawapiga Muhuri wa Roho Mtakatifu. Efeso 1: 13.
Kanisa la Kristo ni watu ambao Yesu anaishi ndani yao kwa njia ya Roho Mtakatifu ambao wanaungamanishwa katika Yesu Kristo. Efeso 2;22.
WATU WANAOKWENDA KANISANI WAKATI HAWANA YESU KRISTO BIBLIA IMEWASEMA HIVI:-
1) WATU WAPAGANI WALIOJIINGIZA KWA SIRI KANISANI Yuda 3 - 4.
2) Mungu hawatambui kama ni Wakristo japo wanaingia kanisani.
1 Korintho6:9-11
Je, hamjui kwamba wasio na haki hawataurithi Ufalme wa Mungu? Msidanganyike, waasherati hawataurithi Ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wapotoshaji; 10 wala wezi, wala wenye tamaa mbaya, wala walevi, wala wanaodhihaki, wala wanyang’anyi. 11 Na baadhi yenu mlikuwa kama hao. Lakini mlioshwa, mlitakaswa, mlihesabiwa haki kwa jina la Bwana Yesu Kristo na katika Roho wa Mungu wetu.
CHOTE KINACHOIGA TARATIBU ZA IMANI YA KRISTO KWA NJE LAKINI KIHALISIA SICHO, AWE MTU BINAFSI AMA KANISA SI MWILI WA KRISTO BALI NI MAGUGU ALIYOPANDA SHETANI. NA BADO HAYANA UWEZO WA KUITWA KANISA BALI NI MAGUGU.
Mathayo 13:24-30.
24 Yesu akawaambia mfano mwingine, akasema, “Ufalme wa mbi nguni unaweza kufananishwa na mtu aliyepanda mbegu nzuri katika shamba lake. 25 Lakini watu walipokuwa wamelala, adui yake aka ja akapanda magugu katikati ya ngano, akaenda zake. 26 Ngano ilipoota na kuzaa, magugu nayo yakachipua.
27 “Watumishi wa yule mwenye shamba wakamwendea, wakamwul iza, ‘Bwana, si ulipanda mbegu nzuri shambani mwako? Imekuwaje kuna magugu?’ 28 Akawajibu, ‘Adui ndiye amefanya jambo hili’. Wale watumishi wakamwuliza, ‘Sasa unataka tukayang’oe?’ 29 Lakini akasema, ‘Hapana msiyang’oe, kwa maana huenda katika kung’oa magugu mkang’oa na ngano pia. 30 Acheni ngano na magugu yakue pamoja mpaka wakati wa mavuno. Wakati huo nitawaambia wavu naji wayang’oe magugu kwanza wayafunge katika mafurushi tayari kwa kuchomwa moto, lakini wavune ngano na kuikusanya ghalani mwangu.’ ”
ANGALIA UFUNUO WA YOHANA 21:8
"Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili."
ANGALIA WAGARATIA 5:19-21
19 Basi matendo ya mwili ni dhahiri nayo ni haya: uasherati, uchafu, ufisadi, 20 kuabudu sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, mafarakano, uzushi, 21 husuda, ulevi, ulafi na mambo mengine yanayofanana na hayo. Nawaonya, kama nilivyokwisha waonya kabla, kwamba watu watendao mambo kama haya, hawataurithi Ufalme wa Mungu.
KILA ATENDAYE DHAMBI, HAIJALISHI ANAINGIA KANISANI AMA HAINGII, HUYO SI WA KRISTO NA SI MWILI WA KRISTO AMBALO NI KANISA. BALI NI MTU WA IBILISI. IBILISI SIYO KANISA ILA ANAWEZA KUWA NA WAWAKILISHI WAKE MAHALA POPOTE. WAKALA WA SHETANI HATA AKIWA KANISANI AMA AKAWA NA KANISA LAKE, BADO SI KANISA LA MUNGU. POPOTE ANAPOKUWA YEYE HUFANYA KAZI YA SHETANI AMBAYO NI "KUCHINJA, KUIBA NA KUHARIBU>
ATENDAYE DHAMBI NI WA IBILISI. KWA HIYO KANISA LA TANZANIA LIKO IMARA KWA KUWA LIMEJENGWA KATIKA YESU KRISTO. LINAMTAMBUA BWANA NA BWANA YESU ANALITAMBUA.
1 YOHANA3:8