JAY THE SON
Member
- Nov 26, 2017
- 43
- 33
Siandiki bandiko hili nikitarajia ujira wowote katika kuandika haya na wala siandiki hili kwa kuwa tunatokea Tanga tena mwahako bali naandika kama raia mwema ninayetambua na kuheshimu uchapakazi wako na ifikie mahali tutambue na kuwatia moyo viongozi wanaochapa kazi kwa moyo kwa maslahi mapana ya nchi yetu.
Utendaji kazi wako usikivu wako kasi yako katika kufika katika maeneo yenye changamoto yanazidi kukuongezea sifa za utandaji kazi ulianza vyema na kufanya kazi nzuri chini ya wizara ya afya, wizara ya ofisi ya makamu wa rais mazingira japo hukukaa sana na sasa wizara ya ofisi ya rais Tamisemi ninayo matumaini makubwa kuwa utafanya mambo makubwa na mazuri zaidi mungu akusimamie na kukutetea zaidi mie kama sehemu ya vijana wa tanga na mtanzania kwa ujumla kutojilaumu dhidi ya kura zetu tulizopiga kukuchagua wewe na viongozi wengine kazi iendelee na unayoyafanya yaendelee kwa viongozi wengine ukizingatia safari yako ni wazi bado ni ndefu katika kutumikia nchi yetu.
Zaidi ya yote wanna tanga mjini tunakuunga mkono tupo pamoja nawe na tutakuombea zaidi chapa kazi mbegu unayoioanda leo itkuja kumea na kuzaa matunda mema kwa vizazi vijavyo na vyaleo.
Jamhuri ya muungano wa Tanzania.