Hongera Wakenya kwa kukuza lugha ya Kiswahili Sudan Kusini

Amani haiwezi kuwepo kusipo kuwepo viongozi wenye utashi,, kama huku Tanzania hakuna kiongozi mwenye utashi,, wote wachumia matumbo yao,, bora akuae abaki madarakani,,
Nyie mna amani. Viongozi wenu ni wazuri. Zunguka katika nchi zingine za Afrika ndio utafahamu maana ya neno "viongozi wabaya"
 
Takriban 95% ya Wakenya wanajua kuongea kiswahili. Nadhani chini ya 35% ya Wakenya ndio wanaoweza kuongea kwa kiingereza. Kwa hivyo kiswahili ndio lugha ya kwanza hapa Kenya. Tembea Kenya ujionee, usingoje kuelezewa.
Iweje shughuli zenu zote za serikali zinafanyika kwa Kiingereza, ina maana zinawalenga 35% ya raia?. Iweje rais wenu anapotoa hotuba za Kitaifa anatumia Kiingereza, Je lengo lake ni kutaka azungumze na 35% ya wananchi wake pekee?
 
Mimi nilichokuelezea ndio ukweli. Njoo Kenya uone kama nadanganya. Halafu Kenya ina lugha mbili za kitaifa Kizungu na Kiswahili. Kwenye hotuba za Rais ni kweli huwa anazungumza kwa kiingereza ila hio haibadilishi ukweli kwamba Wakenya wengi zaidi ya 90% wanaweza kuzungumza kiswahili ila Wakenya waliosoma pengine hadi sekondari ndio wanaoweza kuzungumza kiingereza. Mkenya wa kawaida akienda kwenye ofisi za serikali huwa anazungumza kwa lugha ya kiswahili maana haelewi kiingereza na huwa anasaidika. Kiswahili ndio lugha inayotumika hapa Kenya na wananchi wa kawaida asikudanganye mtu. Njoo ujionee ama uulize Watanzania wenzako walioishi Kenya watakuelezea. Sema Kiswahili chetu ni tofauti na chenu hio ni kweli lakini tunaelewana bado bila tatizo. Mtz akizungumza Mkenya anamuelewa na Mkenya akizungumza Mtz anamuelewa. Ni kama tofauti ya kizungu cha Marekani na UK. Wanaelewana ila kizungu chao kina tofauti fulani.
 
Mimi nimekubali na Kenya nimefika mara nyingi Sana. Jambo linalonishangaza ni kwamba viongozi wenu hawajitambui kabisa, hapa duniani nimepata bahati ya kutembelea nchi mbalimbali, sijawahi kuona Wala kusikia nchi yoyote ambayo shughuli za Kitaifa zinaendeshwa kwa kutumia lugha inayoeleweka na watu wachache na kuacha lugha ya taifa inayoeleweka kwa watu wengi

Kenya lugha ya Kiingereza inathaminiwa na kutukuzwa zaidi ya Kiswahili, 99% ya magazeti yenu yanaandikwa katika lugha ya Kiingereza, 90% ya vipindi vya TV stations ni Kiingereza.

Ni Sasa hivi tu, hasa baada ya Bongo flavor kukubalika na Magufuli kuingia madarakani na kuanza kukikuza Kiswahili duniani ndio wakenya wanaanza kukikubali, kabla ya hapo Kiswahili Kenya kilionekana ni lugha ya "second class citizens in Kenya"
 
Niko huku Sudan Kusini nasaka mpunga kwenye mishe fulani hivi na nimefaulu kukatiza maeneo mengi na kushududia namna Wakenya wamehusika pakubwa kwenye kubadilisha maisha ya hawa watu waliokua wamezoea vita maporini. Kiswahili kinazidi kutamalaki na kuzagaa, leo hii kuna ushindani mkali baina ya Juba Arabic, Kingereza na Kiswahili na kwa namna fulani Kiswahili kinapenya kwa kasi.

Wasudan wengi wamesomea Kenya na kurudi huku na kushika nyadhifa muhimu muhimu, pia shule nyingi za maana zina walimu Wakenya au hao Wasudan waliorudi baada ya kusomea au kuishi Kenya. Kinatumika mtaani, maofisini na nilishangaa kwenye vyombo vya habari wanachomekea sana maneno ya Kiswahili kwenye mada zao hata wakati wanajadili kwa matumizi ya lugha zao za asili kama vile Dinka.

Ni muda tu, rais hatakua na budi ila kukifanya mojawapo wa lugha za taifa, maana mawaziri wake na wabunge wote, watoto wao wanasomea Kenya na hurudi nyumbani wameiva wakiwa tayari kwenye ujenzi wa taifa.

Uganda tu ndio niliwashangaa nilipokua kwao, wameshupaza shingo, wamekomalia Kingereza fulu, unakuta mtu aidha umuongeleshe kwa Kiganda au Kingereza, hajui neno hata moja la Kiswahili.
Waganda ushamba umewazidi wale,wanauhusudu sana uzunguzungu kuliko uafrika wao
 
Kumbe mnajua heshima na umuhimu wa Kiswahili eh? Sasa mbona hadi leo mnaona dili sana mtu kujua Kiingereza tu na huwa mnawakejeli watanzania wasiojua Kiingereza je hao Waganda wanaojua sana Kiingereza wako wapi kimaendeleo?

Anyway hongereni na endeleeni kupambana kukisambaza huko nchi za Kaskazini sisi huku tunapambana kukisambaza kwenye nchi za Kusini maana Zambia nao wataanza kukifundisha mashuleni na kukitumia mitaani! Soon kitasambaa Africa nzima!
 
Mimi nqombq

Hiyo connection ya sudan kusini vipi😁
 
Mimi nilichokuelezea ndio ukweli. Njoo Kenya uone kama nadanganya. Halafu Kenya ina lugha mbili za kitaifa Kizungu na Kiswahili. Kwenye hotuba za Rais ni kweli huwa anazungumza kwa kiingereza ila hio haibadilishi ukweli kwamba Wakenya wengi zaidi ya 90% wanaweza kuzungumza kiswahili ila Wakenya waliosoma pengine hadi sekondari ndio wanaoweza kuzungumza kiingereza. Mkenya wa kawaida akienda kwenye ofisi za serikali huwa anazungumza kwa lugha ya kiswahili maana haelewi kiingereza na huwa anasaidika. Kiswahili ndio lugha inayotumika hapa Kenya na wananchi wa kawaida asikudanganye mtu. Njoo ujionee ama uulize Watanzania wenzako walioishi Kenya watakuelezea. Sema Kiswahili chetu ni tofauti na chenu hio ni kweli lakini tunaelewana bado bila tatizo. Mtz akizungumza Mkenya anamuelewa na Mkenya akizungumza Mtz anamuelewa. Ni kama tofauti ya kizungu cha Marekani na UK. Wanaelewana ila kizungu chao kina tofauti fulani.
Kizungu ndiyo nini wewe nyangau aterere.
 
Mimi nimekubali na Kenya nimefika mara nyingi Sana. Jambo linalonishangaza ni kwamba viongozi wenu hawajitambui kabisa, hapa duniani nimepata bahati ya kutembelea nchi mbalimbali, sijawahi kuona Wala kusikia nchi yoyote ambayo shughuli za Kitaifa zinaendeshwa kwa kutumia lugha inayoeleweka na watu wachache na kuacha lugha ya taifa inayoeleweka kwa watu wengi

Kenya lugha ya Kiingereza inathaminiwa na kutukuzwa zaidi ya Kiswahili, 99% ya magazeti yenu yanaandikwa katika lugha ya Kiingereza, 90% ya vipindi vya TV stations ni Kiingereza.

Ni Sasa hivi tu, hasa baada ya Bongo flavor kukubalika na Magufuli kuingia madarakani na kuanza kukikuza Kiswahili duniani ndio wakenya wanaanza kukikubali, kabla ya hapo Kiswahili Kenya kilionekana ni lugha ya "second class citizens in Kenya"
Ni kweli.
 
Waganda ushamba umewazidi wale,wanauhusudu sana uzunguzungu kuliko uafrika wao

Sio ushamba maana wanaongea lugha zao za asili tena kwa ufasaha, Kiganda, Kinyankole...ni kwamba hawajakaa na kuona umuhimu wa Kiswahili kwenye mzunguko wa maisha yao. Labda tu kwa waliotoka na kwenda Kenya au Tanzania.
 
Kumbe mnajua heshima na umuhimu wa Kiswahili eh? Sasa mbona hadi leo mnaona dili sana mtu kujua Kiingereza tu na huwa mnawakejeli watanzania wasiojua Kiingereza je hao Waganda wanaojua sana Kiingereza wako wapi kimaendeleo?

Anyway hongereni na endeleeni kupambana kukisambaza huko nchi za Kaskazini sisi huku tunapambana kukisambaza kwenye nchi za Kusini maana Zambia nao wataanza kukifundisha mashuleni na kukitumia mitaani! Soon kitasambaa Africa nzima!

Hakuna Mkenya asiyejua umuhimu wa Kiswahili maana tunakitumia kila siku kwenye shughuli zetu, ni kwamba huwa hatujaganda kama mazuzu kwenye lugha moja, Kiswahili tunakitumia ndani kwa ndani, Kingereza kinatuunganisha na dunia hivyo hatukikwepi na tunakipenda pia maana ni dili aisei, tumekichangamkia, pia lugha lazima ujenge uzoefu wake ndio uimudu hivyo kingereza pia huwa tunakitumia baina yetu ila kwa baadhi sio kila Mkenya.
 
Ooh sawa mkuu, nikajua all Kenyans are fluent in english.
 
Hakuna nchi yenye raia wake wote 100% fluent kwa Kingereza, hata hao Waingereza wenyewe kuna wengi tu huchapia kwenye sarufi. Ufasaha wa lugha hususan kiuandishi kunahitaji elimu ya lugha yenyewe tena hadi chuo.

Hata hapo Bongo kwa wengi mlioishia la saba au hata kidato cha nne, hata baadhi ya wahitimu wa vyuo uandishi wenu wa Kisawhili huwa balaa. Sasa mtihani unakua pale Kingereza chenyewe kilishakupiga chenga, lugha yako ya asili kama vile Kisukuma haukijui ipasavyo na unawaita wanaokiongea kuwa washamba, halafu wewe mwenyewe Kiswahili ambacho umeganda nacho, hauko vizuri kihivyo kwamba ukiagizwa uandike report au taarifa kamili kwa Kiswahili utachapia balaa.
 
Taratibu Kiswahili kinaanza kuheshimika Kenya, hongera Sana wanamuziki wa Bongo Flavor, RIP. Magufuli.
 
Nyie mna amani. Viongozi wenu ni wazuri. Zunguka katika nchi zingine za Afrika ndio utafahamu maana ya neno "viongozi wabaya"
Nimeishi na Warthiopia, Eritreans, Somalians, South Sudan and noth Sudan. Tulielewana.
 
Mnaenda kubaka nchi yenye 4B GDP
Screenshot_20211111-213626.png
 
Amani haiwezi kuwepo kusipo kuwepo viongozi wenye utashi,, kama huku Tanzania hakuna kiongozi mwenye utashi,, wote wachumia matumbo yao,, bora akuae abaki madarakani,,
Kwahiyo Tz ni nchi isiyokuwa na amani??..maana umesema hakuna viongozi wenye utashi

Haupo serious kabisa na inaonyesha hujui amani ni nini.
 
By the way ile taaluma yenu pendwa ya uganga mumeileta mpaka huku, nimeona mabango yenu kila sehemu, japo kuna siku mlikamatwa sana maana serikali huku haivumilii ushirikina.
Ushirikina ni nini!?
Define ushirikina
 
Back
Top Bottom