Hongera Wakenya, wana EAC na dunia kwa tulioshiriki Standard marathon leo

Hongera Wakenya, wana EAC na dunia kwa tulioshiriki Standard marathon leo

MK254

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2013
Posts
32,408
Reaction score
50,809
Hii ndio ilikua mara yangu ya kwanza kushiriki mbio hizi ambazo huwahusisha watu wa matabaka yote na hutenganishwa kulingana na umbali, kuna wanaokimbia 42km, wengine 21.1km na hata kunao wa 10km na pia kilomita 2km za wakurungezi na viongozi.

Sikujua huwa raha hivi, kwanza aina za muziki, aisei ngoma zilizorindima wakati tunaanza full mzuka mamaee. Nashauri waandalizi wawe wanaweka hizo speakers baada ya kila kilomita mbili yaani inakuwa mwendo wa mdundo hadi mwisho.

NItajitahidi niwe nashiriki zote hata zile hufanyika Kilimanjaro, Dar na Zanzibar.
Hongera sana kwa walioshiriki, Wakenya na wana Afrika Mashariki, na dunia, maana kuna watu wametokea Ulaya kuja kushiriki tu na kugeuza, halafu special big up kama kunao JF members ambao waliokuwepo.

Na hatimaye hongera ziwaendee mijitu ya wanariadha ambao walimaliza ndani ya muda mfupi, yaani wakati sisi wengine miili bado haijazoea tupo kwenye kilomita tano, mijitu inachana mbuga kwenye kilomita 30, hao watu sijui kama wameoa au kuolewa na huwa vipi kwenye mechi zao za vitandani, haswa jamii ya Wakale...hehehehe

Washindi hawa hapa
Elisha Kiprop - 42km - 2:17
Josephine Chepkoech - 42km - 2:35

Mathew Kiprotich - 21km - 1:04:57
Valerie Aiyabei - 21 km

Walioshiriki walizidi 18,000 kwa idadi

Haya hapa matokeo yangu kwa kutumia Strava app

3.jpg

2.jpg
 
Hongera jombaa, huwa ni raha sio siri. Nilishiriki kwenye Ndakaini Marathon mwaka jana, half marathon pia ila naona ni kama nilikufunika sawa sawa kwenye muda nilioutumia. 😎 Mwezi huu, wiki mbili zilizopita tulioshiriki nao walinialika tena ila bahati yangu sikuwa karibu. [emoji1] Huu mwaka sijafanya mazoezi ya kutosha.
 
Hehehe ulipiga ngapi, lakini kukamilisha 22.4km kwa 2:39 kwa siku ya kwanza ever sidhani kama ni mbaya sana. Have never participated in any other half marathon before, labda kitambo sana nikiwa shuleni.
 
Hehehe ulipiga ngapi.
Sasa umeanza ujasusi eeh? 😡 Hapo kwenye muda wako punguza dagíka ícío, ícío, múgwaja, na usiambie mtu. 😀 Nadhani hiyo altitude ya Ndakaini ndio iliniaffect, ningechomoka na pesa taslimu jombaa, hao jamaa ni makirimino. [emoji38] Anyway ilikuwa for fun tu na huo muda wako ni impressive pia. Mara ya kwanza nilipokimbia 2016 niliishia charge at 18kms. Umenikumbusha, usiku huo mwaka jana nilishikwa na 'muscle pull' kila sehemu ya mwili hadi tumboni. Walikuwa wanadhani nina'go', yaani ninawaacha.
 
Hehehe!! múgwaja (saba) ndio unasema ulinifunika mbaya, hiyo ni kitu nikijua uko mbele yangu heri nipoteze fahamu nikikufukuzia, ila kweli altitude hukwamisha pia...hehehehe eti ulikua una 'Go', tatizo utakua ulikurupuka bila kujiandaa kwanza, haya mambo hutaka maandalizi, mimi kwa mwezi huu nimekua nakatiza Thika road nikijiandaa kwa hafla ya leo, hivyo sasa hivi niko poa hata naweza kutoka out nikacheze densi usiku wa leo, hamna chochote ninachohisi.
 
Nilikuwa nimejiandaa vya kutosha siunaona nilivokufunika kwenye muda? [emoji1] Shida ni kwamba baada ya mbio nilijitosa kwenye cycling ya kijinga Ndakaini, ni kuzuri sana huko. Najua sasa hivi unavojihisi kama Superman. Ntajaribu tena mwaka ujao, Inshaalah. Hongera tena jombaa, naona system zako bado zipo on point.
 
Wewe kichaa, yaani baada ya marathon unakwenda cycling...hehehe ndio maana kila kitu kilikugomea hadi kucha. Mimi nimecheza zile densi za uwanjani baada ya mbio, aisei nikahisi ovyo na kuondoka.
Haya tukutane next Ndakaini au yoyote ile itakayoibuka, nitazisaka na kuzifuata zote hadi Dar na Zanzibar.
 
Alafu hapo juu kwenye taarifa nadhani kuna typo kwenye mshindi wa Half Marathon, nilipoona hizo kilomita na huo muda wa lisaa limoja na dakika nne nilidhani Eliud Kipchoge ameangukia pua. Alafu ntaanza mikakati ya kujiandaa kwa Ndakaini mapema, mungu akipenda mwaka ujao tutajua nani ndiye jogoo. Nasikia Lewa Marathon ndio raha kuliko zote ila mpango wangu huwa ni one per year hizo zingine naachia wataalamu kama wewe. Hahaa! [emoji1]
 
Alafu hapo juu kwenye taarifa nadhani kuna typo kwenye mshindi wa Half Marathon, nilipoona hizo kilomita na huo muda wa lisaa limoja na dakika nne nilidhani Eliud Kipchoge ameangukia pua. Alafu ntaanza mikakati ya kujiandaa kwa Ndakaini mapema, mungu akipenda mwaka ujao tutajua nani ndiye jogoo.

Hayo matokeo niliyatoa kwenye hii link {PHOTOS} Elisha Kiprop, Josephine Chepkoech rule 2018 Standard Chartered marathon
Maana hao binadamu walitutangulia na kumaliza kitambo wakati sisi misuli bado hata haijaanza kushika kasi.
 
Nakuambia mbio zina wenyewe. Huyo Mathew Kiprotich nadhani alishinda kwenye 21km na sio 42 haiwezekani ikawa eti alikamilisha 42km kwa muda wa 1:04:57.

Ooops!! Noted and rectified, that kweli was a typo...
 
Ooops!! Noted and rectified, that kweli was a typo...
Tatizo mwongo mwongo sana we jamaa, hata hizo mbio usikute jamaa yako ndiyo alishiriki ume amua kuvaa uhusika wake [emoji23]
 
Tatizo mwongo mwongo sana we jamaa, hata hizo mbio usikute jamaa yako ndiyo alishiriki ume amua kuvaa uhusika wake [emoji23]

Haya bro, tunakuja Kili marathon mwakani, tatizo Wakenya hunyakua ushindi kuanzia namba moja hadi kumi, tena kwenye nchi yenu, Waswahili hamkimbii.
 
Back
Top Bottom