Nimekita kambi maeneo ya mwambao wa ziwa manyara kama sehemu ya ziara ya kuijua tabia asilia ya Masai, wambulu, Wamang'ati na wengineo!
Huku napata kujua misingi na tabia ya asilia kutoka kwa mababu zao ni ipi!
WAMBULU
Mzee mmoja wa kimbulu ananidokeza kwamba, Kwao mwanamke ambaye Ujauzito uliharibika bahati mbaya! Hakustahili kabisa kuishi na kaya yake (familia)!
Wala hakutakiwa kugusa ama kuchangia vyombo na watu wengine katika kaya!
Alijengewa kibanda cha msonge pembeni kabisa mwa shamba, huduma kama maji alipelekewa huko huko, na chakula alijipikia huko huko, hakutakiwa kabisa kuonana wala kugusana na mwanafamilia yoyote hadi mkosi ule utakapo mtoka!
NAMNA YA KUTOA MKOSI
Njia kubwa wazee hawa waliyoitumia kumtoa mkosi; ilikuwa nikutumia makabila mengine ya wageni, hususani wanyatulu waliokuwa wakijishughulisha na kilimo maeneo hayo, ndiyo waliotumika kutoa mkosi huo!
Wanyatulu walipewa kazi ya kumhudumia na kumpelekea chakula shabani mwanamke aliyetengwa kwa ahadi ya kulipwa ng'ombe!
Katika harakati za kupeleka msosi: Siku nyingine waliombwa kulala kule kwa kisingizio cha kumpa ulinzi!
mnyatulu aliyefanikiwa kumtia mimba mwanamke hadi kujifungua alihesabika kautoa mkosi kwenye familia ile, hivyo alilipwa ng'ombe wawili au watatu;
Pia mwanamke aliporudishwa kujichanganya na familia yake, ilichinjwa mbuzi kama ishara ya kuaga mkosi alioubeba mnyatulu;
Mtoto aliyezaliwa hakuwahi kuhesabika kuwa ni wa mnyatulu hapana, Alihesabika ni zao la familia ya Kimbulu na aliitwa kwa jina babake wa awali wa kimbulu!
Ukiachana hilo; Mwanaume aliyeacha familia nyumbani kwao akasafili mikoa ya mbali katika harakati za kutafta, mathalani aliacha mke ana mtoto mmoja, mwanamke wake endapo angezaa mtoto na mwanaume mwingine haikuwa ajabu kwao, walihesabu ni zao la familia na taarifa na pongezi zilitumwa kwa Mme halisi kuwa " Hongera umepata mtoto mwingine wa pili, au wa tatu n.k) hadi pale Mme atakaporudi, na haikuwa ajabu kwao kwasabu waliamini kinachopatikana ni Mali ya mme! Na waume hawakuona kama hilo lina shida ( ni kama ilivyo ng'ombe wa jilani akipanda ng'ombe katika zizi la jilani, ndama akizaliwa ni Mali ya mwenye jike)
KUWEKA MKUKI NA FIMBO MLANGONI
Makabila haya yanaenda mbali zaidi, walikuwa na ujilani mwema, inamaana Mzee aliruhusiwa kula mkeMwana( mke wa mtoto). Ilikuwa ukitoka marishoni ukikuta Fimbo au mkuki mlangoni! Ilikuwa ni ishara huko ndani mzee anashughulika, hivyo ni lazima usubiri kwanza hadi mzee amalize!
Vile vile walikuwa na utaratibu, chakula cha mzee kiliandaliwa special!
Kama ni nyama wazee walibanikiwa yao special na wake zao, wake walihakikisha Mme anakula anashiba haswa!
Hata maziwa au mboga ikiadimika, lakini ya mzee ilihifadhiwa kwenye kibuyu maalumu!
Na endapo mzee anapenda mbegu ya kijana mchapakazi iingie kwenye familia yake, alimkabidhi mikoba, na mke alimkarimu kijana kwa vyote, hasa zile tarehe za Mimba, mzee aliweza kuaga kwenda safari ilikumpa kijana kupanda mbegu!
Hata siku ya mzee kurudi, hakutakiwa kufika nyumbani moja kwa moja! Alitakiwa kuisha kwenye klabu ya pombe na kutuma mtu yoyote apeleke taarifa kuwa mzee karudi! Hakutakiwa kabisa kufumania ( kwao kufumania ilikuwa haipo)
WAMASAI!
Leo Niko na mzee Lioshon Molani wa zaman wa kimasai!
Ananieleza wamasai zamani hawakuwa wanazika kwa kuchimba kaburi!
Wao walikuwa na utaratibu wao wa kuzika!
Kwanza kabisa ilikuwa ni mkosi kwao kuona mtu anapokata roho, hivyo mgonjwa aliyezidiwa walimtenga, kwa kumjengea kibanda shambani mbali kabisa, walimuacha huko na kumuwekea chakula cha kutosha!
Walifanya kumtembelea kuchungulia kama kafariki kwa kuangalia inzi kwenye tundu maaalum kama kiashilia, pia walitazama ndege hususan kunguru kama dalili ya kitu kuoza!
Baada ya kuona hivyo walijengea boma nyumba ile na kuhama kabisa eneo lile!
NITAENDELEA KUJAZIA NYAMA JUU YA WAMASAI NA WENGINE! ili Uzi usiwe mrefu sana!