Hongera wanafunzi mipango - mmeonyesha dira ya taifa

Hongera wanafunzi mipango - mmeonyesha dira ya taifa

kweleakwelea

JF-Expert Member
Joined
Nov 29, 2010
Posts
3,072
Reaction score
1,545
kwa wale wanaopita pita mjini dodoma leo ni masimulizi ya jinsi FEDHA na UBABE wa siasa umeshindwa kufanya kazi katika jamii ya wasomi......

pamoja na matumizi makubwa ya rasilimali yaliyotumika na CCM na mfumo wake, kuchakachua kazi ya tume ya uchaguzi, na kumpigia kampeni nzito ya aina yake mgombea wake Bwana Kwagilo na mgombea mwenza wake ambaye ni mke wa Mheshimiwa Juma Nkamia ameambulia kuwa wa mwisho kati ya wagombea watatu waliokuwa wakigombea uraisi wa serekali ya wanafunzi chuo cha mipango....WAMEANGUKIA PUA PWAAAAAAAAAAAA!!!!!

kampeni zilizodhaminiwa na CCM zilikuwa nzito kiasi kwamba TAKUKURU walijikuta wakiingilia kati na kubaini kuwa kuponi za chakula zilikuwa zinagawiwa bure na wapambe wa mgombea waliokuwa wakiranda randa huku na kule wakiwa wametinga PIERRE CARDINI mpya kabisa katika migahawa iliyo maeneo ya miyuji...watumishi wa idara hii walienda mbali na kumhoji mgombea huyo baada ya kubaini tuhuma hizo,,,,hadi tunaenda mitamboni hatujapata kujua kilichoendelea bali tu mgombea huyo KUBWAGWA VIBAYA NA KUWA WA MWISHO KATI YA WAGOMBEA WATATU....

huu ulikuwa ni mtihani wa aina yake kwa wasomi hawa ambao ni taswira katika jamii....swali walilokabiliwa nalo ni JE MATUMIZI MAKUBWA YA PESA, UCHAKACHUAJI NA MATUMIZI MABAYA YA MADARAKA YANA NAFASI KATIKA FIKRA ZA WASOMI NA HATIMAYE WATANZANIA?

baada ya kuona matumizi makubwa ya pesa, na vitisho, na misafara, wanafunzi haya waliamua kwa makusudi kabisa kumsupport mgombea asiye na makuu, na ambaye hakuwa na tambo zozote za kisystem...ambaye pia mtazamo wake ni waKILIBERALI na kuexercise nguvu ya umma kuwajambisha bwana kwagilo na mama nkamia....

my take;

1. CCM lazima itambue wazi kuwa kizazi cha sasa hakitishiwi nyau...mapiki piki wala toli toli...inapaswa sasa kufanyia kazi kwa uadilifu kero za wananchi ili kuiwezesha nchi yetu isonge mbele......

2. Wasomi wameonyesha dira, umma unafuata nyuma yao with full support......hongera sana wasomi

3. Vyama vya siasa kusupport CHAGUZIi za vyuoni ni uhuni na unapaswa ukemewe VIKALI

4. ni wakati sheria za uchaguzi kuanza kufuatilia chaguzi za vyuoni ie gharama za uchaguzi

5. narudia tena HONGERA SANA WASOMI WETU....sasa ninyi ni WASOMI KWELI KWELI!

Mungu ibariki Afrika,

Mungu ibariki Tanzania!
 
Siasa sasa moaka kwenye vyuo, hii inadhiirisha kabisa ni jinsi gani ilivyotamu siasa, ukiingia huko unakula bila jasho, ngoja namimi nitafute PIERE CARDINI za kutosha ili nikirudi home nikawachanganye kule kijijini kwetu.

Pia napenda kuchukua fursaa hii kutoa "TAMKO" kuwa wasomi wa MIPANGO DOM mmeonyesha ujasiri mkubwa na kuonyesha ni jinsi gani siasa za Chama cha Magamba kuwa sasa hazikubaliki juu ya jamii ya wasomi, Congs sana!

mwisho kabisa tuungane kuitetea nchi yetu.
 
hayo ni maamuzi sahihi,kwani huwezi kumlazimisha punda kunywa maji,

wasomi sasa wamchoka kuwa ni vichaka wa mafisadi kujificha huo ni mwanzo mzuri na Democrasia imechukuwa mkondo wake
tunaomba wakuu wa chuo cha mipango msianze harakati za kulazimishwa kupinga matokeo hayo mahakamani kama ilivyo tokea mwaka 2010 pale chuo cha waislamu morogoro na chuo cha kilimo sua baada ya wagombea wa upande wa pili kushindwa

haki imetendeka,na iendelee kuheshiwa

pamoja daima,kwa pamoja tutashinda
 
guud the same was done UDOM,CBE-DOM AND IFM BRAVO,maana siasa chuoni wanataka kuifanya ni kwa ajili ya watu wanaoweza kukodi mziki na matarumbeta huu utamaduni unabidi uondolewe kwa kuwamwaga tu wale ambao wanafadhiliwa na watu wenye pesa za wizi..big up mipango............
 
taarifa zilizonifikia hivi punde ni kuwa mgombea wa chama cgha magamba anataka kukata rufaa..

lakini hata hivyo, taarifa zinasema kuwa bado TAKUKURU wana faili lake mezani....

hivyo haijaeleweka kuwa ana uhalali gani wa kukata rufaa....
 
aKSANTE KWA TAARIFA!
CCM hawawezi kitu bila kupitisha ndururu!
 
Haa jamani mnazidi kuwavunja moyo jamaa zetu..... na tangu juzi nilimuona Nape Dodoma et kaalikwa kwenye sherehe ya wana Udom pale kiliman kumbe ana dili jingne pale mipango.
 
Back
Top Bottom