Hongera wanamsimbazi kwa mabadiliko

Hongera wanamsimbazi kwa mabadiliko

Betterhalf

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2016
Posts
2,882
Reaction score
2,560
Habari za jioni wadau.
Naipenda Simba SC na kwa yaliyojiri wiki hii, nitaendelea kuipenda zaidi na zaidi.

Kwa wafuatiliaji wa michezo, hususan soka, hakuna asiyejua ukongwe wa klabu ya Simba.
Iliasisiwa 1936 wakati huo ikiitwa Sunderland.
Hii inaifanya iwe na umri wa miaka 81.Kwa kipindi chote hicho, imeweza kufanya mengi mazuri ingawa haijafikia mafanikio kama ya TP Mazembe,Al Ahly, Esperance, Enyimba,Asante Kotoko na nyinginezo za mfano huo.

Lakini, ninaona nuru mpya kupitia hatua ya maamuzi ya kubadilisha mfumo wa uendeshaji kutoka ule uliozoeleka kwenda mfumo wa hisa.
Sina utaalam sana,lakini naamini timu itakuwa kibiashara zaidi na hivyo kujiuza zaidi kwenye masoko ya ndani na nje ya hisa.

Hali hii, itasababisha timu kujiendesha kwa faida,kulipa wachezaji na waajiriwa wengine kwa wakati, uhakika na haraka pasipo na ubabaishaji.

Rai yangu kwa wana Simba wote, kama tulivyoridhia muundo mpya,pia tuyapokee mabadiliko kwa kushiriki kuyasema mazuri ya mfumo mpya huku tukiyafanyia kazi mapungufu kwa njia sahihi badala ya vurugu.

Pia, naamini muundo mpya lazima utaziba mirija ya ujanja ujanja ambayo iliwanufaisha baadhi huku timu ikipoteza mwelekeo; kwa hali hiyo tujitahidi kutafuta njia nyingine za kujikimu badala ya kuiandama klabu na viongozi au watendaji watakaobeba dhamana ya kutuvusha.

Nitumie fursa hii kuwapongeza wanachama,mashabiki,wapenzi,viongozi,TFF,BMT, Wizara na serikali kwa ujumla kwa kubariki mabadiliko haya chanya kwa maendeleo ya michezo Tanzania, Afrika mashariki na Afrika kwa ujumla.

Nitumie makala hii pia,kuziomba timu nyingine ziige haya ili kuwatendea haki wanamichezo wanaziunga mkono timu zetu.

Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Simba SC.
Wakatabahu,
Nawasilisha.

The Great Gatsby
 
Hata mimi nawapongeza sana hatutaki klabu Yetu iongezwe na wahuni tunataka kila mwenye hisa Simba ni yake na hii itasaidia kuwadhibiti wahuni wachache wanaotaka kufaidi ndani ya simba

Sent using Jamii Forums mobile app
Polite response:
Kwa mfumo uliopo Simba ni mfumo wa Kampuni na siyo Klabu tena. Itasajiliwa chini ya Sheria ya Makampuni (Sura 212 ya Sheria za Tanzania). Tafadhali fahamu kuwa Majority Shareholder (51%) (MO) ndiye mwenye sauti katika kampuni. Shareholders wengine wanaotimiza 49% kwa hisa kidogo kidogo ni kama Kenge tu katika msafara wa Mamba! (Wenye mapovu karibuni sana lakini mapovu yenu hayataondoa ukweli).

Niwapongeze sana watani zetu kwa uthubutu huu.

Yanga tulijaribu kuingia katika mfumo wa Kampuni miaka mingi iliyopita, kwa ujima wa kipindi kile wa aina ya akina Mzee Kilomoni hata sasa, tulijikuta tukizalisha makundi makuu mawili viz. Yanga Kampuni na Yanga Asili, kwa kipindi cha takribani miaka 10 hivi tulipata wakati mgumu sana kuwafunga Simba maana makundi hayo yalikuwa yanahujumiana kwa maslahi binafsi.

Naamini mfumo uliopo Simba sasa utaamsha ari mpya kwa upande wa timu ya Wananchi kuboresha zaidi mfumo huo kwa kuepuka mtu mmoja kuwa majority shareholder.
 
Hakuna povu kwa mwenye uelewa na mpenda maendeleo.Hata Yanga walipoasisi kampuni, binafsi niliwaunga mkono.
No matter MO atakuwa na sauti, lakini uhalisia uko pale pale kwamba timu itasimama imara kiuchumi na hivyo kuyafikia malengo ambayo muda mrefu hayakuwezekana.
Wazee wetu akina Kilomoni na wengine, wataelewa taratibu kadri muda unavyoenda.

The Great Gatsby
 
Back
Top Bottom