Hongera waziri Bashe, hongera Serikali. Lakini ongezeni haya kwa ufanisi zaidi

Hongera waziri Bashe, hongera Serikali. Lakini ongezeni haya kwa ufanisi zaidi

Justine Marack

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2014
Posts
612
Reaction score
1,698
Serikali imesikia kilio cha watanzania. Ilifikia WAKENYA na Wanyarwanda wanakuja Tanzania na kuingiza Mashambani kulangua mazao, mpaka kulangua mazao mabichi yakiwa shambani.

Nimeshuhudia Mnyarwanda anafanya biashara ya kukopesha pesa kwa mkulima ili aje amlipe mazao. Anachofanya ni anakuja mwezi January au February na kukopesha pesa kiasi Cha Tsh 15,000 kwa malipo ya gunia la Mahindi au maharage au karanga. Ifikapo mavuno anakuja kukusanya malipo na kujaza magari kwa gharama ya chini Kisha anatimka nayo.

Pale Rwanda ukienda kupeleka biashara yoyote kama Mtanzania au mgeni yoyote basi utatakiwa kuwa na kampuni na TIN number ya Rwanda. Vinginevyo itakubidi kuukabidhi mzigo wako kwa mtu mwenye kampuni ambaya ni Mnyarwanda na hautajihusisha kwa lolote mpaka mzigo kuuzwa.

Sasa nashauri yafuatayo.
1. Katazo liende mbali zaidi mpaka kwenye unga. Kuna mtindo anakuja mgeni ananunua Mahindi Kisha anakwenda kusaga unga ambao atafanya export kama unga na sio Mahindi.

2. Kuna watanzania ambao watasajili Kampuni lakini watabaki kuwa vibaraka wa wageni kwa kuendeleza utaratibu ule ule. Yaani Mtanzania ataonekana kwenye karatasi lakini ulanguzi huko Mashambani wanafanya WAKENYA au Wanyarwanda. Sasa kuwekwe vigezo vikali ili kuzuia udanganyifu.

Hongera sana
 
Back
Top Bottom