Leonel Ateba Mbinda
JF-Expert Member
- Feb 20, 2023
- 644
- 2,695
Naishukuru sana serikali kwa kuchukua hatua dhidi ya mmiliki wa jengo, naomba kuisaidia Jeshi la Polisi kuendelea kusaka taarifa zaidi za tukio hilo lakini kinachosemwa pale kariakoo na watu mbalimbali kisipuuzwe.
Mimi nimesikia watu wakisema kuwa mmiliki wa jengo hilo alifanya tamaa, kwamba alipoona gorofa limejaa wateja na hakuna pa kupangisha alianza mipango ya kujenga stoo nyingine za kuhifadhia mizigo underground, kwahiyo wakati wanachimba chini ili kujenga jengo lingine underground mafundi wakawa wanachimba hadi kwenye nguzo, hivyo nguzo zilishake kutokana na uchimbaji usiokuwa na maarifa, madhara yake ndio haya tunayoyaona leo.
Kazi kubwa imefanywa na serikali kuokoa maisha ya watu lakini uzembe wa aina hii usivumiliwe, tuendelee kuokoa maisha ya watu, hawa wajinga wajinga wengine wanaoleta siasa katika maisha ya watu tuwaache waendelee na ujinga wao.
Nakupongeza sana RC Chalamila. Waziri Lukuvi kwa kazi kubwa mnayoendelea kuifanya, hii sio siasa hapa kama Taifa tumepata msiba mkubwa, uchunguzi uendelee kufanyika na taarifa za wadau mbalimbali ziendelee kufanyiwa kazi, vyombo vyetu vya usalama naviamini viko kazini na damu za waliopoteza maisha hazitoenda hivi hivi.
Yote kwa Yote namshukuru Rais wetu Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa maelekezo ya kiserikali ili kutoa faraja kwa wananchi wote waliopoteza ndugu zao.
Mwisho, kesho ni Do or Die uwanja wa TAIFA, LAZIMA TWENDE MOROCCO.