Hongera Yanga, hongera Tanzania

Itovanilo

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2018
Posts
2,314
Reaction score
5,150


Mpira wa Tanzania umekua hili halina shaka, nadiriki kusema Tanzania ndiyo nchi inayoongoza kuwa na wapenzi na mashabiki wengi wa mpira afrika mashariki na Kati.

Kitu ambacho kilitushinda sisi na vilabu vyetu ni uwekezaji wa mpira, yaani mguuni hatukuwa na mpira lakini leo hii kirahisi na bila wasiwasi Yanga anatinga fainali ya CAF Confederation Cup, ni hatua kubwa kwa Yanga na Tanzania kujumla.

Timu ya Simba siyo mbovu kama wengi wanavyodhani, bali ni ubora wa Yanga kwa msimu huu. Timu za kaskazini zile maarufu hazijashuka kiwango kama wengi wanavyodai hapana. Bali ni ukuaji wetu wa mpira.

Ni Yanga ambayo ilikuwa na ma strike kama, Sibomana, Balinya, Sarpong, Molinga, na wengineo ambao wasingeweza kuifanya Yanga ikang'ara kimataifa; lakini leo hii ukiondoa Musonda, na viungo kama Aziz Ki, Mudathir na wengineo, Yanga ina Fiston Mayele mtu ambaye analijua lango mpaka anajua tena.

Hongera GSM, hongera Hersi Said.

Alamsiki.
 
Tunahitaji full house kwa Mkapa, hiyo ndio mechi ya kumalizana na Waarabu.

Ukiweza kumuua Mwarabu kwa margin ya goli 3 kwa 0 hilo kombe Yanga wananyanyua kwapa.

Goli tatu za nini,hawa waarabu niwakaida hata 0-0 kwa mkapa bado wanapigika tu kwao..utabiri wangu wanakufa nje ndani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…