Itovanilo
JF-Expert Member
- Jul 30, 2018
- 2,314
- 5,150
Mpira wa Tanzania umekua hili halina shaka, nadiriki kusema Tanzania ndiyo nchi inayoongoza kuwa na wapenzi na mashabiki wengi wa mpira afrika mashariki na Kati.
Kitu ambacho kilitushinda sisi na vilabu vyetu ni uwekezaji wa mpira, yaani mguuni hatukuwa na mpira lakini leo hii kirahisi na bila wasiwasi Yanga anatinga fainali ya CAF Confederation Cup, ni hatua kubwa kwa Yanga na Tanzania kujumla.
Timu ya Simba siyo mbovu kama wengi wanavyodhani, bali ni ubora wa Yanga kwa msimu huu. Timu za kaskazini zile maarufu hazijashuka kiwango kama wengi wanavyodai hapana. Bali ni ukuaji wetu wa mpira.
Ni Yanga ambayo ilikuwa na ma strike kama, Sibomana, Balinya, Sarpong, Molinga, na wengineo ambao wasingeweza kuifanya Yanga ikang'ara kimataifa; lakini leo hii ukiondoa Musonda, na viungo kama Aziz Ki, Mudathir na wengineo, Yanga ina Fiston Mayele mtu ambaye analijua lango mpaka anajua tena.
Hongera GSM, hongera Hersi Said.
Alamsiki.