Hongera Yanga SC kwa kutinga makundi Shirikisho

denooJ

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2020
Posts
18,509
Reaction score
68,228
Salaam.!

Nisiwe mchoyo wa pongezi, nawapongeza Yanga SC kwa ushindi wao walioupata jana wa goli 0-1 dhidi ya waarabu wa Club Africain ya Tunisia uliowawezesha kuingia hatua ya makundi ya kombe la shirikisho.

Pongezi zangu zinachagizwa zaidi na historia waliyokuwa nayo Yanga SC kushindwa kuingia hatua ya makundi ya makombe ya CAF toka mwaka 1998, kuuvunja mwiko huu ni hatua kubwa kwao.

Pia, nafurahi zaidi kwa sababu naamini, kama Yanga SC ingetolewa jana , maana yake ingechukua ubingwa wa ligi kuu ya NBC kwa mara ya pili mfululizo tena kwa urahisi zaidi, kwasababu;

- Wasingekuwa na mashindano ya kimataifa ya kuwasumbua hivyo wachezaji wao wangeepuka uchovu, na majeruhi, na kuwafanya waelekeze nguvu zao zote kwenye ligi ya ndani.

- Mwenendo wa Simba SC kwenye mechi za ligi yetu ya ndani, matokeo yao kwa sasa sio ya kuridhisha.

- Ukubwa/upana wa kikosi cha Yanga SC, kocha wao angekuwa na uwanja mpana wa kuchagua wachezaji wa kuanza kila mechi ya ligi.

Lakini kutokana na wao kutinga hatua ya makundi, maana yake Nabi atalazimika kuwachezesha wachezaji wake wazuri kwenye kombe la shirikisho, na wakati huo huo awachezeshe kwenye ligi kuu ya NBC akiogopa kutowapanga halafu aje kuumbuliwa na timu pinzani za ligi yetu ya ndani.

Nieleweke vizuri, sisemi Yanga SC hawezi kuwa bingwa wa ligi ya ndani, lakini naamini kushiriki kwao kimataifa kutawapunguzia kasi ya ufanisi kwa ligi yetu kwa namna moja au nyingine, hivyo nawatakia wanachi safari njema mfike nusu fainali ya kombe la shirikisho, kwani kutolewa chini ya hapo mtakuwa mmeliangusha taifa.
 
Kati ya timu 16 zilizoingia Makundi Ni timu 6 tuu ndio za Waarabu..

Hapa Yanga Ina nafasi ya kufika robo fainali wakichanga karata vizuri..

Omba kwenye kundi lao wasipangiwe pyramid,far Rabat,USM Algers,Rivers United na Mazembe,waliosalia wanfungika.
 
Kati ya timu 16 zikizoingia Makundi Ni timu 6 tuu ndio za Waarabu..

Hapa Yanga Ina nafasi ya kufika robo fainali wakichanga karata vizuri..

Omba kwenye kundi lao wasipangiwe pyramid,far Rabat,Al Akhdar na Mazembe,waliosalia wanfungika.
Hata wakipangwa na hao wakamaliza nafasi ya pili, nawaona bado wana nafasi ya kufika mbali.

Ule ushindi walioupata jana umewapa mzuka sana, wakienda nao kwenye makundi watacheza kwa kujiamini, na inawezekana kabisa kuanzia hapo, ndio wataanza kutumia faida ya uwanja wa nyumbani kupata matokeo mazuri.
 
Salaam.!

Nisiwe mchoyo wa pongezi, nawapongeza Yanga SC kwa ushindi wao walioupata jana wa goli 0-1 dhidi ya waarabu wa Club Africain ya Tunisia uliowawezesha kuingia hatua ya makundi ya kombe la shirikisho.

Pongezi zangu zinachagizwa zaidi na historia waliyokuwa nayo Yanga SC kushindwa kuingia hatua ya makundi ya makombe ya CAF toka mwaka 1998, kuuvunja mwiko huu ni hatua kubwa kwao.

Pia, nafurahi zaidi kwa sababu naamini, kama Yanga SC ingetolewa jana , maana yake ingechukua ubingwa wa ligi kuu ya NBC kwa mara ya pili mfululizo tena kwa urahisi zaidi, kwasababu;

- Wasingekuwa na mashindano ya kimataifa ya kuwasumbua hivyo wachezaji wao wangeepuka uchovu, na majeruhi, na kuwafanya waelekeze nguvu zao zote kwenye ligi ya ndani.

- Mwenendo wa Simba SC kwenye mechi za ligi yetu ya ndani, matokeo yao kwa sasa sio ya kuridhisha.

- Ukubwa/upana wa kikosi cha Yanga SC, kocha wao angekuwa na uwanja mpana wa kuchagua wachezaji wa kuanza kila mechi ya ligi.

Lakini kutokana na wao kutinga hatua ya makundi, maana yake Nabi atalazimika kuwachezesha wachezaji wake wazuri kwenye kombe la shirikisho, na wakati huo huo awachezeshe kwenye ligi kuu ya NBC akiogopa kutowapanga halafu aje kuumbuliwa na timu pinzani za ligi yetu ya ndani.

Nieleweke vizuri, sisemi Yanga SC hawezi kuwa bingwa wa ligi ya ndani, lakini naamini kushiriki kwao kimataifa kutawapunguzia kasi ya ufanisi kwa ligi yetu kwa namna moja au nyingine, hivyo nawatakia wanachi safari njema mfike nusu fainali ya kombe la shirikisho, kwani kutolewa chini ya hapo mtakuwa mmeliangusha taifa.
Sema hivii wachukue kombe la shirikisho😄,Bora Kama umeuona mziki wao nakuukubali Sasa jua tunachukua nje na ndani🤸🤸
 
Hata wakipangwa na hao wakamaliza nafasi ya pili, nawaona bado wana nafasi ya kufika mbali.

Ule ushindi walioupata jana umewapa mzuka sana, wakienda nao kwenye makundi watacheza kwa kujiamini, na inawezekana kabisa kuanzia hapo, ndio wataanza kutumia faida ya uwanja wa nyumbani kupata matokeo mazuri.
Ila wasifanye mzaha na mechi za nyumbani maana Makundi Ni Ligi.
 
Sema hivii wachukue kombe la shirikisho[emoji1],Bora Kama umeuona mziki wao nakuukubali Sasa jua tunachukua nje na ndani[emoji1732][emoji1732]
Ndani hapana, Simba hawezi kukubali kuburuzwa miaka miwili mfululizo kirahisi, nendeni huko mkachoshwe kwanza.
 
Alishafeli Hadi Sasa Kama anakubali kupigwa na kina Ihefu, na Ruvu Vipi akikutana na Mwananchi[emoji125][emoji125]
Huyo mwananchi mbona last time aliponea chupuchupu.
 
Sisi tukisema uitabidi msubiri miaka 7 mfululizo,na Sasa tumeamua kukwea kimataifa rasmi[emoji1][emoji1]
Sio mbaya, kimataifa ila mmeanzia kule mliposema ni kwa walioshindwa.
 
Salaam.!

Nisiwe mchoyo wa pongezi, nawapongeza Yanga SC kwa ushindi wao walioupata jana wa goli 0-1 dhidi ya waarabu wa Club Africain ya Tunisia uliowawezesha kuingia hatua ya makundi ya kombe la shirikisho.

Pongezi zangu zinachagizwa zaidi na historia waliyokuwa nayo Yanga SC kushindwa kuingia hatua ya makundi ya makombe ya CAF toka mwaka 1998, kuuvunja mwiko huu ni hatua kubwa kwao.

Pia, nafurahi zaidi kwa sababu naamini, kama Yanga SC ingetolewa jana , maana yake ingechukua ubingwa wa ligi kuu ya NBC kwa mara ya pili mfululizo tena kwa urahisi zaidi, kwasababu;

- Wasingekuwa na mashindano ya kimataifa ya kuwasumbua hivyo wachezaji wao wangeepuka uchovu, na majeruhi, na kuwafanya waelekeze nguvu zao zote kwenye ligi ya ndani.

- Mwenendo wa Simba SC kwenye mechi za ligi yetu ya ndani, matokeo yao kwa sasa sio ya kuridhisha.

- Ukubwa/upana wa kikosi cha Yanga SC, kocha wao angekuwa na uwanja mpana wa kuchagua wachezaji wa kuanza kila mechi ya ligi.

Lakini kutokana na wao kutinga hatua ya makundi, maana yake Nabi atalazimika kuwachezesha wachezaji wake wazuri kwenye kombe la shirikisho, na wakati huo huo awachezeshe kwenye ligi kuu ya NBC akiogopa kutowapanga halafu aje kuumbuliwa na timu pinzani za ligi yetu ya ndani.

Nieleweke vizuri, sisemi Yanga SC hawezi kuwa bingwa wa ligi ya ndani, lakini naamini kushiriki kwao kimataifa kutawapunguzia kasi ya ufanisi kwa ligi yetu kwa namna moja au nyingine, hivyo nawatakia wanachi safari njema mfike nusu fainali ya kombe la shirikisho, kwani kutolewa chini ya hapo mtakuwa mmeliangusha taifa.

Hongera zako hatuzipokei ila tunachokuahidi ni kuendeleza utamaduni wa kutembeza vichapo iwe ndani ya nchi na hata nje ya nchi
Team ya wananchi
 
Back
Top Bottom