denooJ
JF-Expert Member
- Mar 31, 2020
- 18,509
- 68,228
Salaam.!
Nisiwe mchoyo wa pongezi, nawapongeza Yanga SC kwa ushindi wao walioupata jana wa goli 0-1 dhidi ya waarabu wa Club Africain ya Tunisia uliowawezesha kuingia hatua ya makundi ya kombe la shirikisho.
Pongezi zangu zinachagizwa zaidi na historia waliyokuwa nayo Yanga SC kushindwa kuingia hatua ya makundi ya makombe ya CAF toka mwaka 1998, kuuvunja mwiko huu ni hatua kubwa kwao.
Pia, nafurahi zaidi kwa sababu naamini, kama Yanga SC ingetolewa jana , maana yake ingechukua ubingwa wa ligi kuu ya NBC kwa mara ya pili mfululizo tena kwa urahisi zaidi, kwasababu;
- Wasingekuwa na mashindano ya kimataifa ya kuwasumbua hivyo wachezaji wao wangeepuka uchovu, na majeruhi, na kuwafanya waelekeze nguvu zao zote kwenye ligi ya ndani.
- Mwenendo wa Simba SC kwenye mechi za ligi yetu ya ndani, matokeo yao kwa sasa sio ya kuridhisha.
- Ukubwa/upana wa kikosi cha Yanga SC, kocha wao angekuwa na uwanja mpana wa kuchagua wachezaji wa kuanza kila mechi ya ligi.
Lakini kutokana na wao kutinga hatua ya makundi, maana yake Nabi atalazimika kuwachezesha wachezaji wake wazuri kwenye kombe la shirikisho, na wakati huo huo awachezeshe kwenye ligi kuu ya NBC akiogopa kutowapanga halafu aje kuumbuliwa na timu pinzani za ligi yetu ya ndani.
Nieleweke vizuri, sisemi Yanga SC hawezi kuwa bingwa wa ligi ya ndani, lakini naamini kushiriki kwao kimataifa kutawapunguzia kasi ya ufanisi kwa ligi yetu kwa namna moja au nyingine, hivyo nawatakia wanachi safari njema mfike nusu fainali ya kombe la shirikisho, kwani kutolewa chini ya hapo mtakuwa mmeliangusha taifa.