Hongereni Azam Media kwa kuendelea kuongeza thamani ya Ving'amuzi vyenu.

Hongereni Azam Media kwa kuendelea kuongeza thamani ya Ving'amuzi vyenu.

Wakuu Salaam.

Binafsi napenda kuwapongeza Azam Media kwa kuanza kuonyesha UK FA competitions, naamini taratibu mtatuletea UCL, EPL ili na sisi ambao bado hatijafika viwango vya kumudu DSTV tuweze kupata burudani pendwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Unahisi yakija hayo ma EPL NA UCL bado bei zitakuwa hizohizo za vifurushi
 
Na sasa wameongez ile channel ya KFS na imani kuna baadhi ya mechi za ligi kuu ya uingereza tutakuwa tunaziona live kupitia channel hii...
 
kuonyesha EPL na UCL ni gharama sana sidhan kama Asam watafikia hizo gharama
 
Wakuu Salaam.

Binafsi napenda kuwapongeza Azam Media kwa kuanza kuonyesha UK FA competitions, naamini taratibu mtatuletea UCL, EPL ili na sisi ambao bado hatijafika viwango vya kumudu DSTV tuweze kupata burudani pendwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Azam Walipaswa kwanza kuongeza channel zao za michezo. Wamejibebesha mizigo mingi halafu channel zenyewe za michezo ni chache. Mfano kuna mechi za ligi kuu Tanzania bara zinaendelea lakini wanashindwa kuzionesha kutokana na muingiliano wa michuano mbalimbali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kuonyesha EPL na UCL ni gharama sana sidhan kama Asam watafikia hizo gharama
Unahisi bei wanazotoza dstv kwa ajili ya kifurushi chenye premier league na uefa champions league(169000)ni sahihi kabisa?Kwamba hiyo bei ni sawa au wanapiga sana?Na unadhani azam wakirusha the same competitions kwa labda kwa 50000 hawatapata wateja?

Hao dstv wanalindwa sana na serikali ili mwananchi akamuliwe kuona hizo mechi lakini bei zao ni hatari sana na mtanzania wa kawaida ambaye azam wanamwangalia,hawezi kulipia hiyo kikawaida....labda kwa biashara ya vibanda umiza au baa.Usishangae akitokea mtu wa kurusha hizo mechi kwa bei za kitanzania halafu akawekewa zengwe na serikali ili tu kumlinda bepari dstv.
 
Back
Top Bottom