Hongereni Chadema kwa kufanikisha maandamano, ninaomba mpokee ushauri wangu

Hongereni Chadema kwa kufanikisha maandamano, ninaomba mpokee ushauri wangu

Polisi wameandamana kwa niaba ya Chadema na kufikisha ujumbe kuwa CCM inaatumia mabavu ya vyombo vya dola kukadamiza upinzani ili iendelee kutawala.

Chadema hakiamini kuhusu demokrasia, kinahubiri mambo kisiyoyaishi kihalisia. Kinakua too personal kwa maana ya yeyote au chama chochote kinachotoa mtazamo tofauti na wa chadema, hicho chama kinabandikwa jina na kuitwa CCM B sababu kina-back up mawazo ya ccm.

Chadema kinaunga mkono unyimwaji wa ruzuku kwa vyama vingine vya siasa, isipokuwa tu mpaka vipate mbunge au kura nyingi za mgombea urais. Hizi ni sera za ccm kuhakikisha vyama havikui na hivyo kuua demokrasia. Je chadema hapo kinakua ni CCM C??

Hizi mambo za personal ndio zinafanya kila ajenda inayoibuliwa kuonekana ni ya kichama (wanachama) na sio ya kitaifa (wananchi). Wasikilize ushauri wako au la utaendelea kuwa mchezo wa paka na panya.
Hakika, Chadema haina public trust kwa sababu Ndani yake kuna mambo mengi ambayo CCM are proving to public kuwa hiki sio chama bali ni tawi la familia


Ni lazima tujitunze kuukubali ukweli ili tuwe bora. And it is not so easy kuiondoa CCM kwa structure ya Chadema ya sasa na agenda zenu muhimu zote hazitoweza kuwa na public trust kwasababu huwezi kuubiri usafi wakati wewe huoneshi usafi.

Binafsi natamani Chadema iwe bora maana ndio chama pekee chenye uthubutu but kama chadema ikiendelea kubaki jinsi ilivo bila ya kusikiliza…….. basi njia iliyopita CUF na Chadema itapita na mbowe na kuna Lissu wote watakuwa kama Lipumna, Cheyo na wengineo
 
Wananchi wapewe elimu ya uraia na wakielimika watafanya maamuzi wenyewe. Hata yale yalikuwa maombolezo kuhusu watekaji na wauaji na watuhumiwa kwa mujibu wa Chadema ni vyombo vya Dola na uchunguzi unafanyika kupata ukweli.
Sahihi, unless chadema wameridhika na ruzuku
 
Polisi wameandamana kwa niaba ya Chadema na kufikisha ujumbe kuwa CCM inaatumia mabavu ya vyombo vya dola kukadamiza upinzani ili iendelee kutawala.
Hii haina msaada bila Action na uthubutu

Na uthubutu hauwezi kuja bila public awareness , na uthubutu wa kweli ni katiba mpya ….. mengine yote yatajiset
 
Umejaribu kueleza mapungufu ya Chadema lakini core reason hujipata!
1. WATANZANIA TU WAOGA! TUNAOGOPA KUFA!

2. Sasa tufanyeje ili tuache uoga. Ukipata jawabu la hilo swali, then andiko lako utakuwa umelikamilisha by 100%.

3. Issue ya umri, kubadirisha viongozi hayo ni mambo ambayo yanaweza kufanyika baada ya kuwaondoa wananchi woga. Huwezi ku disturb uongozi wa juu katika hali ambayo serikali inatumia billions kuhonga wapinzani! Utaweka akina Mwambe !

4. Msikiliz huyu
Ndugu shida kubwa Chadema tupo reactive hatutaki kusikia madhaifu yetu


Wa Tanzania sio waoga ; bali watanzania hawana awareness ya kile mnachotaka kukifanya na je mnataka ku achieve nini as a long term goals ?

Not so easy mtz aache kwendq kutafuta ugali wa watoto akajiunge na Samia must go ! That is absurd

Ili muweze kusema mtanzania ni muoga , ni lazima kwanza mjisafishe na muwe na organization yenye public trust , kisha mtengeneze main objective yenye public interest, kwangu mm ni katiba mpya, kisha mfanye awareness kwa public , mkiwa serious tunawatafutia
Fund, baada ya awarenes, leteni maandamano yenye long term achievement for public interest…. See the output .

Otherwise tuendelee kuamini kuwa ipo siku God will do it ! na hamtokuwa na tofauti na wale wanaomsubiri Yesu arudi.
 
Chadema hawasingiziwi kwenye ukabila...

Ni wakabila na wakanda wa ajabu sana...

Na hawana hoja zaidi ya matusi so usitegemee mabadiliko...
 
Sahihi, lakini Slogan ya Samia must go , was it realistic ?Ule ilileta taswira ya kukosa main objective and was of more chadema agenda na sio public .

The most important thing that we must learn to accept ni Chadema ku focus kwenye Cut off point yaani ile point ambayo ukisolve factor moja unakuwa ume solve problem zote.

It is time now Chadema ianze na long term strategy ya kuweka maandamano ya kudai katiba mpya. Ifahamike kuwa hakuna mwenyekiti wa CCM atakae kuja kuweka katiba mpya unless by push and force .

JK alipojaribu kina Ben walitaka kurudisha kadi na kumsusia chama. Magufuli alisema wazi not my agenda, na yoyote aliyejaribu kudai alitobolewa.Samia nae alisema not her agenda . Hakuna Rais wa CCM atakaepitisha katiba ya warioba , kufanya hivo ni kuondoa maslahi yao, it will never happen

Kuweka maandamano ya aina yoyote bila long term strategy , yaani mnataka kuachive matokeo ya kuitwa ikulu na kupewa bahasha za kaki na mpige story na Rais ? au mnataka kuleta ukombozi ?

Hamuwezi kupata ukombozi bila katiba mpya, that is naked truth .

Tupo tayari ku mobilize fund behind our scenes kwa ajili ya intensive sensitization kwenye public awareness ya kwanini tunataka katiba mpya, baada ya sensitization ndio tuanze kufanya maandamano ya ni lazima tuwe na katiba mpya ndio tufanye uchaguzi. This gesture , haitokuwa ni kwa benefit ya CHADEMA Ila ni kwa public interest ikiwemo CCM na hao mapolisi wenye hali mbaya ya kimaisha with salary of 700K.

90% ya viongozi wa CCM waliopinga katiba mpya wapo mavumbini, na hawana msaada tena. Hivyo tusipokuwa awake, hii cycle will never end till our deaths.

Generation zetu zitaendelea kuugua ugonjwa wa CCM na kutawalia na wahuni till their deaths, generations zetu zitaendelea kubaki kwenye poor quality of life huku failures wa shule kama kina Abdul, Riz na watoto wa viongozi with no history of our country wakitafuna national cake all alone and imposing conditions kwenye maisha yetu.

Nashauri Chadema mjisafishe kwanza na muweke long term strategy. Honestly you will have our support financially na kimawazo. Otherwise mnapigana vita bila ya kujua what is your long term output , CCM itawa outsmart eneo hili. Vita yoyote bila Strategy ya maana, ni kupoteza resources na muda
Yeah!...kwa andiko hili ina maana wananchi hawataweza kudai katiba mpya bila kuongozwa na chama cha siasa/upinzani (Chadema), hii ni ngumu kumeza ila lina ukweli.

JokaKuu Pascal Mayalla Mag3 zitto junior Mzee Mwanakijiji
 
Uliyoandika mbona CDM wamefanya yote?
1. Kususia uchaguzi
2. Kudai katiba mpya
3. Ku recruate kutoka chuoni. N.k

Jipya uliloongea ni kuwa wewe upo majuu unaweza ku support kwa ku mobilize wazungu.
Nasema tena , na Kama umesoma kwa ufahamu. Chadema haina public trust na haina long term strategy. Kwa mfano term limit kama ilivo kwa CCM , usiichukulie powa inaharibu reputation
Ya Chadema kwenye public

Ishu ya ukabila, hata kama chadema haina ukabila…. Ni matope tu , but inaondoa trust kwa public, you must work on it

Huwezi kuubiri usafi wakati sisi tunakuona unanuka kisha ukataka tukuamini, not easy

Also , kudai katiba bila public awareness ni waste of time , zipo research za Twaweza zinaonesha only 12% ya TZ population ndio wanaelewa umuhimu wa katiba. Na Hawa ni wale wenye kujihusisha na siasa . Imagine , more than 80% hawajui umuhimu wa katiba , sasa think unaenda ku achieve nini ?
Hayo uliyoandika Chadema imeyafanya mindless bila ya strategy , ni sawa na kuwa na jeshi lenye vifaa vingi na wanajeshi wengi but hamna Strategy ya maana …….. wanajeshi wote watauliwa na jeshi dogo tu

Chadema you must learn to listen na muwe Strategically as well as you make sure kuwa you are clean , otherwise mtakuwa na mindless demonstrations yasiyokuwa na output yoyote ya maana ;

Chadema sio ya kwanza kufanya hayo mambo ya reactive responses , CUF ilifanya sana na kwa sasa ipo juu
Ya mawe. Angalie msipite njia ya CUF
 
Chadema hakiamini kuhusu demokrasia, kinahubiri mambo kisiyoyaishi kihalisia. Kinakua too personal kwa maana ya yeyote au chama chochote kinachotoa mtazamo tofauti na wa chadema, hicho chama kinabandikwa jina na kuitwa CCM B sababu kina-back up mawazo ya ccm.

Chadema kinaunga mkono unyimwaji wa ruzuku kwa vyama vingine vya siasa, isipokuwa tu mpaka vipate mbunge au kura nyingi za mgombea urais. Hizi ni sera za ccm kuhakikisha vyama havikui na hivyo kuua demokrasia. Je chadema hapo kinakua ni CCM C??

Hizi mambo za personal ndio zinafanya kila ajenda inayoibuliwa kuonekana ni ya kichama (wanachama) na sio ya kitaifa (wananchi). Wasikilize ushauri wako au la utaendelea kuwa mchezo wa paka na panya.
Hao wananchi wao huwa hawawezi kuanzisha ajenda zao za kitaifa zinangoja kuanzishiwa tu na vyama vya siasa?
 
kwa wao kujinasibisha na chagadema yan sina ham nao. naona tunavopata tabu ofisn dili zote wanajipa wao wachaga wkwa wachaga
 
Yeah!...kwa andiko hili ina maana wananchi hawataweza kudai katiba mpya bila kuongozwa na chama cha siasa/upinzani (Chadema), hii ni ngumu kumeza ila lina ukweli.

JokaKuu Pascal Mayalla Mag3 zitto junior Mzee Mwanakijiji
Sahihi

katiba mpya ni lazima iongozwe na kuwa initiated na strong political party nchini. Na strong political party ni CHADEMA tu na ndio kina watu wenye uthubutu. But wapinzani wao ambao ni CCM , kuna namna wanatembea na weakness za chadema na kuharibu trust ya public . Hivyo ili ku gain public trust, Chadema must ifanye baadhi ya mambo.

Ni lazima Chadema ifanye reforms na mabadiliko kwanza ndani ya Chadema ili public ije kuamini, kuwa these people wanamaanisha

We can support chadema to mobilize funds kwa ajili ya sensitization tupate angalau 50 % ya wa Tanzania wawe na awareness ya katiba and as to why we need constitution reforms .

Otherwise ni kupigana vita huku una silaha but huna strategy. The bottom line , there is no way Chadema itashika nchi na katiba iliyoundwa kwa masilahi ya CCM , it is waste of time na resources to believe that
 
Police wangekaa pembeni na kulinda maandamano ya CHADEMA am sure ungeona uhalisia mwingi zaidi

Watanzania ni waoga.

NI kweli kama wangeechia Mbowe aanze kuandamana .... naamini picha ingekuwa tofauti kabisa.

Ila ushauri wangu kwa Chadema, waaitishe maandamano mengine next week na wafanye hivyo continuously kila baada ya week wawachoshe Police. Hao police wasipolala siku mbili tu wanaishiwa nguvu.

Pia kuna udhaifu mkubwa umeonekana kutoka jeshi la police. Jamaa hawana vifaa vya kutosha. Wana magari machache sana kufanya hiyo kazi. Sidhani kama Chadema wangetokea 1000 mtaani wangeweza kuwamudu unless kwa kutumia silaha za moto.
 
Na huo ndo ukwel wenyewe
kwa wao kujinasibisha na chagadema yan sina ham nao. naona tunavopata tabu ofisn dili zote wanajipa wao wachaga wkwa wachaga
Binafsi silioni hilo, na Kama lipo basi ni lazima wajisafishe otherwise ni waste of time

Issue ya uchaga ni useless , Chaga ni kabila dogo na lenye watu wachache sana , it cannot even make 1.5% of the total population.! Ni kukosa utimamu wa akili kuamini kuwa only wachaga they can make it alone

Aidha, sio kila mchaga ni Chadema. My parents ni wachaga and they have been CCM maisha yao yote, my father alinipatia mpaka kadi ya CCM and he is always insist , CCM is the way to life na future , hao chadema chauma cuf Act ni waganga njaa na hakuna future huku, but haya ni mawazo ya watu wa zamani
CCM haijawqhi kuwa future .
Ishu ya kupendeleana kwa ofisi sio tu kwa wachaga, Wasukuma did the same , Jk did the same , Samia is doing the same ,hiyo no hulka tu ya wa afrca
Ukabila wa CHadema umejengwa na CCM just as udin wa CUF ilivojengwa na CCM

kuamini kuwa wachga ndio Chadema sidhan kama ni sawa , they are less than 1% of the total population , inawaso wachache sana
Kabila pekee la kuohopwa ni kanda ya ziwa , wanawasomi wengi, wanapenda kusoma na population yao ni kubwa lakini bado pamoja na hilo , they can’t make alone

Chadema hili eneo la ukabila msipo jisafisha HAMTOBOI na soon mtaenda kuwa kama CUF , mbowe is getting old na lissu as well
 
Watanzania ni waoga.

NI kweli kama wangeechia Mbowe aanze kuandamana .... naamini picha ingekuwa tofauti kabisa.

Ila ushauri wangu kwa Chadema, waaitishe maandamano mengine next week na wafanye hivyo continuously kila baada ya week wawachoshe Police. Hao police wasipolala siku mbili tu wanaishiwa nguvu.

Pia kuna udhaifu mkubwa umeonekana kutoka jeshi la police. Jamaa hawana vifaa vya kutosha. Wana magari machache sana kufanya hiyo kazi. Sidhani kama Chadema wangetokea 1000 mtaani wangeweza kuwamudu unless kwa kutumia silaha za moto.
Watu mil 2 tu wanadhibiti hao polisi, kwanza wengi ni Vito to vidogo kwa umbo , havina hata miili, ukivipiga vibao tu unapokonya dilata zao . But as I Said kibali cha wananchi ni muhimu , Chadema alone will not be able . Tumzjifunzq jeshi la polisi hakika ni dhaifu
 
Hao wananchi wao huwa hawawezi kuanzisha ajenda zao za kitaifa zinangoja kuanzishiwa tu na vyama vya siasa?
Wanaweza. Ila kwa mujibu wa Sheria zetu za uchaguzi na za vyama vya siasa, ili ufanye jambo lihusulo siasa na serikali, ni lazima uwe na mwamvuli wa u-chama, yaani uwe mwanachama wa chama fulani cha siasa.

Mpambanaji Hayati Mchungaji Christopher Mtikila alipinga sana hii dhana kwa kupambania uwepo wa mgombea binafsi, ili kuruhusu mtu yoyote kupata jukwaa la kuzungumzia agenda za nchi bila kulazimishwa kuwa mwanachama wa chama cha siasa. Ajabu na yeye aliishia kuvuliwa uanachama na chadema haohao
 
Kupitia maandamano, kwamba tumejifunza hatuna jeshi la polisi lenye uwezo wa kudhibiti watu 5Mil tu walioamua kutafuta haki yao.

Ili kufanikisha maandamano ya watu mil 5 tu , ni lazima Chadema mtengeneze main Objective ambayo ndio tatizo kuu la Tanzania na hiyo Objective itamgusa kila mwananchi.

Ninaomba kushauri yafuatayo;

1. Slogan ya Samia Must go was a reactive response and inadequate strategy.

Ili kuboresha hili eneo ni lazima mkae chini na kutengeneza long term na short term strategy za kuikomboa nchi kutoka katika ugonjwa unaoitwa CCM.

Long term strategy ambayo inaweza kuja to capture attention ya kila raia ni kutofanya uchaguzi au kususia uchaguzi kama hakutokuwa na KATIBA ya Warioba hii itaendana sambamba na maandamano ya kudai katiba mpya.

Maandamano ya katiba mpya yatakuwa ni ya wananchi yaliyokuwa mobilized na Chadema. Shida zote za Tanzania pamoja na kupata viongozi kama Samia, the root cause ni Katiba na hii ndio cut off point. Katiba hii ilituletea Magufuli. Kilichotokea kwa Magufuli na kwa sasa Samia, katiba Mpya becames mandatory for the welfare of the country.

On the other hand, ili Chadema mfanikishe hili swala, kuna namna mnatakiwa kujiboresha kwanza nyie ili wananchi wawe na trust kwenu ;

2. CUF ilipakwa matope ya Udini, those days CUF ilikuwa ndio strong party baada ya CCM , it was intimidating, wananchi wakaamini kweli CUF ni udini, ngangari ngangari , wazee wajino kwa jino . Where is Lipumba now?

Chadema mmepakwa matope ya Ukabila, CCM knows better how to analyze the areas of weakness na kuzifanyia kazi.Ni lazima mjisafishe na haya matope kwa gharama yoyote. Otherwise, mbowe na Lisu are getting old and older, they will tired na watapotea just as Lipumba , Seif na CUF yao.

3. Nafasi ya Mwenyekiti na Naibu wake ni lazima iwe na time limit of maximum 10 years na kufanya transition ya hizo nafasi to younger generation, only then , mta develop public trust. May be katiba ya Chadema iwe reviewed na kufanyiwa amendment na addendum.

4. Kufanya makongamano na sensitization ya kutoa elimu kwa Raia umuhimu wa katiba mpya hadi kwenye remote areas, lazima muwe na kitengo maalum cha hii kazi, na kama tatizo ni fund , watu waliokuwa huku majuu tunaweza kufanya mobilization kwa wazungu na wakatoa hela to support hizo activities, only then , mkija ku announce maandamano ya kudai katiba mpya, you will make sense.

4. CUF ilikufa kwa kukosa vijana wenye uwezo, Lipumba alipo zeeka, CUF nayo ikazeeka; Chadema mnatakiwa kutengeneza vijana watakaofanya replacement za mbowe na lissu na wengineo. Mnaweza mkawa mnachukua cream za vyuoni na kuwajengea uwezo hao vijana waje kuwa kina lisu na mbowe wa baadae

Kuitoa CCM bila katiba mpya, it is totally impossible, na CCM wanapoona mnautaka ugali wao , wataulinda kwa kutumia polisi na kusema maneno kama tusiwasikilize wanaotaka kutugawa kisiasq. Kwa CCM, kudai haki yako ni kutaka kugawa watu kisiasa.

Kama kweli Chadema mnaitaka nchi; ni lazima baadhi ya maeneo mkubali kuyafanyia kazi ili mpate kibali cha wananchi. Lakini pia Bila katiba mpya itawalazimu kuwa na hizo reactive strategies za Samia must go ambazo kimsingi output yake ni Zero na inafanya muonekane you people are too personal, for own interest, and public will never support that .

Soma Pia:


Unasemaje kuhusu CDM mlipokuwa mnamuunga mkono Samia baada ya kumtoa Mbowe gerezani moja kwa moja ikulu na tangu siku hiyo vita, kejeli dhihaka ilikuwa dhiidi ya JPM mkakati wa Samia na CDM, maridhiano. Miaka mnasema lowassa ni fisadi kuu baadaye mnamchukua na kumsafisha.

Mliungwa mkono wakati wa Slaa mlipokuwa wakweli sasa hivi mnasaka tonge. Samia akiwapa ubunge nafasi 20 hivi, wizara mbili tatu, mtaanza kumsifia anaupiga mwingi. Tatizo ni washauri wake, Wasukuma, Sukuma gang.
 
Wanaweza. Ila kwa mujibu wa Sheria zetu za uchaguzi na za vyama vya siasa, ili ufanye jambo lihusulo siasa na serikali, ni lazima uwe na mwamvuli wa u-chama, yaani uwe mwanachama wa chama fulani cha siasa.

Mpambanaji Hayati Mchungaji Christopher Mtikila alipinga sana hii dhana kwa kupambania uwepo wa mgombea binafsi, ili kuruhusu mtu yoyote kupata jukwaa la kuzungumzia agenda za nchi bila kulazimishwa kuwa mwanachama wa chama cha siasa. Ajabu na yeye aliishia kuvuliwa uanachama na chadema haohao
Wananchi wao hawawezi kudai hiyo haki ya mgombea binafasi, wao wanasubiri wanasiasa wawaombee tu?!
 
Wananchi wao hawawezi kudai hiyo haki ya mgombea binafasi, wao wanasubiri wanasiasa wawaombee tu?!
Mtikila alipoiomba alifanya kama mwananchi wa kawaida (sio mwanasiasa). Alishinda kesi hiyo na hata Rasimu ya Warioba ilikua inapendekeza uwepo wa mgombea binafsi, maana yake ni kuwa wananchi walipendekeza hilo. Kwenye kudai sasa ndio wanalazimishwa kuwa ili wafanye mikutano au maandamano basi lazima wawe wanavyama wa wa vyama vya siasa
 
Back
Top Bottom