Hongereni Chadema kwa kufanikisha maandamano, ninaomba mpokee ushauri wangu

Kuna mantiki katika uliyoandika hapa. LAKINI hili si jawabu.

Siku zote CCM na wasiotaka mafanikio ya CHADEMA wanafanya propaganda zote kuvuruga ajenda na mwelekeo wa chama hicho. Na kwa vile njia pekee ya uhakika ya kupima kukubalika kwa CHADEMA kwa wananchi ni kupitia sanduku la kura njia ambayo serikali ya CCM imehakikisha haifanikiwi, propaganda hasi zinaonekana ndio ukweli kuhusu CHADEMA.

Kwa hiyo ili kuboresha taswira yao kama unavyopendekeza, CHADEMA wanaweza wakijikuta wanahangaika muda wote “kujirekebisha” kuondoa “kasoro” wanazodaiwa kuwa nazo kila zinapotolewa: udini, ukabila, ukanda, ubinafsi, udikteta, ukibaraka, n.k. Endless, futile, uphill struggle.

Pamoja na umuhimu wa “taswira sahihi” naona CHADEMA hadi sasa wameshafanya ya kutosha katika mazingira magumu sana ya kisiasa tuliyo nayo tena wamelipa gharama kubwa sana. Kama wananchi wameshindwa kabisa kuwaelewa, basi tatizo ni kubwa zaidi ya kuwa na vyama makini vya upinzani.

Hitimisho ni kwamba Watanzania bado hawahitaji au hawako tayari kupigania mabadiliko ya mfumo wa uongozi na siasa za nchi hii.

Hali iliyopo (STATUS QUO), ni himilivu: inakubalika au inavumilika kulinganisha na gharama ya kuibadili. Bado hatujafikia brink point. CHADEMA wanaweza kukubali ushauri wa kuendelea “kujiremba” zaidi lakini wasiambulie kitu.

Hivyo, tuvute subira. Siku ikifika, Wananchi wenyewe watachukua hatua, iwe ni kwa kupitia CHADEMA au mwanaharakati binafsi au hata ghafla tu (spontaneously).
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…