Hongereni first year (ba-ed) at udom.

Hongereni first year (ba-ed) at udom.

Maige Maro

Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
15
Reaction score
1
baada ya kimya cha mda mrefu cha tcu hatimae wametoa majina ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza kwa vyuo vyote.Kwa wale wa BAED UDOM karibuni sana.

kuhusu BAED
Wanafunz wa BAED walihamishwa kutoka college of education kwenda college ya social science&humanities.Lengo la kuhamishwa ilikua ni kuboresha course ya BAED kwan baed msingi wa degree yao ni arts na sio education,hivyo course nyingi za baed ziko humanities.

JINSI YA KUCHAGUA MASOMO YA KUFUNDISHIA
BAED wapo chini ya idara ya arts media and design ambapo mwanafunzi atakua huru kuchagua masomo yoyote anayotaka ila moja ya masomo hayo liwe major na lingine minor.kwa mfano unaweza kuchukua liguistics kama major naliterature kama minor.masomo mengine ni acting kwa wale waigizaji,vidio production,kiswalili,history,geo nk.


MAZINGIRA YA HUMANITIES

Mazingira ni mazuri ambapo kuna hostel za kutosha,msosi upo kwa bei ya kawaida sh 1000 wali maharage.kwa wale wanaotaka kushiba kuna mama ntilie pembeni msosi wa kumwaga.


CHANGAMOTO

Tofauti na pesa inayotakiwa na chuo jitahidi ubaki na pesa ya kutosha kwa matumiz binafsi,usitegemee boom kwan huwa wanachelewesha sana kiasi kwamba unaweza kujuta kuchaguliwa UDOM.vinginevyo karibun sana tulijenge TAIFA.










 
Thanx mkuu,kwan kama shiling ngp mwanafunz anaweza kuingia nazo hapo?wengne watoto wa makabwela
 
Back
Top Bottom