Hongereni Halmashauri ya Mji Bariadi kwa kulitengeneza gari hili la maji taka

Hongereni Halmashauri ya Mji Bariadi kwa kulitengeneza gari hili la maji taka

KwetuKwanza

Senior Member
Joined
Mar 13, 2023
Posts
127
Reaction score
245
1771567479872.IMG_20260220_085703_969.jpg
IMG_20260220_085328_985.jpg

Siku chache zilizopita kupitia Jukwaa hili, nilileta moja ya hoja kutoka kwenye Halmashauri yangu ya Mji wa Bariadi.


Hoja hiyo ilihusu gari la maji taka, pamoja na vifaa vingine kama gari la kubeba taka na mashine ya kuzoa uchafu (Greda).

Vifaa hivyo nilivikuta vikiwa vimepakiwa kwenye eneo la Hospitali ya Mji wa Bariadi baada ya kuharibika Kwa kipindi kirefu hasa gari la maji taka.

Gari Hilo ambalo lilinunuliwa Kwa Kodi za wananchi, lilipakiwa Kwa muda mrefu bila ya kutengenezwa huku wananchi wa Mji wa Bariadi tukiangaika kupata gari la maji taka.

Watu tulifikia kutafuta gari kutoka Mwanza, huku magari ya watu binafsi ya Mji wa Bariadi yakiwa na Bei kubwa.

Leo naleta mrejesho kuwa Nina wiki mbili hili gari naliona Barabarani tangu niandikie kuhusu kutelekelezwa.

Siyo hivyo tu, juzi limekuja kwangu na kutoa huduma, Kwa sasa gari kila siku linafanya kazi, na linaendelea kutoa huduma Kwa Kasi Kwa wananchi wa Mji wa Bariadi.

Napenda kutoa Pongeze kubwa Kwa Uongozi wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi Kwa kufanyia kazi kero hili na hatimaye huduma Kwa wananchi imerudi kama kawaida.
 
Jambo jema.
Liende sima,malambo, nyankokolwa,pia nyakabindi
 
Back
Top Bottom