Hongereni RFA kurejea kwa matangazo

Dah! Aisee!
Yaani huwezi amini katika hiyo list waliopo ni 3 tu, wengine wamehamia vituo vingine na wengine wamepumzika kwa amani.
 
Ukiacha TBC , RFA inakuza sana vipaji vya vijana na kuwapa ajira nje ya RFA, ndani na nje ya Tanzania
 
Sahara media wana tatizo la management hakuna kingine
Inawezekana- lakini hata wale wenye management nzuri wana matatizo ya ulipaji wa mishahara. Una kumbuka mtangazaji mmoja wa kike wa ITV Radio one alipokufa ndiyo michango yake ya hifadhi ya jamii na malimbikizo ya mishahara ikalipwa wakati wa mazishi yake tena wakati huo Mzee Mengi alikuwepo bado. JPM aliposhika uenyekiti wa CCM, radio uhuru na magazeti ya uhuru na mzalendo walikuwa na malimbikizo ya mshahara wa miaka 3. Jenerali ulimwengu kauza rai na dimba akafungua Raia mwema sasa amelikimbia kwa kumuuzia Kubenea anayeliendesha anavyojua mwenyewe. Ukitaka kumtukana mtu mpe kubenea 1m anakuandikia na kuchapisha unachotaka na gazeti linatoka.
 
Hii redio, Dialo angeikodisha tu, imeshamshinda kuendesha,, nadhani hapati matangazo ya kutosha, na hata kamari hailipi kivile, watu wamejanjaruka sana, awape chadema kwa mkataba maslumušŸ˜‚
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…