MdengestanfromCuba
JF-Expert Member
- Dec 26, 2012
- 629
- 658
Leo Uto mmejua kutufunga midomo tusiyowaombea mazuri, mmetisha sana🫡🫡. Kwenye mechi ya leo nimeona mambo kadhaa:
- Kilichowaangusha Waarabu ni dharau yao kwa Yanga, hii mechi wangeweza kuimaliza Taifa, kwani Yanga walikuwa goigoi kwenye first leg. Dharau hiyohiyo imewafanya leo wasiamini wanachokiona kwenye uwanja (Yanga walijipanga).
- Ushindi wa hii mechi tunaweza kumpongeza kocha sawa, ila nguvu kubwa sana imetumika na GSM kufuatia kelele za wananchi (ahadi ya m 500 kwa kikosi)!
- Yanga walishindwa kupata matokeo mechi ya nyumbani kwa sababu ya hofu, na wameweza kupata matokeo ugenini kwa sababu ya hofu!