Papi Chulo
JF-Expert Member
- Jun 8, 2018
- 6,260
- 7,395
- Thread starter
-
- #61
Wa-Kenya wao huwa hawaui Albno lakini. Nawasifu sana kwa hilo. Wahenga waliwahi kuimba wimbo unasema "Mtu chake apendacho, hakina hila moyoni, huridhika kuwa nacho japo hakina thamani." Halafu juzi tu Wa-Kenya hawa hawa wameturudishia pesa yetu nyingi sana iliwahi kuibiwa NBC Moshi, huko nyuma mwaka 2004, pamoja na dhahabu waliyoikamata Polisi wa Kenya Airport mwezi juzi mwaka huu. Bado tu wa-Kenya wanapondwa, tena na mtu m-Tanzania. Unajua nini, baadhi yetu sisi wa-Tanzania huwa ni wajinga sana!
Halafu ngoja nikupe tip hii: kwa uzoefu wangu mimi, M-Kennya na M-Tanzania wakikutana tuseme kwa mfano Ulaya, wasiowajua huwa hawawezi kuwatofautisha kuwa huyu ni M-Kenya na yule ni M-Tanzania. Huwa wanawaona kuwa aidha wote ni wa-Tanzania au wote ni wa-Kenya. Hadi mfikie hatua ya kuwajulisha kuwa yule ni M-Kenya na yue ni M-Tanzania. Ni kama walivyo wa-Malawi na wa-Zambia!
We mgeni humu eeehh???
Hatuna undugu na kenya sisi..!!