Hongereni Tanesco kutuletea Smart Meters, lakini mtatuunganishia bure ili kubadili zilizopo au tutalipia?

Hongereni Tanesco kutuletea Smart Meters, lakini mtatuunganishia bure ili kubadili zilizopo au tutalipia?

Idugunde

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2020
Posts
6,404
Reaction score
6,969
Hii habari ni faraja kubwa kwa watumiaji wa umeme maana sasa habari za kulala giza kidogo au kwa sana zitapungua maana hata ukiwa Songea safarini utaweza kununua umeme na kuwasha nyumba iliyopo Mwanza. Maana hakutakuwa na haja za kuingiza tokeni ili kuwasha umeme.

Lakini je, hizi mita zitabadilishwa kwa wateja wote? Na kama zitabadilishwe itakuwa bure au kwa gharama?
 
Tanzania kupewa cha bure utakisotea sana tena kwa gharama kubwa mfano kadi za nida. Hivyo hizo meters wauze tu kwa bei nafuu kuepusha usumbufu
 
Yakeyale tu hata ukinunua kama voucher unatuma tu namba nyumbani wanaweka na mgumo huu upo hata nchi zilizoendelea sana kama southafrica bado wanatumia voucher na umeme ni wa uhakika sasa sijui kama tunajitambua hv kweli kuna haja gani ya kubadili. Meter wkt umeme wenyewe hauna uhakika shughulika na tatzo kwanz la umeme hakuna aliye lalamika hzo voucher ila watu wanalalamika umeme kukatika sasa hapa ninujinga hapo watu wanapiga pesa za manunuzi zile percent zao unaambiwa mita ni sh 5000 wakt kanunua tsh 2000 badae wanaingiza 3000 ya boss kwa kila.kita js kwa Tz nzima bilioni kama si trilioni ngapi huyu jamaa mpigaji sana.
 
Haya Sasa July ishaisha Tanesco,hata dalili za hizo Smart meter hakuna.

Story story story
 
hizo meter zao mpya zanaitwa wasion zinasumbua sana kuweka token ni ovyooo hata hizo smart meter zitakuwa ovyooo hakuna kitu serikali inaleta kwa wananchi ikawa ni kizuri
 
Napendekeza hizo meters ziwe ni hiyari kuzifunga,

Wasilazimishe wanainchi kuzitumia..

Kwangu Mimi shida sio meter Bali umeme gharama za manunuzi ya umeme ni kubwa,
Washushe gharama za kununuwa umeme.

Waache blah blah
 
Back
Top Bottom