Hongereni Wabunge wa Mbeya ila msiishie hapo!

Hao ni wale wapuuzi waliokariri..Hao waache hivyo hivyo usiwastue ,nimesema kunguru mwingine akisema eti Mbeya hawajengi nyumba za kisasa nikaishia kucheka tuu.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]wapuuzi hao mbeya vijana Wana uchumi mkubwa sana na ndiyo sehemu kununua nyumba barabaran sikuhiz kama huna million 150 kupanda juu kupanda eneo barabarani ni ishu watu wanajenga majumba ya kifahari iwambi huko ,ivumwe huko na kwingine afu anatokea mjinga mmoja anasema sijui Nini

Mbeya adui wetu ni serikali wao wenyewe wanakwamisha sana maendeleo na kipind cha kikwete ndiyo ilikuwa hatari hujuma tulizofanyiwa hata Leo hii uwanja wa songwe ingekuwa haupo lakin wazee wetu wakina mwandosya walipambana sana na akina mwakyembe kama mnakumbuka hata kuanza kurusha ndege ulianza ukiwa hauna hadhi Ile ambayo nchi za SADC walipanga iwe kikwete na akina lowasa walifanya figisu sana had leo ule uwanja hauna ile hadhi iliyotakiwa lakin lengo ilitakiwa uwe mkubwa ili uweze kusadia kuhudumia mataifa ya ukanda ule lengo ni kuongeza biashara na uwekezaji
 
Kijana hapo Mbeya hakuna la maana hapo! Kuhusu kufanya biashara ya mitumba mpaka S/Africa wala sio tija! Hao vijana ni wangapi katina watu wa hapo Mbeya? Mbeya mnauanaharakati mwingi lakini matokeo zero!
 
Kikwete nae aliwahi kupopolewa na mawe na BANYAMBALA; toka hapo yeye na hao watu ni paka na chui!!! Aliamini walikuwa wanamdharau kwa uwezo wake mdogo.
Na Magufuli hivo hivo wanamrishia mawe wakijua wanae Rais wao Sugu! Acheni ujuaji mtaendeleakiwa kijiji kikubwa! Sasanaona mnamtegemea Mama Samia na chawa wake Tulia hahahha
 
Yaani wewe ni mpuuzi hiyo mijengo yenu hata kuezeka tu hamjui nyumba hapo ulipopataja hakuna nyumba za maana hapo ila kwa level yako na upeo wako unaona ni nyumba za maana wakati ni ujinga ujinga tu! Kiwanja cha ndege Songwe hata abiria wa Bukoba ni wengi kuliko nyinyi kijiji kikubwa! Nenda hapo airport ukatazame abiria wengi wa wali ni Mwanza na kilimanjaro huko ndo kwa wanaume!
 
Ule mji wote wa Mbeya unapaswa kuvunjwa wote na kuanza kujengwa tena, nyumba zimejengwa hovyohovyo sana na mipangilio ya barabara haiko sawa kifupi ni moja ya miji ambayo ipo kiholela sana....ni kama kamji ka Goma pale DRC.....

Wakazi kuendekeza imani za kichawi na utakiri wa ndagu pia kwa kiasi kikubwa huchangia ile hali pale Mbeya.... Maana unakuta jitu linamiliki maduka na mali kadhaa lakini linaishi kama mganga wa kienyeji...Wakazi wake wengi wanachanganya dini na ushirikina aka uchawi, wanaona kama ni vitu viwili vilivyo sawa....wake up Mbeya..
 

unaposema maendeleo ni pamoja na kuwa na nyumba bora, nyumba bora ya kuishi binafsi haijengwi na serikali, inajengwa na mtu binafsi, sasa kwa tafsiri ya hicho unachokisema tungeona mijengo mizuri kila mahala hapo Mbeya...

Kuna wakati sio lazima serikali ipange mtaa, ila kama watu husika wa eneo husika wamestaarabika wanaweza kuupanga mtaa wao...
 
Kuna wakati sio lazima serikali ipange mtaa, ila kama watu husika wa eneo husika wamestaarabika wanaweza kuupanga mtaa wao...👊
 
Na Magufuli hivo hivo wanamrishia mawe wakijua wanae Rais wao Sugu! Acheni ujuaji mtaendeleakiwa kijiji kikubwa! Sasanaona mnamtegemea Mama Samia na chawa wake Tulia hahahha
Banyambala akili kubwa wewe kifuu; hawatakuwa chawa wa mtu hata siku moja!!
 
Asante kwa ushauri wako mkuu.mi ni mkazi wa Mzaliwa wa Mbeya nakubaliana kabisa na hoja yako kuwa tunajenga nyumba chini ya kiwango pia hatufuati mipango miji.Ila mi mkuu kwetu soko matola kumepangiliwa japo nyumba za kizamani.
Soko matola USHUANI pazamani..!!

#YNWA
 
Umesema ya kweli kabisa ndugu!

Penye uchawi/ ushirikina Hakuna maendeleo
 
Kijana hapo Mbeya hakuna la maana hapo! Kuhusu kufanya biashara ya mitumba mpaka S/Africa wala sio tija! Hao vijana ni wangapi katina watu wa hapo Mbeya? Mbeya mnauanaharakati mwingi lakini matokeo zero!
Kijana una uchungu wa mimba na chuki zisizojificha juu ya wazawa wa Mbeya, Hata kama kuna mahali wamekukosea hebu punguza masononeko!
 
Kama reference yako ni Mbalizi basi unapaswa kupimwa mkojo. Maana Mbalizi ni Mbeya vijijini. Kwa upande mwingine inafurahisha kuipima Mb vijijini na hiyo miji yako mingine.
 
Ngumu kumeza kila kitu, Hospital ya Mkoa wa Mbeya imejengwa from scratch na JK,hata ujenzi wa Mbeya-Chunya Road imejengwa awamu ya JK.

Kama Magufuli alitoa kibali na eneo la ujenzi wa Chuo mbona kila mahafari akija JK Mbeya huwa anaulizia eneo? Na akasema wakiendelea na danadana watahamisha chuo kwa mikoa iliyo tayari.

Mbeya hakuna cha bandari kavu iko tuu bandari pale,hata hivyo kiwanda cha TBL kile limejengwa awamu ya JK.

Upanuzi wa barabara ya Tanzam ukianza toka enzi za JK kule moro na Iringa,Magu ameifikisha Igawa..

Basi tuseme hakuna mtu wa kusema fulani alichukia au hakuchukia.
 
Hao ni wale wapuuzi waliokariri..Hao waache hivyo hivyo usiwastue ,nimesema kunguru mwingine akisema eti Mbeya hawajengi nyumba za kisasa nikaishia kucheka tuu.
Hao wanaotumia daladala hawawezi jua ukubwa na ubora wa Mby, maana ukianzia Uyole highway kuelekea Iyunga, unapasua Km zaidi ya 15 katikati ya jiji, inakuruhusu kuingia kulia au kushoto zaidi ya km 5 kila upande. Huko ndiko utajua kama Mb ina majengo ya ovyo au vp? Sasa wao wakipita high way tu basi. Sidhani hapa Tz kama kuna miji zaidi ya 3 iliyojengwa eneo kubwa kama Mb.
Hawa ni kama wanaopima ubovu wa DSM kwa kutumia Manzese. Hata DSM nje ya Masaki na maeneo mengine kama hayo kuna mchanganyiko wa nyumba mbovu na za maana, mfano Mikocheni kuna nyumba za ovyo ikiwa nyingine ni nzuri ajabu mpaka huwezi amini kama ni mji mmoja.
Kinachokosekana Mb ni majengo makubwa ya taasisi za umma. Lakini wananchi ni wapambanaji sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…