Etugrul Bey
JF-Expert Member
- Aug 6, 2020
- 6,514
- 15,247
Kwanza tupongezane sote kwa siku hii ambayo ni kumbukizi ya Uhuru ambao wapendwa wetu walipambana kwa jasho na damu mpaka leo hii tunajitawala na kuyaendesha mambo yetu kwa utashi na uhuru kabisa bila bughudha yoyote ile.
Ilikuwa ni ndoto ya waafrika wengi kutaka kuwa huru dhidi ya utawala wa kikoloni ambao ulikuwa na dhuluma na manyanyaso mengi sana,tumesoma katika historia madhila mbali mbali ambayo wapendwa wetu walipitia,lakini hatimaye Tanzania ikawa huru
Sasa yale mambo ambayo mkoloni aliyafanya kupunguza nguvu ya mwafika katika kudai haki zake kwa kupasa sauti yake yanaonekana kurudi tena kupitia kivuli cha Tanzania iliyo huru,je tumeridhishwa sana na amani tuliyo nayo kiasi kwamba tunaona amani si chochote tena?
Ndugu zangu watanzania ogopa sana mwananchi akishaona na kuzoea kuona vurugu na ghasia,hakika akishayazoea mambo haya mwisho wa siku inakuwa sehemu ya maisha yake,na hapo ndipo amani itaanza kutoweka hapa nchini
Wengi wetu ni mashahidi hii si hulka na tamaduni ya mtanzania,sisi ni wakarimu na wenye kupenda amani,hatupendi shari,na tunafurahia upendo ambao tunajivunia kama Taifa,mataifa mengine yanajivunia kwa mda mrefu utulivu ambao tumekuwa nao
Masuala yanayopelekea ukosefu wa amani nchini ya kupigwa vita na kila mtu kwani yanaweza kuligharimu taifa huko baadaye. Serikali na wenye mamlaka nawaomba sana tuchukue hatua madhubuti kukomesha hali hii kabla hatuja chelewa,tumeachiwa Tanzania salama na waasisi wetu hivyo isifike mahali juhudi zao na nguvu zao kwenda bure,naamini kabisa tutathamini na kuzienzi juhudi zao na kuliendeleza gurudumu hili kwa vizazi vijavyo.
Mungu ibariki Afrika na Mungu ibariki Tanzania
Asanteni kwa kunisikiliza
Ni hayo tu!