Eeka Mangi
JF-Expert Member
- Jul 27, 2008
- 3,173
- 482
Naaam leo hii,,, leo jioni Mgombea wa ubunge Moshi Mjini ndugu Salakana amepita kwenye baadhi ya maofisi na kugawa fedha. Mojawapo ni kampuni maarufu ya utalii hapa Moshi. Taarifa za ndani ya ofisi hiyo zinasema kuwa walipewa shs 2000 kila mmoja ila jamaa mmoja cha pombe aliyeanza kuongea pumba kwa mgombea huyo alipewa msimbazi moja. Sasa jamaa kahamia Njoro na Majengo ananunua mbege na dadii zote kwa wanywaji wote. Amini usiamini hafui dafu. Pia habari za sasa hivi mgombea mmoja wa udiwani ndg mangia amefunguliwa kesi ya kushambulia kwenye kituo cha kati cha polisi kwa kumshambulia kiongozi mmoja wa Chadema.
CCM bye bye Moshi hawakubaliki. Kesho naja na za JK moshi maana anakuja tena huku.
CCM bye bye Moshi hawakubaliki. Kesho naja na za JK moshi maana anakuja tena huku.